Kwa kuliokoa Taifa letu la sasa lenye Vijana 'Nyoro Nyoro' wengi naomba Mafunzo ya JKT yawe ni ya Lazima

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,741
109,177
Utakuwaje na Taifa lenye Watu Shupavu ( tena kwa Vijana ) kama unakutana na Kijana wa Kiume kapanda DalaDala kutoka Makonde Mbezi Beach na anashukia Kituo kinachofuata cha Goigi huku akijiona ni Mjanja?

Nilikuwa najiuliza sana tu ni kwanini Vijana wengi wa Kiume Siku hizi ni Wavivu, hawapendi Shuruba ( Taabu ), wanapenda Kujiremba na kufanyiwa Scrub na Massage huko katika Masaluni, wakiongea wanabana Sauti, wanapenda Kujilambalamba Midomo yao, wakiagiza Chips hawali mpaka iwekewe Mayonaizi, wanapenda Kuvaa Suruali Modo na zinazowabana na hupenda kuwa karibu na Mabinti ila kwa nilichokiona leo Mchana nimepata Jibu.

Ngoja Junior wangu akue kue Kidogo ili nami Baba yake GENTAMYCINE nianze Kumlea Kijeshi / Kimedani kama ambavyo Baba yake nililelewa na Babu yake ili huko mbeleni asije kuwa Msukuma Ukuta kama walivyo Vijana wengi waliozaliwa kuanzia Mwaka 1990 na nianavyo huko mbeleni hali itakuwa mbaya mno na si ajabu hata Tanzania tukaja Kuongozwa na Msukuma Ukuta kwani dalili ya Mvua ni Mawingu.

Serikali kwa Kushirikiana na Jeshi ( JWTZ ) tafadhali GENTAMYCINE nawaombeni Tangazeni Mafunzo ya Kijeshi ya JKT ni lazima ili tukiokoe Kizazi cha Vijana wengi wa Kiume wa sasa ambao wanaonekana Kupenda na hata kutamani Kusukuma Ukuta na kufanana na Dada / Mama zao.
 
Inasikitisha sana kijana na nguvu zake eti anapanda daladala Mapipa anaenda kuteremka mwembe chai tena mida ya jioni hata jua hakuna
Ndiyo maana Siku hizi wengi Wao Wanasukuma sana Ukuta Mkuu na Wataisukuma mno tu wasipojirekebisha.
 
Utakuwaje na Taifa lenye Watu Shupavu ( tena kwa Vijana ) kama unakutana na Kijana wa Kiume kapanda DalaDala kutoka Makonde Mbezi Beach na anashukia Kituo kinachofuata cha Goigi huku akijiona ni Mjanja?

Nilikuwa najiuliza sana tu ni kwanini Vijana wengi wa Kiume Siku hizi ni Wavivu, hawapendi Shuruba ( Taabu ), wanapenda Kujiremba na kufanyiwa Scrub na Massage huko katika Masaluni, wakiongea wanabana Sauti, wanapenda Kujilambalamba Midomo yao, wakiagiza Chips hawali mpaka iwekewe Mayonaizi, wanapenda Kuvaa Suruali Modo na zinazowabana na hupenda kuwa karibu na Mabinti ila kwa nilichokiona leo Mchana nimepata Jibu.

Ngoja Junior wangu akue kue Kidogo ili nami Baba yake GENTAMYCINE nianze Kumlea Kijeshi / Kimedani kama ambavyo Baba yake nililelewa na Babu yake ili huko mbeleni asije kuwa Msukuma Ukuta kama walivyo Vijana wengi waliozaliwa kuanzia Mwaka 1990 na nianavyo huko mbeleni hali itakuwa mbaya mno na si ajabu hata Tanzania tukaja Kuongozwa na Msukuma Ukuta kwani dalili ya Mvua ni Mawingu.

Serikali kwa Kushirikiana na Jeshi ( JWTZ ) tafadhali GENTAMYCINE nawaombeni Tangazeni Mafunzo ya Kijeshi ya JKT ni lazima ili tukiokoe Kizazi cha Vijana wengi wa Kiume wa sasa ambao wanaonekana Kupenda na hata kutamani Kusukuma Ukuta na kufanana na Dada / Mama zao.
Ifike hatua waacheni vijana wapumzike mshawasakama vya kutosha. Kama wewe uliishi maisha ya kigumu sio lazima kila mmoja aishi ivyo, kuishi maisha ya tabu sio mashindano, mtu akipanda daladala bamaga akashukia itv wewe inakuhusu nini? Unamlipia nauli? labda kuna mchongo wa muhimu alikua anauwahi. Maisha yanabadilika kuanzia fashion ya nguo, urahisi wa kupata ajira, trend ya vyakula, uharaka wa kukamilisha kazi n.k haiwezekani kila kitu kikabaki vile vile kila generation. Hii nchi ina wazee wa ovyo sana na ndio waliotufikisha hapa kuanzia kiongozi wa nchi na wakuu wa almost taasisi zote ni wazee miaka 60 ya uhuru sasa hivi hata madawati mashuleni tu ni shida ila kutwa lawma kwa vijana tu.
 
Pole sana kwa kupatwa na jiwe gizani i
 
Nimeshangaa sana kushuhudia vijana wanakula chipsi mayai ya kuku mataahira na wanashiba kabisa, bila shaka kwa sasa hii dunia itakuwa haijavaa hata chupi
 
Ifike hatua waacheni vijana wapumzike mshawasakama vya kutosha. Kama wewe uliishi maisha ya kigumu sio lazima kila mmoja aishi ivyo, kuishi maisha ya tabu sio mashindano, mtu akipanda daladala bamaga akashukia itv wewe inakuhusu nini? Unamlipia nauli? labda kuna mchongo wa muhimu alikua anauwahi. Maisha yanabadilika kuanzia fashion ya nguo, urahisi wa kupata ajira, trend ya vyakula, uharaka wa kukamilisha kazi n.k haiwezekani kila kitu kikabaki vile vile kila generation. Hii nchi ina wazee wa ovyo sana na ndio waliotufikisha hapa kuanzia kiongozi wa nchi na wakuu wa almost taasisi zote ni wazee miaka 60 ya uhuru sasa hivi hata madawati mashuleni tu ni shida ila kutwa lawma kwa vijana tu.

Siku ukipata ajira utapunguza haya makasiriko.
 
Back
Top Bottom