In Loving memory of Zai, Rey, Justine, Lily, Rafael (ulikua rafiki halisi, sitasahau siku ile uliponiita na kunishika mkono na kunieleza, Elli jikinge, nakufa kwa AIDS! Mdomo wako ulikua umejaa vidonda, ulishindwa kula na kinywa chako kilijaa harufu mbaya), Nakukumbuka pia Dada na Rafiki yangu Vero, sikuamini kwamba siku ile ingekua mwisho wa kuonana na wewe Dada yetu, mchana ule ulinituma nikamuite Muinjilisti Gaddy! Nilikuja nae, tukasali pamoja, ukatubu! Kisha kesho yake ukapumzika kwa amani.
Sitakusahau classmate wangu Pili, uliondoka ukiwa mdogo! Hukufaidi hata matunda ya kusoma kwako! Ulianza matibabu na mshahara wako wa kwanza!
Kaka yangu Chris, mara ya mwisho nilikupeleka Ocean Road Hospital, kwakua kinga zako zilikua chini sana walishindwa kuendelea na mionzi, on that morning ya January 2013 nilifika Ocean Road kukuona, nikakuta kitanda kitupu! Maumivu yake hayaelezeki
Kwako Aunt G, pumzika! Hakika ulipigana Vita vigumu! Mapele, majipu, mkanda wa jeshi na kuchanganyikiwa yote haya yaligeuka kuwa sehemu ya maisha yako! Sitasahau simu ya Kaka Gasper siku ile Jumatano SAA tano asubuhi, Elli, Aunt G amepumzika daima! Dah
Vijana wangu AIDS is real