lugendosisty
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 219
- 103
Kama atakuwa na ujasiri huo atatubu na kujirudi lakini sio leo wala kesho ni mpaka pale atakapogundua kuwa alitumika kwa malengo yaliyo wazi
Kaka Mshana Jr,sina budi nikupongeze kwa hili bandiko hapo juu. Maana hiki kitu niliwahi elezwa na mzee wangu kwamba Dr. w Slaa kamwe hatofika mbali au kupata mamlaka ya juu ya nchi kisiasa au katika utawala kwani tayari amekiuka kiapo. Niwazi hichi kinachotokea si kwa mamlaka yake yy bali ni nguvu ya rohoni inamtesa. Tutegemee makubwa kumfika na kudhihirisha nadhiri aliyofunga na Mungu wake haikupaswa kutenguliwa na Mwanadamu kwa matamanio yasioweka hazina Mbinguni.
Ni wakati wa wanasiasa wa Chama cha Mapinduzi na Chama cha demokrasia na Maendeleo kulianagalia hilo suala kwa umakini mkubwa.Ili basi pale wanapoamua kujibu hoja zake au kumtumia kisiasa waangalie na madhara yake kwa mama Tanzania. Hatuhitaji alete mpasuko kwa Taifa letu kama alivyonena tarehe mosi juu ya maaskofu na kanisa la kilutheri