Kwa herini wana MMU hamtaniona huku tena

Kwa herini wana MMU hamtaniona huku tena

Mama Mkwe siku hizi umetulia kweli. No more Ban. Umekuwa kama Laigwanan Edo baada ya kuonywa

Kwa jina lako tu nadiriki kuhakikisha kuwa wewe ni katika misukule. Angalia, usichafuwe jukwaa huku, nitakuja kukupa vidonge vyako kwenye siasa. Hapa ni rusha roho tu.
 
Kwa jina lako tu nadiriki kuhakikisha kuwa wewe ni katika misukule. Angalia, usichafuwe jukwaa huku, nitakuja kukupa vidonge vyako kwenye siasa. Hapa ni rusha roho tu.

Mama Mkwe tuliza munkari. Maisha hayaendi hivyo. Hongera kwa kutopigwa Ban kwa mda mrefu
 
MMU ni pasua kichwa na rusha roho juu.

Karibu siasani, huko mambo shwari hakuna pasua kichwa wala rusha roho.

Subiri kidogo, kule kuna bayana tu hakuna mapenzi, unaweza kuiaga JF moja kwa moja ukileta za kuleta, tena nakutahadharisha, kule uwe makini la sivyo utaiaga JF kabisa. Maana kule kuna misukule kibao, kalagabaho.

Mama yangu una mambo wewe! Kwema?
 
jaman si kaaga tu fukunyuku ya nn mmmh...byeee nami ntafukunyuliwa bureeee
 
Duuuuuuh wana mmu wana visa na wivu sana wanaona jukwaaa lao la maaaana, mtu kaaaaga vizuri tu anashambuliwa ka kutukana jukwaa
 
hapana wana MMU wanaustaarabu na ndio walio nitunza na kunilea kwa mawazo yao mpaka nimefika hapa na kuniwezesha kupata kilicho chema.ndio maana niliona itakuwa vibaya sana kuondoka kimyakimya bila kuwaaga.

Tokea muda ulioanza kuaga, saa hizi ungekuwa ushafika siasani. Kama hujisikii kuondoka we baki tu.
 
nilicho kipata huku ni kikubwa sana kushinda ripoti hii unayo nipa. niliomba ushauri kwenu kupitia thread ya SIJUI LINI NITAPATA MKE MWEMA. kweli nikashauriwa na sasa nimesha mpata mwenza mwenye tabia njema ambaye tutafunga ndoa miaka ljayo.kwa sababu hiyo nimeona ni vibaya kuondoka kimya kimya bila kuaga.

Hongera na nakutakia maisha mazuri ya siasa za bongo.
 
embu mtaje nikusaidie kuthaminisha aya taja ,..... hata wenye michepuko wana ndoa nzuri sana na ni wazuri sana ila ndo hivyo tu

samahani sana miss chaga. Nimetoka kumuuliza sasa hivi ya kwamba nimtaje au nisimtaje lakini kanisisitiza sana nisimtaje kwani anaogopa kusumbuliwa na baadhi ya wana JF.wasiokuwa waaminifu kwa PM zao.naomba uniwie radhi kwa hili.
 
Tokea muda ulioanza kuaga, saa hizi ungekuwa ushafika siasani. Kama hujisikii kuondoka we baki tu.

leo ni siku yangu rasmi ya kuagana nawana MMU.kuanzia kesho na kuendelea sitakuwepo huku tena.kwa hiyo nataka kuagana nao vizuri mama sijawahi kugombana na mwana MMU yoyote mimi mtu wa amani tu.
 
Mmmh hebu ngoja kwanza nipekenyue ushiriki wako hapa MMU nione kama kweli wastahiki kuaga au tukuache tu uende zako...

anahitaji kick huyo achana nae ongalia hata tarehe ya kujiunga
 
kijana unaondoka saa ngapi utuandae hafla fupi tujipigie vifungu vyetu sie!!!

hebu sema bana, unajuamjini kila kitu dili.....!!!!!

ukizaliwa, dili!

ukifa, dili!

ukiumwa, dili!

kila kitu ni dili siku hizi!

kesho ndo siku yangu ya kuingia rasmi jukwaa la siasa na katiba mpya.leo ni siku yangu rasmi ya kuagana na wana MMU.
 
Mbona unaweza uktumia majukwaa yote tu kuingia jukwaa lingine hadi uage?
 
Mbona unaweza uktumia majukwaa yote tu kuingia jukwaa lingine hadi uage?

mshika mawili moja humpony'oka. sasa sijui mshika mengi itakuwaje. huwezi kutumikia majukwaa yote vile ipasavyo kwa wakati mmoja.
 
kweli mkuu huku hapafai ubongo wako utadumaaa.

sio kwamba hapa hapafai ila wapo wachache wanataka kupafanya hapa pawe hapafai.lakini ukiwa humu unahitaji kuwa na hekima na uvumilivu wa hali ya juu maana usipo kuwa makini unaweza kujikuta unapigwa ban kila siku.
 
SAYANSIKIMU usisashau basi kuwaaga wakwe zako utakapofunga ndoa na mke wako. Waambie hivyo hivyo kwamba ulichokuwa unatafuta kwao umeishakipata kwa hiyo hutokanyaga tena kwao. Ukifanya hivyo utakuwa umekamilisha zoezi la kuaga.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom