MUME MWEMA
JF-Expert Member
- May 16, 2013
- 327
- 44
Kwenye siasa hakuna adui na wala CCM haina maadui, hayo niliyoweka hapa ni marekebisho tu kwa mwenyekiti wa CDM kwamba ameenda chaka.
Greenguard ni maadui wa nani?
Kwenye siasa hakuna adui na wala CCM haina maadui, hayo niliyoweka hapa ni marekebisho tu kwa mwenyekiti wa CDM kwamba ameenda chaka.
Hamy-D,
Ebu utusaidie. Wewe mwenye upeo mkubwa wa sheria kuliko Mbowe, utujulishe na Watanzania wajue ni sababu zipi zinampa Tendwa kufuta usajili wa Chadema. Tukusikie na tukupime Kama wewe na Mbowe ni yupi mwenye upeo mkubwa. Kwanini tunaandikia mate, labda kweli unaweza kusaidia wengi!
maprosoo hawezi kujidhalilisha hivi.ndugu hujui hamy-d ni maprosoo,
Kusudi la msingi la sheria ni kulinda maslahi makuu ya umma sio kuendekeza utashi wa mtu mmoja dhidi ya wengi. Tendwa kama Tendwa mtu mmoja hawezi kuhukumu maslahi ya wabunge wote hao na wananchi walioko nyuma yao na pia kuiingizia serikali hasara ya kuitisha uchaguzi mwingine kwa kuunguza mabilioni ya pesa. Sheria gani za ovyo namna hiyo hazina hata prudence. Watu wanaandika katiba mpya ili kuongeza mambo mengine yenye maslahi mapana kwa jamii na inaweza kuibuka na pendekezo la kumfuta kabisa msajili wa vyama kwenye ramani ya siasa lakini sio cdm. Matakwa ya watu ndio sheria mama sio matakwa ya kibaraka mmoja na njaa zake.WanaJF!
Mwenyekiti wa CHADEMA taifa na mbunge wa jimbo la Hai, bwana Mbowe, amethibitisha kuwa yeye ana upeo mdogo sana kuhusu mambo ya sheria.
Bwana Mbowe amethibitisha hilo baada ya kueleza kuwa CHADEMA kufutwa haiwezekani kabisa na hiyo sababu aliyoitumia ndio kichekesho na imemdhalilisha kweli.
Sababu aliyoitoa bwana Mbowe ya kukingia chama chake kifua kuwa hakitaweza kufutwa na msajili si nyingine bali ni idadi ya wabunge, madiwani na wenyeviti wa vijiji.
Bwana Mbowe alieleza kuwa, "kufuta CHADEMA ni sawa na kufuta wabunge 49, madiwani zaidi ya 600 na wenyeviti wa vijiji zaidi ya 1000".
Kama bwana Mbowe angekuwa na maarifa kidogo sana ya sheria (kwa kupitia tu ile sheria ya vyama vya siasa) asinge weza kuongea hayo maneno ya ovyo kabisa kuhusu kufutwa kwa CHADEMA.
Ieleweke kuwa, chama cha siasa hakifutwi kwa kuangalia idadi ya wabunge, madiwani na hata wenyeviti wa vijiji waliotokana na chama hicho, bali kinacho angaliwa ni kama vigezo ama masharti yaliyo kwenye sheria yamevunjwa.
Dr.W.Slaa,Kwanza ningependa tukubaliane kuwa chama chochote chenye usajili wa muda na kilicho na usajili wa kudumu, vyote hivi vikikiuka masharti yaliyo kwenye sheria vinaweza kufutwa.baada ya hilo, sasa tuzungumze kuhusu CHADEMA, Dr Slaa wewe mwenyewe unafahamu fika kuhusu ulinzi unao zungumzwa kwenye katiba ya nchi na hata sheria mbalimbali za nchi.Kwenye sheria ya vyama vya siasa ulinzi wote unao hitajika kwenye shughuli yoyote ya chama husika ufanywa na jeshi la polisi.Hicho ambacho CHADEMA mnataka kukiimarisha kinatoa ishara ya kwamba mnataka kuunda kitu ambacho kitafanya majukumu kama ya jeshi la polisi, jambo ambalo ni kunyume cha sheria, na kwa mujibu ya kifungu cha 19 cha sheria ya vyama vya siasa, msajili anao uwezo wa kufuta chama bila ya kuhojiwa na chombo chochote.
wewe huko tofauti kabisa na fikra na sheria za tendwa maana wewe unasema chama chochote kinaweza kufutwa kikikihuka sheria lakini tendwa alishasema kuwa anaweza kuifuta chadema lakini hawezi kuifuta ccm maana ni serikali na akifanya hivyo itakuwa ni gharama kwa uchaguzi mwingine, kwa maneno hayo ya tendwa ni wazi kuwa ccm wanaruhusiwa kuvunja sheria, kutesa, kujeruhi, kuunda vikundi vyovyote hata kinyume na sheria lakini wataachwa sababu ni serikali. Ndio maana tunaona ccm wanafanya wanavyo taka lakini wanao kemewa ni wapinzani. Hebu tueleze ni sheria hipi ambayo ina kikingia kifua chama tawala au tuseme hii ni sheria ya tendwa na ccm?dr.w.slaa,
kwanza ningependa tukubaliane kuwa chama chochote chenye usajili wa muda na kilicho na usajili wa kudumu, vyote hivi vikikiuka masharti yaliyo kwenye sheria vinaweza kufutwa.
Baada ya hilo, sasa tuzungumze kuhusu chadema, dr slaa wewe mwenyewe unafahamu fika kuhusu ulinzi unao zungumzwa kwenye katiba ya nchi na hata sheria mbalimbali za nchi.
Kwenye sheria ya vyama vya siasa ulinzi wote unao hitajika kwenye shughuli yoyote ya chama husika ufanywa na jeshi la polisi.
Hicho ambacho chadema mnataka kukiimarisha kinatoa ishara ya kwamba mnataka kuunda kitu ambacho kitafanya majukumu kama ya jeshi la polisi, jambo ambalo ni kunyume cha sheria, na kwa mujibu ya kifungu cha 19 cha sheria ya vyama vya siasa, msajili anao uwezo wa kufuta chama bila ya kuhojiwa na chombo chochote.
Hamy -D,Sikuhitaji nadharia au hadithi ya alfu Lela ?.... Nilihitaji kujua 1) sheria zipi ambazo chadema imevunja kustahili kufutwa 2) je umesoma Barua ya Tendwa ya December 2004 na majibu yetu ya Januari 2005 na Majibu ya Tendwa ya 2005. Kama hujasoma huna msingi wa kujadili chochote, kwa kuwa hujui hata tulichokuwa tunajibizana na Tendwa. Ni mbaya zaidi Kama na barua yetu kwa Tendwa ya 16 July 2013. Kama umezisoma msaidie basi Tendwa kuzijibu kwa kuwa hata katika majibu yake ameendelea kupiga pori na porojo. Chadema hatuna muda wa Porojo. Tunaijui Sheria ya Nchi, tunajua majukumu yetu. Uwe mkeli uwaambie watanzania Kama umesoma barua hizo, na ili wakuamini jibu basi hoja alizoshindwa kujibu Tendwa.3) unaamini kuwa ulinzi wa mtu na makundi ni jukumu la polisi tu? Kama ni hivyo ni lini basi kila kay a itagawiwa askari wake, na wao wasihangaike kuweka walinzi wao? Hivi umeishawahi kuona Sheria inayohusu silaha nchi hii? Ebu tuelimishe inatoa masharti gani mtu mwenye kampuni kumiliki silaha kwa ulinzi wake na Mali zake, na inseam nini kuhusu watu wengi wanaomiliki bastola. Ni hatari kuwa vuvuzela bila kujua mambo ya msingi.4) Hivi unajua kuwa mahakama iliisha kutoa hukumu ya kutosimamisha uchaguzi mdogo wa Jimbo mmoja tu la Tunduru tu kwa kuogopa gharama? Sembuse wambunge 25 wa majimbo na wadi zaidi ya 600. Sasa Pima upeo wako na Mbowe ndio ujilinganishe Kama hamjui mam
WanaJF!