Kwa Kauli hii ni rasmi kuwa Msemaji wa Yanga SC Hassan Bumbuli ana Akili Kubwa kuliko Wanayanga wote na mpaka Injinia Hersi wa GSM

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,559
108,898
"Hivi ni kwanini Waandishi wa Habari wa Michezo wa Tanzania mnapenda sana Kuzusha na Kutuchonganisha Yanga SC na Vilabu vyenye hao Wachezaji mnaotuhusisha nao kuwa tumeshawasajili? Ukweli ni kwamba mpaka hivi sasa naongea nawe hivi Yanga SC haijasajili Mchezaji yoyote yule kutoka nchi yoyote na nawaomba acheni Uzushi na Kutuchonganisha tafadhali "

Chanzo: Sports Extra Clouds FM Jana Usiku.

Haya GENTAMYCINE nikisema kuwa Injinia Hersi Said na GSM yake ameshazijua Akili za 'Oya Oya' wengi waliopo Yanga SC hivyo anacheza na Akili zao katika 'Kuwahadaa' huwa hawaniamini.

Injinia Hersi Said na GSM yake (yao) anajua ana Deni la Kuwajibu Yanga SC na Uwongo aliowapa kuwa Msimu huu Yanga SC itakuwa Bingwa na kwamba isipokuwa aulizwe Yeye.

Anachofanya sasa (Injinia Hersi Said na GSM yake) anajua kuna Mkutano Muhimu unakuja Jumapili ijayo hivyo amewahonga Wahariri na mpaka Waandishi wa Habari za Michezo ili wamuandike mno kuwa anasajili 'Majembe' Yanga SC ili wamuamini, wasahau Kumuhoji na GSM yake iaminike, ipewe Timu rasmi katika Mabadiliko ya Katiba Jumapili ijayo Mkutanoni ili aendelee Kupiga ( Kuchuma ) bila Jasho jingi ndani ya Yanga SC.

Haya mpingeni sasa Msemaji wenu HB.
 
Kiukweli Yanga wanahitaji wakae chini na kuitengeneza timu yao. Na ili wafanikiwe lazima waanza kwanza kuujenga uongozi wao.

Yaani waanze kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa katika idara za uongozi na baada ya hapo ndio warudi kupambana na kuijenga timu uwanjani
 
Kiukweli Yanga wanahitaji wakae chini na kuitengeneza timu yao. Na ili wafanikiwe lazima waanza kwanza kuujenga uongozi wao.

Yaani waanze kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa katika idara za uongozi na baada ya hapo ndio warudi kupambana na kuijenga timu uwanjani
Tafadhali Mkuu acha kuwapa hizi Akili na huu Ushauri kwani hawa wakija kuwa sawa kwa kila Kitu watatusumbua na hata Kukutesa mno Simba SC ndani na nje ya Uwanja.

Acha waendelee kuwa 'Wapuuzi' hivi hivi walivyo na kila Uchao ( Siku ) wawe ni Watu tu wa Kuvurugana, Kulalamika na hata Kugombana wao kwa wao.
 
Back
Top Bottom