mkuu hata hio kodi uliokuwa unaangalia na kuscratch ni iptv pia. iptv inamaanisha tu internet protocal television au kwa lugha rahisi kuangalia tv kwa kutumia bundle lako la internet.
kuangalia tv kwa internet ili isikusumbue ionyeshe vizuri bila kunata nata unahitaji mambo matatu.
1. server ya uhakika ambayo hizo tv zime hostiwa
2. internet yenye speed ya uhakika kulingana na quality unayoplay
3. internet iwe na ping ndogo.
kwa uzoefu wangu internet nzuri ya kuangalizia tv online ni vodacom 3g na 4g, halotel 3g na tigo, smart, ttcl na smile 4g. 4g zote zina ping ndogo na 3g ya voda na halotel zinajitahidi.
nenda playstore download app inaitwa speedtest kisha pima speed yako. angalia mtandao unaokupa ping chini ya 50ms huo utafaa kustream na download speed angalau mbps kadhaa. ukifanikisha hapa utakuwa umesolve point ya pili na tatu kwenye list hapo juu
point ya kwanza huwezi kusolve wewe bali mhusika mwenye hizo tv alieziweka online. tumia chanell zetu za kitanzania itv na azam tv kama standard, nyingi ukiwa na internet nzuri hazita scratch hivyo zikiwa hazi scratch na unakutana na tv nyengine inascratch inamaana hio tv nyengine itakuwa kwenye server mbovu na sio internet yako.
kwakua ndio unaanza, test hizo za kitanzania kwenye vlc, copy hizo url kisha kwenye vlc click file halafu chagua network stream kisha paste hio url na play (kwa pc). vlc ya simu au mx player pia zina uwezo wa kustream hizo url.