Kwa hii aibu niliyopata, naenda kujifunza Kiingereza

Hayo Mambo yananikutaga sana Mimi (Ni muisilam)

Wajihi wangu ni Mweupe (Brown) Niko na ndevu halafu zile ndefu za kiustadhi kabisa, na huwa navaaga na Baraka Shia (kofia). Watu wamezoea kuniita Mpemba ilhali ni Mnyamwezi Pure wa Tabora.

kwahio huwa nikihudhuria Shughuli za Dini (Misiba /Maulidi) hawakawii kusema Shekh hapo tunaomba Duwa. Hapo ndio shida hutokea sijui kusoma wala kuomba Duwa, Mara nyingi huwa ni kwa kiarabu.

Kiukweli naibikaga sana, uzuri natumiaga mbinu ya kudanganya kifua au Sauti haitoki.
 
Muonekano wangu umekaa kishua mtu akiniona tu anajua nina hela halafu naongea Kiingereza balaa.

Jana kuna mzungu kaja pharmacy ya mama mkwe kununua dawa sasa mama mkwe Kingereza akipandi akamtuma mtoto aje kuniita, nimefika dukani ile kumuona mzungu tu kimoyo moyo nikajisemea nimekwisha.

Kilichofata najua Mimi na Mungu wangu yes no, yes boss, yaah yaah ndio zilitamalaki hadi mama mkwe akaanza kucheka.

Hii aibu nzito sana. Kweli Mimi ni kiazi
lazima tujifunze mkuu hili ni balaa...
 
Mimi kuna siku nilijizolea point 3 kwa wapiga debe wa stand,kisa niliwatafsiria kuwa abiria alikua anaomba wamwandikie ticket coz alikua kwenye mizunguko ya kikazi na alitakiwa kupeleka risiti ofisini kwao.abiria mwenyewe alikua mmama wa kimarekani aliyekua anafanya utafiti wa masuala ya changamoto za usafiri kwenye majiji makubwa ya africa ikiwemo Dar es salaam.basi wapigadebe wakanishangilia hatari
 
Siku moja npo arusha posta kuu,mara ghafla wazungu wakike wawili hawa hapa mbele yangu wakanisalimia,wakatoa raman ya mji wa arusha wakaniuliza kama najua ilipo hotel waliyofikia ilikuwa inaonekana hapo kwenye raman,sikujua ilipo hyo hotel ila nilijibu kifupi sana,nilitaman niongee nao mengi zaidi hata niwasaidie kutafuta lakin ndo hvyo kidhungu changu mpaka ntumie nguvu nying wakawa wamesepa fasta nikabak najilaum nikijisemea inatakiwa hii lugha nipambane nayo

Mji wa arusha ukiwa na duka afu hujui kiingereza ujue kuna siku utaumbuka
 
Muonekano wangu umekaa kishua mtu akiniona tu anajua nina hela halafu naongea Kiingereza balaa.

Jana kuna mzungu kaja pharmacy ya mama mkwe kununua dawa sasa mama mkwe Kingereza akipandi akamtuma mtoto aje kuniita, nimefika dukani ile kumuona mzungu tu kimoyo moyo nikajisemea nimekwisha.

Kilichofata najua Mimi na Mungu wangu yes no, yes boss, yaah yaah ndio zilitamalaki hadi mama mkwe akaanza kucheka.

Hii aibu nzito sana. Kweli Mimi ni kiazi
Ungeongea ki swedish
 
Hakuna mbaya hapo, Zinedine Zidane hajui kuongea hiyo lugha ya malikia. Kuna inchi kibao tu za ulaya hawajui kuongea hiyo lugha, Kama vile warusi, wafaransa, wajurumani hata Spain
 
Wewe na mama mkwe wako mtauzaje famasi bila vyeti hamukumaliza form four na kusoma chuo cha afya.....mgejua angalau kiingereza cha kuanzia.
Kujua majina ya dawa na matumizi yake sio kujua kiingereza, wapo wengi tu lugha ya malikia haipandi
 
Wala sio aibu na usijione wewe ndio mwenye jukumu la kujua kiingereza, hata huyo mzungu naye inabidi ajifunze kiswahili mbona wenzake nyomi huku street wanaongea hadi kinyakyusa??
Lakini sio mbele ya mama mkwe, kheri kingepanda kwa muda tu baadae kikasepa!!
 
Poor thinking capacity,kesho akija msukuma anaongea kisukuma chake itakubidi uanze kujifunza kisukuma
 
Muonekano wangu umekaa kishua mtu akiniona tu anajua nina hela halafu naongea Kiingereza balaa.

Jana kuna mzungu kaja pharmacy ya mama mkwe kununua dawa sasa mama mkwe Kingereza akipandi akamtuma mtoto aje kuniita, nimefika dukani ile kumuona mzungu tu kimoyo moyo nikajisemea nimekwisha.

Kilichofata najua Mimi na Mungu wangu yes no, yes boss, yaah yaah ndio zilitamalaki hadi mama mkwe akaanza kucheka.

Hii aibu nzito sana. Kweli Mimi ni kiazi
Kuna jamaa humu aliweka post akisimulia jinsi alivyofedheheka ughaibuni alipoambiwa afungue kikao kwa maombi kwa kiinglishi. Kwa kweli duniani tunapitia changamoto za aina mbalimbali.
 
Muonekano wangu umekaa kishua mtu akiniona tu anajua nina hela halafu naongea Kiingereza balaa.

Jana kuna mzungu kaja pharmacy ya mama mkwe kununua dawa sasa mama mkwe Kingereza akipandi akamtuma mtoto aje kuniita, nimefika dukani ile kumuona mzungu tu kimoyo moyo nikajisemea nimekwisha.

Kilichofata najua Mimi na Mungu wangu yes no, yes boss, yaah yaah ndio zilitamalaki hadi mama mkwe akaanza kucheka.

Hii aibu nzito sana. Kweli Mimi ni kiazi
Usione aibu, lugha ya taifa ni kiswahili, tuliosoma shule za kata kinge hakipandi kama hawa wtt sikuhizi. Unaweza jifunza lkn
 
Muonekano wangu umekaa kishua mtu akiniona tu anajua nina hela halafu naongea Kiingereza balaa.

Jana kuna mzungu kaja pharmacy ya mama mkwe kununua dawa sasa mama mkwe Kingereza akipandi akamtuma mtoto aje kuniita, nimefika dukani ile kumuona mzungu tu kimoyo moyo nikajisemea nimekwisha.

Kilichofata najua Mimi na Mungu wangu yes no, yes boss, yaah yaah ndio zilitamalaki hadi mama mkwe akaanza kucheka.

Hii aibu nzito sana. Kweli Mimi ni kiazi
Yaah yaah yaah, ok ok ok
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom