mshana jr Ooh hivi kumbe kwenye jukwaa tunazuiwa matumizi ya neno "NATUMIA NGUVU kubwa" samahani mkuu ikiwa limekukela ingawa nasikitika kwamba uzuiaji huu unanirudisha kwenye kuamini unalazimisha hoja ya laana kwa Dr.
Upotoshaji hautaisha na waliopotoshwa wakashindwa kujikwamua watabaki kuwa waliopotoka. Tatizo unacheza na akili yako mwenyewe unaamini padri hawezi kutoka katika upadri na akawa salama, wakati unashindwa kuelewa hata Pope alijiuzuru. Sijui yeye atakuwaje maana daraja lake huwa ni mpaka moshi mweupe toka kwa Mungu utoke ndio anasimikwa. Ukiwa mweusi maana yake Mungu hakupenda matokeo ya cardinals.
hoja yangu toka awali nilitamani sana uje na fact za laana ya Dr. lakini unarukaruka tu. CDM plus EL hakuna yeyote aliye jibu tuhuma za Dr. Maana tuhuma lazima zijibiwe ili kuupata ukweli. Iwe Dr aliongea na kada yeyote wa CCM bado haitoshi kwamba alichokisema ni tofauti alichohubiri sikuzote kabla ya kujitoa CDM.
Zaidi aliongeza mshangao wake kwa alie muita mshenga jinsi alivyo kuwa akijisifu kwa rushwa aliyotapanya....nimesikiliza majibu yao bado sijashawishika kuwa wamekuwa wakweli.
Kutumia dini kumshambulia Dr kisiasa kwenye jukwaa la siasa ni kosa. Angalia imani yako, na uombe modes wauhamishe uzi huu, uende kule kwenye dini.