Kwa jinsi morali ya wachezaji na mashabiki wa Simba ilivyokuwa wakati wa mechi dhidi ya Asec Mimosas ni dhahiri kwamba mambo hayako sawa.

Baba Oruch

Member
Nov 4, 2023
51
92
Heshima yenu wadau.

Ni ukweli usiofichika kwamba tangu kumalizika kwa mechi ya Simba dhidi ya Yanga morali ya mashabiki na wachezaji imeshuka sana na pengine ikaendelea kushuka zaidi kwani wapo waliokata tamaa wakiamini upngozi ndio chanzo cha haya yote.

Wapo wanaoamini Kuna mzaha unafanywa na viongozi katika usajili, wapo wanaoamini kuna hali ya kusalitiana miongoni mwa viongozi, benchi la ufundi na wachezaji lakini pia wapo wanaoshangaa aina ya maamuzi yaliyofanywa wakati wa kuamua mchezaji gani abaki na nani aondoke kabla ya msimu mpya kuanza.

Timu inahitaji top class players na hata mwaka juzi kuna kiongozi aliwahi kusema anaahirisha kununua Rolls Royce ili asajili top straker kwa lengo la kuifanya klabu ifanye vizuri katika mashindano ya ndani na yale ya kimataifa. Tangu wakati huo timu haijawahi kuwa na aina ya mshambuliaji aliyekuwa akidhaniwa na imebaki bila muunganiko jambo ambalo linazidi kushusha zaidi morali. Kuna jambo kubwa sana linatakiwa kufanywa na viongozi hasa kwenye suala la usajili vinginevyo huko mbeleni timu inaweza kukosa mashabiki uwanjani kama tulivyoshuhudia katika mechi dhidi ya Asec Mimosas​
 
Back
Top Bottom