Kwa hili, Rostam Aziz hutasameheka

Wabunge wengi walioleta maendeleo ya kweli kwenye majimbo yao kama vile barabara, shule, zahanati, kilimo na ufugaji endelevu ni wale waliobahatika kuwa mawaziri wa wizara husika na wakaondoa woga, wakaelekeza miradi mingi majimboni kwao. Mifano ni mingi lakini mawaziri waliotoka Kilimanjaro ni mfano wa kuigwa tangu enzi za Mwalimu akina Eliuffoo, Mtei, Mramba, CD Msuya,......
Tusisahau pia kwamba watu wenyewe wawe tayari kuyapokea, kuyaenzi na kuyafanyia kazi maendeleo haya.
 
Binafsi napenda nilingalie hili kwa jicho la tofauti,...tatizo sio rostam,...tatizo ni sera za chama chake.
Hakuna jimbo katika tanzania hii utaenda ukose kuyaona uliyo yaona Igunga,..haijalishi jimbo
hilo linaongozwa na mbunge tajiri wa ccm au mbunge maskini wa chama cha upinzani,...kote hali ni sawa kabisa.

Nimeona picha hapo juu ya watoto wakiwa darasani wamekaa chini wanajifunza kuandika....
Well,hainishtui hata kidogo,...trust me.

Nimesoma shule za serikali,kwanzia vidudu hadi chuo kikuu.
Nasoma UDSM,lakini hakuna tofauti ha hayo unayo yaona kwa watoto kukaa chini.
Labda tofauti tu ni kwamba udsm wanaosoma ni watu wazima kwahiyo hata wakikaa chini watakaa katika
hali ya ku-maintain usafi na unadhifu wao.
Lakini ukweli ni kwamba hata chuo kikuu na kikongwe kabisa Tanzania wasomi wake wanakaa chini wakiwa
wana sikiliza lecture.
(Nikipata nafasi nitatoa picha hapa siku moja)

Sasa kama chuo kikuu katika Tanzania kiko hivo unategemea nini kwa watoto wa shule ya msingi
walio vijijini kabisa?
Ni kawaida kabisa.

Mjini hapa watu wengi wamepanga,wapo wenye hela lakini hazitoshi kujenga,...
tatizo ni sera mbovu za ccm zinazo sababisha bei za bidhaa ya ujenzi kuwa juu.

Tofauti kati ya hawa wa mjini walio panga (nikiwemo mimi) na wale wa vijijini wanao onekana
kanika nyumba za tembe ni kwamba wao wameweza kujenga zao kutokana na kipato chao
hata kama tunaziita mbovu na sisi tumeshindwa kujenga ingawa tunawazidi kipato.

Chimbuko la haya yote ni sera mbovu za CCM,...lakini swali ni je,....
Kuna chama chenye sera nzuri za kuleta maisha mazuri kwa watanzania kweli?
Sidhani
 
Huyo ndiye bilionea Rostam Aziz. Amepiga madili lukuki na kukusanya mabilioni na akayapeleka zake nje huku akiwatumia wana Igunga na kuwatema kama kapi za muwa.
 
nchi yetu tunamatatizo sana, raia wamepoteza uzalendo ukiangalia viongozi wetu ndo balaaa!
matumaini yote yamepotea kwani sasa ni ubinafsi kwenda mbele..hakuna kujali tena watanzania wenzako
raia wa kigeni wamejazana nchini kwetu bila sababu za msingi,matokeo yake imekuwa ni kero ya kunyanyasika
kwani kazi hakuna na matarajio ya kupata ajira ni finyu.
CCM wameshachoka..tafadhali tuwaondoeni.
 
Dada yote unayosema hapa ni kweli kabisa lakini mbona hamkuyasema wakati mkiwa Igunga?
Mkuu ulifuatilia kampeni au umejua kuwa kuna uchaguzi mdogo Igunga baada ya matokeo kutangazwa?
 
Nasema mara nyingi humu tunaigharamia sana SIASA bila sababu. Kama mabilioni yaliyotajwa kwenye TD ya leo ni kweli mnashangaa nini Igunga kuwa katika hali hii? Eti dada Regia, CHADEMA peke yenu mmetumia milioni mianne (400,000,000/=) kutafuta ubunge wa Igunga pekee?
 
Nimeamua kuandika habari hii baada ya kujishauri tangu nikiwa Igunga!

Rostam Aziz amekuwa Mbunge wa Igunga tangu mwaka 1994 ambapo mpaka sasa ni takribani miaka 17 chini ya uongozi wake. Nilikuwa sijawahi kufika Igunga kabla hivyo sikuifahamu ilivyo.Siku Rostam anajiuzulu alieleza mafanikio mengi aliyoyafanya Igunga nikadhani Igunga hali ni shwari na watu wanamaendeleo mazuri,nilivyofika sikuamini nilichokiona. Rostam alitudanganya. Katika tembea yangu yote hapa nchini sijawahi kuona Wananchi wanashida kama wa Igunga.

Mambo yafuatayo nimeyagundua katika jimbo la Igunga;

1. Wananchi wengi wa Jimbo la Igunga hawajui kusoma na kuandika mpaka vijana wadogo

2. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 13 kufuata maji kwenye Makomero tena maji yenyewe sio safi wala salama

3. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 10 kufuata shule,wengine wanaenda hadi 20

4. Kwenye kata nilizopita hawaelewi wala kuzijua shule za awali.

5. Wananchi wengi wanatembea umbalimrefu kufuata Zahanati na hayo majengo yenyewe ya Zahanati unaweza kulia.

6. Hakuna barabara za kuunganisha kijiji kimoja na kingine,njia zilizopo ni mapitio ya ng'ombe.

7. Wananchi wengi hawana vyoo wala hawana mpango wa Kujenga vyoo,wao wajenga mabafu tu yanayotumika kuogea na kujisadia haja ndogo,haja kubwa utajua mwenyewe.

8. Zipo Kata ambazo hazing mawasiliano ya simu

9. Lipo Kabila mpaka leo wanatembea uchi kama kwa King Muswati.

10. Wapo wanaotembea karibu Kilomita 13 kufuata TV waone taarifa ya habari na mambo mengine. Hii ni Kata anayotoka Dr. Kafumu

11. Na mengine mengi madogo madogo.

Rostam alikuwa na uwezo wa kupunguza hayo niliyoyataja kwasababu zifuatazo

1. Alikuwa ni Mbunge hivyo alikuwa na fursa ya kupiga kelele ndani na nje ya Bunge na akasililizwa.
2. Alikuwa Mbunge mwenye ushawishi ndani ya chama chake hivyo angeweza kushawishi Mawaziri ili miradi iende Jimboni kwake.
3. Alikuwa Mbunge tajiri sana,kama aliweza kuipa CCM,Mabilioni ya shillingi,Kama aliweza kuhonga watu mbalimbali mamilioni ya shilingi alishindwaje kusaidia Jimboni kwake? aliishia kuwanunulia tu simu Mabalozi wa Nyumba Kumi ili wamfanyie Kampeni.
4. Alikuwa anafahamiana na wafadhili wengi tu wa Maendeleo wa ndani na nje ya nchi alishindwaje kuwashawishi wawekeze kwake?

Rostam aliyaweza haya yote lakini hakujali kwakuwa hakuwa na lengo la kuwatumikia Wananchi wa Igunga. Kwasababu hizo basi nashawishika kusema kuwa Rostam ni zaidi ya DUBWANA ni mtu anayeongoza kwa roho mbaya hapa nchini. Hana huruma hata kidogo, anajali maslahi yake tu.. Bora ulivyojiuzulu, ungejiuzulu na utanzania kabisa, ukaombe uraia wa nchi nyingine huko ughaibuni sio Afrika!

Nawasilisha!
Haha hao wananchi sio ndio walikuwa wanasema Igunga bila Rostamu hakuna maendeleo na wengine ndio walikuwa wanalia na kuzimika kumbe ilikuwa ni ze komedy au ndio wajinga ndio waliwao
 
Sasa Mbunge mwenyewe alikuwa bubu bungeni, atashawishi vipi? Naishukur sana CDM kwa kuanza kuwaonyesha wana-Igunga ukweli!
 
Mimi nawaombea hawa watu wapate pigo zaidi. Wana macho, hawaoni. Wana masikio, hawasikii. Wanamiguu lakini hawaendi.
Wale wote waliokuwa wanashinda kwenye mtandao sasa wanawacheka wanaigunga na kuwatimulia vumbi.
Nikiona watanzania wanavoumizwa kwa ujinga wao machozi hulenga lenga.[/QUOTE
Sio wote mkuu wapo watu wenye dhati ya kuikataa ccm lakini si umeona mizengwe ya uchaguzi ? kuna mtu alianzisha thread kuonyesha cdm ilivyokuwa na maadui wengi igunga mfano ccm, cuf, polisi, mkurugenzi, na wengine wengi ndio maana tunawajibika kuwapongeza wale wote waliochagua cdm mbali na vitisho ,ubaguzi wa kidini nk badala ya kuwalaumu mie nawaona kama mashujaa wataendelea kupata tabu lakini ni bora hawakuichagua ccm.
 
wajemeni shida hizo ziko kila mahali hata kule karatu. Rostam alikuwa mbunge tu, kazi ya kuondoa kero hizo ni ya serikali.... aghh!

Pamoja na serikali ndo inatakiwa kufanya hivyo mmwakilishi wao ambae ni mbunge anatakiwa kupiania kuhakikisha serikali gaitajishau kwa muda mreru kuelekezea maendeleo jimboni kwake, pindi serikali inaposhindwa mbunge anaweza kufanya alternative nyingine kama kutafuta wawekezaji toka ndani na nje ya nchi na hata kuomba misaada mbalimbali kwami babu ndesamburo moshi aliweza je?
 
Ndumba naomba nijue kitu kimoja tu,umewahi fika igunga?na karatu?kama bado tembelea hizi wilaya halafu urudi hapa utueleze ulichokiona personally i have been to both districts

Tuambie wewe ulivyoenda uliona nini?
 
Regia

hakuna haja ya kuwasikitikia wananchi wa Igunga kama hawajui kwamba wanakosa basics.... wamechagua wanachodhani kinawaletea maendeleo... tena maendeleo mazuri ya kuona magari kipindi cha kampeni, pombe zimeuzwa sana, vumbi limetimka, wamepata wali na nyama

SIWAONEI HURUMA WANAIGUNGA NA SIMLAUMU ROSTAM KWANI AMEWATUMIA KAMA WALIVYOSTAHILI.... MTAJI WA SIASA

Kwenye siasa za uchwara, unatakiwa kuwafunga watu macho, kuwafanya wapumbavu na wajinga na wao watakuabudu.... AND THAT IS WHAT ROSTAM DID!!! (AND MANY CONSTITUENCIES CCM WALIPO STRONG)

Chunguza utajua kwanini umaskini ni lazima kwa chama chochote tawala kubaki madarkani
 
Dada Regia Mtema
Kwanza hongera kwa kuwa mstari wa mbele kwenye mapambano dhidi ya wadhalimu na waporaji wa rasilimali za nchi yetu.Najua Chadema mlijitahidi kuwaeleza wana igunga haya mapungufu na kwa nini wasichague CCM tena.Napenda kuipongeza chadema kwa mtaji mkubwa wa kisiasa walioupata Igunga.Maswali ninayoyataka kupata majibu kutoka kwako ni haya yafuatayo.....
  1. Kipi kiliwafanya wana Igunga kuichagua tena CCM pamoja na umasikini wote huu wa kutawaliwa na CCM kwa miaka 50?
  2. Je wewe unaamini kwamba CCM walishinda kihalali?{ jamabo ambalo mimi amabaye sikuwepo igunga siamini}
  3. kama walishinda kihalali Nini kilikuwa mtaji wa CCM kwa wananchi wakati wakijinandi?
  4. Je ni kweli kuna mahali Chadema hawakufanikisha vya kutosha kulikopelekea kutopata Ushindi zaidi ya tulioupata?
  5. kuna dhana kwamba Chadema walijuwa kuwa hawatashinda Igunga piga ua na kwamba CCM hata kama ingebidi kupoteza uhai wa watu wasingekuwa radhi kuliachia jimbo la Igunga . je hii ni kweli na kama ni kweli kulikuwa hakuna njia nyingine ya kukabiliana nayo zaidi ya kushindana na mtu unayejua fika hata kubali matokeo?
  6. Nini chadema imejifunza Igunga ambacho mlikuwa hamkijui kabla?
  7. Nini Ushauri wako kwa siku za usoni , hasa kwetu tunaotaka kujitosa kwenye mapambano.
nakutakia kila la heri kwenye kazi zako. mungu akubariki nawakilisha
 
Nimeamua kuandika habari hii baada ya kujishauri tangu nikiwa Igunga!

Rostam Aziz amekuwa Mbunge wa Igunga tangu mwaka 1994 ambapo mpaka sasa ni takribani miaka 17 chini ya uongozi wake. Nilikuwa sijawahi kufika Igunga kabla hivyo sikuifahamu ilivyo.Siku Rostam anajiuzulu alieleza mafanikio mengi aliyoyafanya Igunga nikadhani Igunga hali ni shwari na watu wanamaendeleo mazuri,nilivyofika sikuamini nilichokiona. Rostam alitudanganya. Katika tembea yangu yote hapa nchini sijawahi kuona Wananchi wanashida kama wa Igunga.

Mambo yafuatayo nimeyagundua katika jimbo la Igunga;

1. Wananchi wengi wa Jimbo la Igunga hawajui kusoma na kuandika mpaka vijana wadogo

2. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 13 kufuata maji kwenye Makomero tena maji yenyewe sio safi wala salama

3. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 10 kufuata shule,wengine wanaenda hadi 20

4. Kwenye kata nilizopita hawaelewi wala kuzijua shule za awali.

5. Wananchi wengi wanatembea umbalimrefu kufuata Zahanati na hayo majengo yenyewe ya Zahanati unaweza kulia.

6. Hakuna barabara za kuunganisha kijiji kimoja na kingine,njia zilizopo ni mapitio ya ng'ombe.

7. Wananchi wengi hawana vyoo wala hawana mpango wa Kujenga vyoo,wao wajenga mabafu tu yanayotumika kuogea na kujisadia haja ndogo,haja kubwa utajua mwenyewe.

8. Zipo Kata ambazo hazing mawasiliano ya simu

9. Lipo Kabila mpaka leo wanatembea uchi kama kwa King Muswati.

10. Wapo wanaotembea karibu Kilomita 13 kufuata TV waone taarifa ya habari na mambo mengine. Hii ni Kata anayotoka Dr. Kafumu

11. Na mengine mengi madogo madogo.

Rostam alikuwa na uwezo wa kupunguza hayo niliyoyataja kwasababu zifuatazo

1. Alikuwa ni Mbunge hivyo alikuwa na fursa ya kupiga kelele ndani na nje ya Bunge na akasililizwa.
2. Alikuwa Mbunge mwenye ushawishi ndani ya chama chake hivyo angeweza kushawishi Mawaziri ili miradi iende Jimboni kwake.
3. Alikuwa Mbunge tajiri sana,kama aliweza kuipa CCM,Mabilioni ya shillingi,Kama aliweza kuhonga watu mbalimbali mamilioni ya shilingi alishindwaje kusaidia Jimboni kwake? aliishia kuwanunulia tu simu Mabalozi wa Nyumba Kumi ili wamfanyie Kampeni.
4. Alikuwa anafahamiana na wafadhili wengi tu wa Maendeleo wa ndani na nje ya nchi alishindwaje kuwashawishi wawekeze kwake?

Rostam aliyaweza haya yote lakini hakujali kwakuwa hakuwa na lengo la kuwatumikia Wananchi wa Igunga. Kwasababu hizo basi nashawishika kusema kuwa Rostam ni zaidi ya DUBWANA ni mtu anayeongoza kwa roho mbaya hapa nchini. Hana huruma hata kidogo, anajali maslahi yake tu.. Bora ulivyojiuzulu, ungejiuzulu na utanzania kabisa, ukaombe uraia wa nchi nyingine huko ughaibuni sio Afrika!

Nawasilisha!
Mbona wabunge wa aina hiyo wako wengi, ebu jiulize jimbo la Mheshimiwa Six liko vipi????? Sasa kwa sababu hawana uwezo wa kufanya mambomengi kwa pamoja huo ni mtajia tosha wa CDM!!!!!!!!!! Watu wafahamiswhwe kuwa wapo hapo kwa kujaza mtumbo yao tuu!!!!!!!! Tukazanie katiba mpya na watu wataelewa ukweli bila wizi kwa katiba mpya watangoka tuu!!!!!!!!!
 
Nimeamua kuandika habari hii baada ya kujishauri tangu nikiwa Igunga!

Rostam Aziz amekuwa Mbunge wa Igunga tangu mwaka 1994 ambapo mpaka sasa ni takribani miaka 17 chini ya uongozi wake. Nilikuwa sijawahi kufika Igunga kabla hivyo sikuifahamu ilivyo.Siku Rostam anajiuzulu alieleza mafanikio mengi aliyoyafanya Igunga nikadhani Igunga hali ni shwari na watu wanamaendeleo mazuri,nilivyofika sikuamini nilichokiona. Rostam alitudanganya. Katika tembea yangu yote hapa nchini sijawahi kuona Wananchi wanashida kama wa Igunga.

Mambo yafuatayo nimeyagundua katika jimbo la Igunga;

1. Wananchi wengi wa Jimbo la Igunga hawajui kusoma na kuandika mpaka vijana wadogo

2. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 13 kufuata maji kwenye Makomero tena maji yenyewe sio safi wala salama

3. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 10 kufuata shule,wengine wanaenda hadi 20

4. Kwenye kata nilizopita hawaelewi wala kuzijua shule za awali.

5. Wananchi wengi wanatembea umbalimrefu kufuata Zahanati na hayo majengo yenyewe ya Zahanati unaweza kulia.

6. Hakuna barabara za kuunganisha kijiji kimoja na kingine,njia zilizopo ni mapitio ya ng'ombe.

7. Wananchi wengi hawana vyoo wala hawana mpango wa Kujenga vyoo,wao wajenga mabafu tu yanayotumika kuogea na kujisadia haja ndogo,haja kubwa utajua mwenyewe.

8. Zipo Kata ambazo hazing mawasiliano ya simu

9. Lipo Kabila mpaka leo wanatembea uchi kama kwa King Muswati.

10. Wapo wanaotembea karibu Kilomita 13 kufuata TV waone taarifa ya habari na mambo mengine. Hii ni Kata anayotoka Dr. Kafumu

11. Na mengine mengi madogo madogo.

Rostam alikuwa na uwezo wa kupunguza hayo niliyoyataja kwasababu zifuatazo

1. Alikuwa ni Mbunge hivyo alikuwa na fursa ya kupiga kelele ndani na nje ya Bunge na akasililizwa.
2. Alikuwa Mbunge mwenye ushawishi ndani ya chama chake hivyo angeweza kushawishi Mawaziri ili miradi iende Jimboni kwake.
3. Alikuwa Mbunge tajiri sana,kama aliweza kuipa CCM,Mabilioni ya shillingi,Kama aliweza kuhonga watu mbalimbali mamilioni ya shilingi alishindwaje kusaidia Jimboni kwake? aliishia kuwanunulia tu simu Mabalozi wa Nyumba Kumi ili wamfanyie Kampeni.
4. Alikuwa anafahamiana na wafadhili wengi tu wa Maendeleo wa ndani na nje ya nchi alishindwaje kuwashawishi wawekeze kwake?

Rostam aliyaweza haya yote lakini hakujali kwakuwa hakuwa na lengo la kuwatumikia Wananchi wa Igunga. Kwasababu hizo basi nashawishika kusema kuwa Rostam ni zaidi ya DUBWANA ni mtu anayeongoza kwa roho mbaya hapa nchini. Hana huruma hata kidogo, anajali maslahi yake tu.. Bora ulivyojiuzulu, ungejiuzulu na utanzania kabisa, ukaombe uraia wa nchi nyingine huko ughaibuni sio Afrika!

Nawasilisha!

Mh. Regia Shida kubwa ya nchi yetu kuendelea kukosa maendeleo, ni ulimbukeni wa wananchi wa vijijini. Hao ndio walio na ushawishi mkubwa wa kubadili matokeo ya chaguzi zote hapa nchini. Nakumbuka nimewahi kwenda kijiji kimoja huko kwetu, nilipowaambiwa watu wabadilike, waliniambia mwenyekiti wao wa CCM amewaambia vyama vya upinzani vinaleta vita. Kwa hiyo wachague chama cha Nyerere. Bila wao kujua hizo ni propaganda za kuendelea kuwa watumwa ndani ya nchi yao. Hakuna kitu kibaya kama kutawaliwa kifikra, na ndiyo Tanzania yetu.

Pendekezo
Chadema ifanye kila inachoweza kuanza kufanya kampeni za vijijini. Najua vijiji ni vingi mno lakini hakuna ujanja wa kuwakomboa watanzania bila ya kufika vijijini ambako ndio mtajiwa CCM. Ni gaharama kubwa lakini pia kizuri lazima kighalamiwe kwa faida ya wananchi. Natamani sana fedha za kununulia mashangingi ya viongozi yangetumika katka kuwaletea maendeleo wananchi. Wezentu waliondelea huwezi kukuta gari la serikali la mamilioni ya pesa za mlipa kodi. Lakini kwetu ni fasheni.

Nawakilisha.
 
Mbona wabunge wengi wa CCm ndio zao kama vp nyie wapinzani tuonesheni utofauti kati yenu nyie nao wao la sivyo nyie nao tutashindwa kuwaamini halafu tutaingia msituni
 
Back
Top Bottom