Kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi la Rwanda sasa ni Imani yangu Jeshi la Polisi la Tanzania litaimarika zaidi na kubadilika kiuweledi

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,548
108,882
IGP Sirro umeona mbali sana na GENTAMYCINE nakupongeza kwa Kuomba 'Ushirikiano' wa Kiuzoefu na Kiuweledi kutoka kwa Jeshi bora la Polisi Afrika la Rwanda nchi iliyobarikiwa kama ilivyobarikiwa nchi ya Israeli.

Kwakuwa IGP Sirro wa TP ameanza nawaomba na akina Msuya wa SSIT na Mabeyo wa ZTWJ nao wasione 'aibu' kuomba kupata 'Ushirikiano' wa 'Kiujuzi' na Taasisi kama zao zilizoko nchini Rwanda (Israeli ya Afrika)

Na hata Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan jitahidi sana uwe karibu 'Kiushirikiano' na Rais wa Rwanda 'Shujaa wa Uchumi, Teknolojia na Maendeleo' Mheshimiwa Paul Kagame.

Na Watanzania wote ipendeni Rwanda.
 
Hao Rwanda wamepata wapi huo weledi?

Je, ina maana watanzania hawana ubunifu wao wenyewe mpaka wategemee akili za jirani yao?

Tatizo siyo hayo wanayotaka kuambukizwa na Rwanda, ila ni uvivu wa kufikiri, huyo PGI ndiye mvivu wa kufikiri na kuja na ubunifu, hao Rwanda hawakuzaliwa na huo uzoefu, ila wameishughulisha akili yao wakaja na hayo tunayotaka ku copy na ku paste.

Kwanini nasi tusitumie watu wetu wa ndani tukafanya mambo ambayo Rwanda watajifunza toka kwetu?
 
Tanzania ikifuata weledi haina cha kujifunza kutoka kwa hizo nchi
 
zero brain wewe, shujaa wa uchumi mita kadhaa kutoka mji wa kigali nyumba kibao za matope na barabara za vumbi, ujuzi gani rwanda walionao wakashindwa kulinda amani ya rwanda?
Yote haya yapo Burundi na siyo Rwanda.
 
tanzania ndiyo inayoisaidia rwanda kama kama tunapowasaidia majirani wengine ingawaje wanajawa na viburi
Tanzania inafaidika kwa Akili kubwa za Wanyarwanda na bila shaka mtafaidika mno na kuondokana na 'Uswahili Uswahili' wenu unaowachelewesha Kimaendeleo mpaka Rwanda inawazidi tu sasa.
 
zero brain wewe, shujaa wa uchumi mita kadhaa kutoka mji wa kigali nyumba kibao za matope na barabara za vumbi, ujuzi gani rwanda walionao wakashindwa kulinda amani ya rwanda?
Huyo sio ziro huyo Ni sifuri kabisa naona akihama kwa shemeji yake atakuwa na akili.. Siro huyu mwanasiasa aliyesaidia kuharibu uchaguzi au yupi hao wote lazma waondolewe muda Ni mwalimu

Jeshi limejaa wala rushwa mwenye jeshi yupo bize kukimbizana na akina Mnyika na Jacob..
 
Hao Rwanda wamepata wapi huo weledi?
Je ina maana watanzania hawana ubunifu wao wenyewe mpaka wategemee akili za jirani yao?
Tatizo siyo hayo wanayotaka kuambukizwa na Rwanda, ila ni uvivu wa kufikiri, huyo PGI ndiye mvivu wa kufikiri na kuja na ubunifu, hao Rwanda hawakuzaliwa na huo uzoefu, ila wameishughulisha akili yao wakaja na hayo tunayotaka ku copy na ku paste.
Kwanini nasi tusitumie watu wetu wa ndani tukafanya mambo ambayo Rwanda watajifunza toka kwetu?
Tanzania inaihitaji Rwanda ( tena hasa kwa Akili zao kubwa walizobarikiwa nazo na Mwenyezi Mungu ) kuliko ambavyo Rwanda inaihitaji Tanzania yako ( yenu ) sawa?
 
Back
Top Bottom