Naomba kutofautiana na watanzania wengi ambao bado wanaamini JKT inawajengea vijana, uzalendo n.k
Jana nimeshuhudia ki video kikitembea mitandao kikionyesha vijana waki "craw" kwenye tope.
kwa kweli nilikuwa very much shocked na kujiuliza kijana wa leo akipelekwa katika kambi na kupewa mafunzo haya yanamjenga vipi kukabiliana na changamoto za leo.
kama taifa ni lazima tujue zama zipi tulizopo na je ni elimu gani tuwape vijana wetu kujenga taifa letu kama jina linavyosema.
nikirudi katika historia ninaweza kusema miaka ya zamani jamii zilikuwa na elimu za jando na unyago. Vijana walipelekwa katika makambi kufundishwa mbinu za kuwa kijana bora katika jamii ikijumuisha jinsi ya kutimiza shughuli za kifamilia na ulinzi katika jamii.
Zama hizo zilipita tukaingia katika zama za ukombozi na hapa vijana walihitaji kufundishwa ukakavu na uzalendo ambao enzi hizo ulikuwa na kupelekwa msituni kupambana kukomboa nchi zao kutoka mikononi mwa watu. Baada ya kupata uhuru, serikali zetu nyingi hazikuwa na nguvu za kuajiri majeshi ya kutosha kulinda nchi zao na enzi hizo jamii zetu zilikuwa zimekumbwa na migogoro ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na vita kati ya nchi moja na nyingine. Katika mazingira yale huo ndiyo ulikuwa uzalendo.
Lakini leo hii mazingira yamebadirika, jamii inakabiliwa na tatizo na kugawa rasilimali bila kufaidisha nchi zao, jamii zinakabiliwa na wingi wa wasomi kutoka katika mifumo ya elimu na kukosa ajira, tunakabiliwa na jamii ambazo masokoni kumejaa bidhaa za kigeni tena zinazoweza kutengenezwa kwa ujuzi kidogo tu.
bado tunakumbatia elimu ya miaka ya 60 na tukiamini tunajenga uzalendo.
Uzalendo wa miaka ya 60 ni mtu kwenda msituni kukomboa nchi yake lakini uzalendo wa mwaka 2000 ni mtu kuacha kuagiza nguo china na kufungua sehemu ya kushona nguo hizo hizo kwa ubora huohuo.
Uzalendo wa miaka ya 60 ilikuwa ni mtu kufundishwa kula chakula katika mazingira magumu maana hayo ndiyo vijana walitarajia katika kukomboa mataifa yao lakini uzalendo wa miaka ya 2000 ni kijana kuelimishwa kukataa kugawa rasilimali za taifa kwa vizawadi vidogo na jamii ielewe kuwa matajiri wanaotajirika kwa kugawa rasilimali zetu ni laana kwa taifa.
uzalendo wa miaka ya 60 ulikuwa wa kijeshi lakini uzalendo wa miaka ya 2000 ni wa uchumi zaidi maana tayari tuna uhuru wa bendera lakini bado tu watumwa kiuchumi.
Sioni ni kwa namna gani hizo program za JKT zinajenga taifa letu.
Wanasema zizi lisilokuwa na ndama halina "future" na nguzo ya taifa lolote ni vijana lakini iwapo vijana watajengwa katika kupeleka fikra zao kuendana na wakati ujao.
Je tumewahi kufanya utafiti hawa vijana wanaotoka jkt wanakuwa na impact gani katika jamii au tunatengeneza walinzi wa makampuni binafsi na ndivyo tunajenga nchi yetu?