Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,499
- 9,279
Mbunge wa viti maalum, Ester Bulaya ameishauri Serikali ya Tanzania kutoa mafunzo ya kutumia silaha kwa vijana wachache wanaoshiriki mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) badala ya kuwafundisha wengi.
Bulaya amesema kutoa mafunzo ya silaha kwa vijana wengi wakati hawapati nafasi za kujiunga na jeshi hilo, baadhi si waaminifu wanaweza kutumia mafunzo hayo kufanya uhalifu.
Bulaya ameeleza hayo leo Jumatano Machi 31, 2021 bungeni mjini Dodoma wakati akimuuliza swali la nyongeza Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Elias Kwandikwa.
Katika majibu yake Kwandikwa amesema jeshi hutoa mafunzo ya silaha kwa vijana katika idadi inayotakiwa na kwamba hakuna shida katika jambo hilo.
Amesema mafunzo ya JKT yanalenga kuwajengea vijana uwezo wa kujitegemea badala ya kuajiriwa, kwamba jeshi linafanya tathmini ya kuboresha zaidi mafunzo hayo.
Wakati huohuo, Serikali imetoa sababu za kuwarudisha nyumbani mapema vijana waliokuwa kwenye mafunzo ya JKT.
Kwandikwa ametaja sababu hizo ni kuangalia mtaala utakaosaidia kuboresha mafunzo na kuangalia muda wa mafunzo ya miezi mitatu ya waliomaliza kidato cha sita yafikie mwaka mmoja na kuwafanya vijana wapate ujuzi wa kujitegemea.
Chanzo: Mwananchi