Kuwa makini anayechapa kadi ya harusi

marcoveratti

JF-Expert Member
Sep 21, 2017
967
1,693
Bibi Harusi alienda stationary aliomba achapiwe 1 Yohana 4:18 kwenye CARD YA HARUSI lakini mchapaji alifanya kosa kwa kutoweka "1" kabla ya Yohana hivyo akachapisha Yohana 4:18_

1 Yohana 4:18 inasema "Katika pendo hamna woga, bali pendo lililo kamili hufukuza hofu zote"_

Lakini Yohana 4:18 inasema "Kwa maana umekuwa na waume watano hapo awali, na huyu uliye naye sasa si mume wako"

Bado tuko mahali hapa kusuluhisha, bado tunamsihi Bwana Harusi kuwa kosa ni la mchapaji wa stationary siyo Bibi Haru
 
Muwe mna quote na maneno kabisa, ukiweka mstari sidhani kama kuna m Tanzania atakayejipa shida ya kusoma Bible.
 
Bibi Harusi alienda stationary aliomba achapiwe 1 Yohana 4:18 kwenye CARD YA HARUSI lakini mchapaji alifanya kosa kwa kutoweka "1" kabla ya Yohana hivyo akachapisha Yohana 4:18_
Kwanini alikwenda Bibi Harusi, kitu gani kilimfanya .Bw Harusi asiende? Tuanzie hapo
 
Back
Top Bottom