Kwa hili; kweli mbowe ana upeo mdogo sana!

Kila sheria inapotungwa haisomwi kama unavyosoma gazeti,unasoma kwa kuongozwa na nia ya mtungaji,madhara yawezayo kuletwa na sheria husika na masilahi ya watu.Angalia ibara ya 8 ya katiba iko wazi kuhusu nguvu ya umma.Hicho ndo Mwenyekiti wako(usibishi) alichomaanisha.

Kuna nguvu ya umma inayo shinda sheria?

Mbona kila siku mnakimbia mnapowaona polisi wamechachamaa?

Wekeni basi hiyo nguvu ya umma kwa polisi.
 
Kwahiyo kwa kuwa kuna effect ya kurudia hizo chaguzi ndio maana chadema mnaamua kuvunja sheria makusudi kisa tu mnadhani kuna gharama katika chaguzi hivyo serikali haitachukua hatua?

Usijidanganye mkuu.

Ni sheria ipi iliyovunjwa? Ina maana kuweka ulinzi binafsi ni kuvunja sheria? Kama ni hivyo bas makampuni binafsi ya uinzi yafungwe ikiwemo green guard
 
Siku hiz jf imejaa wahuni tu wasiojua sheria,siasa imevamiwa na genge la vibaka wa amani,hamy d alichosema nikwel kabisa
 
WanaJF!

Mwenyekiti wa CHADEMA taifa na mbunge wa jimbo la Hai, bwana Mbowe, amethibitisha kuwa yeye ana upeo mdogo sana kuhusu mambo ya sheria.

Bwana Mbowe amethibitisha hilo baada ya kueleza kuwa CHADEMA kufutwa haiwezekani kabisa na hiyo sababu aliyoitumia ndio kichekesho na imemdhalilisha kweli.

Sababu aliyoitoa bwana Mbowe ya kukingia chama chake kifua kuwa hakitaweza kufutwa na msajili si nyingine bali ni idadi ya wabunge, madiwani na wenyeviti wa vijiji.

Bwana Mbowe alieleza kuwa, "kufuta CHADEMA ni sawa na kufuta wabunge 49, madiwani zaidi ya 600 na wenyeviti wa vijiji zaidi ya 1000".

Kama bwana Mbowe angekuwa na maarifa kidogo sana ya sheria (kwa kupitia tu ile sheria ya vyama vya siasa) asinge weza kuongea hayo maneno ya ovyo kabisa kuhusu kufutwa kwa CHADEMA.

Ieleweke kuwa, chama cha siasa hakifutwi kwa kuangalia idadi ya wabunge, madiwani na hata wenyeviti wa vijiji waliotokana na chama hicho, bali kinacho angaliwa ni kama vigezo ama masharti yaliyo kwenye sheria yamevunjwa.

Anorexia nevosa!
 
HAMY-D na wewe kwa uzuzu......mbona klie chama chenye ...Meremeta,AnBen,EPA,Kagoda,Richmond hakijafutwa na bado kinapumua japo kwa mashine?....wishful thinking kutaka chama dume CHAEDAMA kifutwe!..Wishful thinking indeed!
 
Ni sheria ipi iliyovunjwa? Ina maana kuweka ulinzi binafsi ni kuvunja sheria? Kama ni hivyo bas makampuni binafsi ya uinzi yafungwe ikiwemo green guard

Kilicho kwenye sheria ni kwamba vyama vimeruhusiwa kuwa na ulinzi, ulinzi ni jambo ambalo lipo wazi kabisa, ila kilicho pigwa marufuku ni hicho wanachotaka kukiimarisha CHADEMA, ni kwanini CHADEMA maimarishe vijana waliopo sasa? mafunzo gani hayo ya nguvu ambayo vijana wa CHADEMA watafundishwa mpaka wawe imara kama jeshi la polisi?

Hapo ndipo sheria na katiba vyote viwili kwa pamoja vinapo vunjwa.
 
WanaJF!

Mwenyekiti wa CHADEMA taifa na mbunge wa jimbo la Hai, bwana Mbowe, amethibitisha kuwa yeye ana upeo mdogo sana kuhusu mambo ya sheria.

Bwana Mbowe amethibitisha hilo baada ya kueleza kuwa CHADEMA kufutwa haiwezekani kabisa na hiyo sababu aliyoitumia ndio kichekesho na imemdhalilisha kweli.

Sababu aliyoitoa bwana Mbowe ya kukingia chama chake kifua kuwa hakitaweza kufutwa na msajili si nyingine bali ni idadi ya wabunge, madiwani na wenyeviti wa vijiji.

Bwana Mbowe alieleza kuwa, "kufuta CHADEMA ni sawa na kufuta wabunge 49, madiwani zaidi ya 600 na wenyeviti wa vijiji zaidi ya 1000".

Kama bwana Mbowe angekuwa na maarifa kidogo sana ya sheria (kwa kupitia tu ile sheria ya vyama vya siasa) asinge weza kuongea hayo maneno ya ovyo kabisa kuhusu kufutwa kwa CHADEMA.

Ieleweke kuwa, chama cha siasa hakifutwi kwa kuangalia idadi ya wabunge, madiwani na hata wenyeviti wa vijiji waliotokana na chama hicho, bali kinacho angaliwa ni kama vigezo ama masharti yaliyo kwenye sheria yamevunjwa.

Mzee HAMY - D hivi kweli huna shughuli nyingine ya kukuingizia KIPATO 24/7 wewe na CHADEMA tu uko so BIAS any way kuna kipindi nilikushauri uombe page kwa MICK pale UHURu gazeti la CCM uweze kuwa mwandika riwaya badae wanaweza kukupa uandishi wandamizi kabla ya 2015 Evaluate ur self
 
Kilicho kwenye sheria ni kwamba vyama vimeruhusiwa kuwa na ulinzi, ulinzi ni jambo ambalo lipo wazi kabisa, ila kilicho pigwa marufuku ni hicho wanachotaka kukiimarisha CHADEMA, ni kwanini CHADEMA maimarishe vijana waliopo sasa? mafunzo gani hayo ya nguvu ambayo vijana wa CHADEMA watafundishwa mpaka wawe imara kama jeshi la polisi?

Hapo ndipo sheria na katiba vyote viwili kwa pamoja vinapo vunjwa.

Subirini mafunzo yatolewe, ikionekana mafunzo hayo ni zaidi ya mafunzo ya polisi ndo mlalamike. Pili polisi wamesaau kabisa wajibu wao wa kulinda raia na mali zake badala yake wanawalinda majambazi wa ccm na kuwadhuru wananchi wasiokuwa na hatia, na kibaya zaidi polisi hao hao wamekuwa ndo vinara wakubwa kwa matukio ya kuvunja sheria, bora cdm iendelee na mkakati wake na imani yangu ni kwamba huyo tendwa kazeeka ndo maana anatoa kauli zisizokuwa na maana.
 
Unajua kijana you are too far from the truth!
Lissu alitoa sababu za kisheria za kwa nini CHADEMA haiwezi kufutwa katika vyombo vya habari!
Dr.Slaa akatoa sababu za kifalsafa na kisiasa kwa nini CHADEMA haiwezi kufutwa.
Marando akatoa sababu za jeuri kwa nini CHADEMA haiwezi kufutwa!
Mwisho Mwenyekiti Mbowe akatoa sababu as a visionary leader kwa nini CHADEMA haiwezi kufutwa...
KILA KIONGOZI ALITOA HOJA KULINGANA NA MUKTADHA NA HII NDIYO TEAM WORK....WHEN YOU COMBINE THEM ALL YOU GET THE LOGIC...OTHERWISE HAVE IT YOUR OWN WAY!
 
Ieleweke kuwa, chama cha siasa hakifutwi kwa kuangalia idadi ya wabunge, madiwani na hata wenyeviti wa vijiji waliotokana na chama hicho, bali kinacho angaliwa ni kama vigezo ama masharti yaliyo kwenye sheria yamevunjwa.

Kama kweli hii ingekuwa ni akili yako mwenyewe ungetambua kuwa Chadema haiwezi kufutwa na katibu mwenezi wenu wa pili John Tendwa.

Kama ungekuwa unatumia akili yako mwenyewe unge recall kauli ya mwenezi wenu wa pili John Tendwa kuwa hawezi kuifuta ccm, sio kwa sababu sheria haimruhusu bali kwakuwa yeye ni kada wa ccm na hawezi kuipindua serikali ya chama chake.

Lakini kwakuwa unatumika na wazee wa lumumba, buku saba fc project basi unaweweseka na Chadema na viongozi wake ili angalau upate shilingi mbili za kununulia uji wa futur!
 
Subirini mafunzo yatolewe, ikionekana mafunzo hayo ni zaidi ya mafunzo ya polisi ndo mlalamike. Pili polisi wamesaau kabisa wajibu wao wa kulinda raia na mali zake badala yake wanawalinda majambazi wa ccm na kuwadhuru wananchi wasiokuwa na hatia, na kibaya zaidi polisi hao hao wamekuwa ndo vinara wakubwa kwa matukio ya kuvunja sheria, bora cdm iendelee na mkakati wake na imani yangu ni kwamba huyo tendwa kazeeka ndo maana anatoa kauli zisizokuwa na maana.

Tutor B,

Ningependa urudi tena kwenye huu uzi ili ujibu swali langu!

Hivi, kati ya Tendwa na Dr Slaa ni nani ana umri mkubwa?
 
Last edited by a moderator:
Ningekuwa Nchemba Mwigulu ningekuongezea buku nyingine7 ju ya zile 7 za kawaida.Topic yako ni mahiri na ina uchambuzi wa kina kwa wavivu wa kufikiri
 
Subirini mafunzo yatolewe, ikionekana mafunzo hayo ni zaidi ya mafunzo ya polisi ndo mlalamike. Pili polisi wamesaau kabisa wajibu wao wa kulinda raia na mali zake badala yake wanawalinda majambazi wa ccm na kuwadhuru wananchi wasiokuwa na hatia, na kibaya zaidi polisi hao hao wamekuwa ndo vinara wakubwa kwa matukio ya kuvunja sheria, bora cdm iendelee na mkakati wake na imani yangu ni kwamba huyo tendwa kazeeka ndo maana anatoa kauli zisizokuwa na maana.

Tutor B,

Ningependa urudi tena kwenye huu uzi ili ujibu swali langu!

Hivi, kati ya Tendwa na Dr Slaa ni nani ana umri mkubwa?
 
Last edited by a moderator:
Hapo ndipo sheria na katiba vyote viwili kwa pamoja vinapo vunjwa.

Kifungu gani cha katiba unachokizungumzia hapa wewe kilichovunjwa? ni sheria gani unayoizungumzia hapa iliyovunjwa? usiandike tu kwakuwa unapata ujira, twende kwa ushahidi wa katiba na sheria unazokaririshwa hapo lumumba.
 
Hammy-d naona una kazi kubwa ya kuwalazimisha wasomaji kwenda na ideology yako ya kutumia tochi kutafuta makosa ya cdm.
 
sasa wewe unaona tendwa ndio ana upeo mkubwa aliposema kuwa hawezi kuifuta ccm kwa sababu ni serikali hata kama itafanya kosa linapolekea kufutwa?
 
Hamy-D,
Ebu utusaidie. Wewe mwenye upeo mkubwa wa sheria kuliko Mbowe, utujulishe na Watanzania wajue ni sababu zipi zinampa Tendwa kufuta usajili wa Chadema. Tukusikie na tukupime Kama wewe na Mbowe ni yupi mwenye upeo mkubwa. Kwanini tunaandikia mate, labda kweli unaweza kusaidia wengi!

WanaJF!

Mwenyekiti wa CHADEMA taifa na mbunge wa jimbo la Hai, bwana Mbowe, amethibitisha kuwa yeye ana upeo mdogo sana kuhusu mambo ya sheria.

Bwana Mbowe amethibitisha hilo baada ya kueleza kuwa CHADEMA kufutwa haiwezekani kabisa na hiyo sababu aliyoitumia ndio kichekesho na imemdhalilisha kweli.

Sababu aliyoitoa bwana Mbowe ya kukingia chama chake kifua kuwa hakitaweza kufutwa na msajili si nyingine bali ni idadi ya wabunge, madiwani na wenyeviti wa vijiji.

Bwana Mbowe alieleza kuwa, "kufuta CHADEMA ni sawa na kufuta wabunge 49, madiwani zaidi ya 600 na wenyeviti wa vijiji zaidi ya 1000".

Kama bwana Mbowe angekuwa na maarifa kidogo sana ya sheria (kwa kupitia tu ile sheria ya vyama vya siasa) asinge weza kuongea hayo maneno ya ovyo kabisa kuhusu kufutwa kwa CHADEMA.

Ieleweke kuwa, chama cha siasa hakifutwi kwa kuangalia idadi ya wabunge, madiwani na hata wenyeviti wa vijiji waliotokana na chama hicho, bali kinacho angaliwa ni kama vigezo ama masharti yaliyo kwenye sheria yamevunjwa.
 
Unajua kijana you are too far from the truth!
Lissu alitoa sababu za kisheria za kwa nini CHADEMA haiwezi kufutwa katika vyombo vya habari!
Dr.Slaa akatoa sababu za kifalsafa na kisiasa kwa nini CHADEMA haiwezi kufutwa.
Marando akatoa sababu za jeuri kwa nini CHADEMA haiwezi kufutwa!
Mwisho Mwenyekiti Mbowe akatoa sababu as a visionary leader kwa nini CHADEMA haiwezi kufutwa...
KILA KIONGOZI ALITOA HOJA KULINGANA NA MUKTADHA NA HII NDIYO TEAM WORK....WHEN YOU COMBINE THEM ALL YOU GET THE LOGIC...OTHERWISE HAVE IT YOUR OWN WAY!

Mkuu heshima kwako,

Mkuu ingekuwa vyema kama ungeacha ushabiki badala yake uweke hayo mambo ya kisheria ambayo Lissu ameyasema.
 
Inawezekana kweli, lakini huyu anayeitwa tendwa ndo dodoki kabisa...sijui kiazi....
 
Back
Top Bottom