Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,516
Nawasalimu waungwana wote wa JF,
Nimesoma mahali kuwa CHADEMA wameanza kupokea ruzuku za kila mwezi zinazotokana na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. Ulikuwa ni msimamo wa CHADEMA kuwa uchaguzi mkuu wa 2020 haukuwa halali na ulikuwa uchafuzi na si uchaguzi. Kutokana na kutokuwa halali, ulikuwa ni msimamo wa CHADEMA kuwa mazao yote ya uchaguzi huo: Wabunge wa kuchaguliwa na wale wa viti maalum pamoja na ruzuku yalikosa uhalali.
Rais Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe 'wamefanikisha na kuasisi' maridhiano ya kitaifa ya kisiasa ambayo yapo kwenye utekelezaji unaotia matumaini na nguvu ya kusonga mbele tukiwa wamoja kama taifa. Pamoja na kubatilishwa katazo la mikutano ya hadhara ya kisiasa, Rais Samia anaonyesha kwa vitendo utekelezaji wa maridhiano hayo. CHADEMA nao hawako nyuma. Wameanza mikutano yao ya hadhara na kupokea ruzuku.
Leo hii, Rais Samia ni Mgeni Rasmi kwenye Kongamano la Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA) (katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani) huko Moshi, mkoani Kilimanjaro. Sasa ni dhahiri kuwa maridhiano yanaleta mapatano; amani; utulivu; ustahimilivu wa kisiasa; msamaha na ustawi wa kidemokrasia. Ni wakati sahihi wa akina Halima Mdee kusamehewa na kurejeshwa kundini CHADEMA, kama wako tayari kwa jambo hilo.
Akina-Halima Mdee ambao walifukuzwa uanachama wa CHADEMA na sasa wako Mahakama Kuu ya Tanzania kusaka haki yao, hata kama walikuwa na makosa na ukakasi wa kuteuliwa kwao kuwa Wabunge wa Viti Maalum wanasameheka. Ni wakati wa zama mpya. Ni wakati wa kuwa pamoja. Binafsi, mbele ya Rais Samia huko Moshi, naitarajia kauli ya CHADEMA kupitia Mbowe au mwingine kuwa akina Halima Mdee wamerudishwa kundini. Kesi yao nayo yapaswa kuondolewa mahakamani. Halafu, heshima;kufuata utaratibu; nidhamu na adabu zinapaswa kutembea nao popote.
Kila la heri Wanawake wote wa Tanzania katika kuadhimisha siku yao!