Sheria ya Vileo Sura ya 77 ya Mapitio ya Sheria za Tanzania ya mwaka 2002

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,653
11,657
1. KILEO NI NINI
Kileo kimeelezewa na sheria kuwa katika makundi mawili [Section 2-(a) (b)

[a]mvinyo, bia, pombe nyeusi ya kizungu (porter), cider-kinywaji kinachotengenezwa kwa kusindika matofaa (apple), hop beer-tafsiri yake ni mti wenye maua unaotumiwa kutengenezea pombe ya kizungu na kinywaji chochote ambacho kilevi chake ni zaidi ya asilimia mbili isipokuwa dawa inayotolewa kwa nia njema ikiwa na kilevi kama kilivyotafsiriwa na sheria, inayotolewa au kuuzwa na mtu aliye pitishwa kama mtaalam katika fani ya udaktari,au ufamasia au imetolewa na mtu yoyote kwa ajili ya dawa au matibabu.

-La msingi ni kwamba kinywaji chochote chenye kilevi zaidi ya asilimia mbili ni kileo

-Isipokuwa dawa inayotolewa/kuuzwa na mtaalam/Daktari/famasia/mtu yoyote

Vile vile sheria imetaja Spirit/pombe kali ya aina yoyote mbali na zile za viwandani kama zilivyotafsiriwa na kifungu cha 2 cha sheria hii lakini haijumuishi pombe za kienyeji au Moshi.Pengine kuna watu hawajui Moshi ni nini,hii ni pombe yenye jina maarufu kama Gongo kwa Tanzania,Kenya inajulikana kama Chang’aa.Hii imepigwa marufuku na ni haramu.

Sheria imetafasiri pombe ya kienyeji kumaanisha, pombe,asali iliyovundikwa[wanzuki],tembo,ulanzi na pombe zote zinazoandaliwa na watu wa asili ya Tanzania ambazo kilevi chake ni zaidi ya asilimia moja na pombe yoyote ambayo Waziri ataitangaza kuwa ni pombe ya kienyeji.

2. MAMLAKA ZA UTOAJI WA LESENI KWA BIASHARA ZA VILEO

Mamlaka ya kutoa Leseni yako chini ya Serikali za Mitaa ambapo halmashauri za Wilaya na Miji ndizo hutoa leseni husika

3. AINA ZA LESENI ZA VILEO

a] Leseni za kuuza jumla

MUDA WA KUUZA- Saa mbili asubuhi hadi saa moja usiku katika siku za kawaida na siku za juma mosi na jumapili na sikukuu saa tatu kamili asubuhi hadi saa sita mchana

b] Leseni ya kuuza Rejareja kwa Watumia vileo wanaoondoka navyo

c] Leseni ya kuuza rejareja kwa wateja wanaokunywa hapohapo

Hawa wana ruksa ya kuuza vileo kuanzia saa kumi na mbili jioni hadi saa tano usiku kwa siku za jumatatu hadi ijumaa

-Hii inamruhusu mteja kununua kileo na kunywa papo hapo au kuondoka nacho

Kama sheria imekataza kwamba muda Fulani sehemu ya kuuzia vileo isifunguliwe, sehemu hiyo itafungwa na itafungwa ili watu wote wasiweze kuingia na mtu yoyote, isipokuwa mtu aliyepewa leseni, familia yake,au wafanyakazi wake wataruhusiwa kuwa katika eneo hilo au kuruhusiwa kuwa hapo au kuingia na hakuna kileo chochote kutoka popote kitakachoruhusiwa kutumiwa katika eneo hilo kabla ya muda halali kisheria.

MUDA UNAORUHUSIWA KWA KUUZA VILEO KWA WAUZAJI WA REJAREJA KWA WATEJA WANAOKUNYWA HAPO HAPO

-Kwa maeneo ya mjini: JUMATATU-IJUMAA=Saa kumi na mbili jioni mpaka saa tano usiku

WIKIEND NA SIKUKUU=Saa Tano asubuhi mpaka saa sita usiku-Kwa maeneo ya vijijini=JUMATATU TO IJUMAA-Saa Tisa jioni mpaka saa mbili usiku.

WIKIEND NA SIKUKUU=Saa nane mchana mpaka saa Tano Usiku

d]Zipo aina nyingine za leseni kama leseni za kuuza vileo kwenye hoteli kwa ajili ya wateja wa hotel,Leseni kwa ajili ya kuuza kileo kwenye Mgahawa,Leseni ya kuuza kileo kwenye Mabehewa ya Treni,Leseni ya kuuza vileo kwenye Meli za abiria,Leseni kwa ajili ya klabu,Leseni kwa ajili Kantini etc.

6. JE KUNA UTARATIBU UPI WA KUTOA LESENI ZA VILEO CHINI YA SHERIA HII

SECTION 36

-Maombi ya leseni yatapelekwa na kusikilizwa na mamlaka husika iliyo na malaka ya kutoa leseni katika mahala hapo na mamlaka hiyo inao uwezo wa kukubali au kukataa kutoa leseni hiyo.Huyu mara nyingi huwa ni Afisa Biashara.Mamlaka hayo ya utoaji leseni ina mamlaka ya kukubali au kukataa maombi ya Leseni.

-Maombi hayo yanatakiwa yawe na ushahidi wa maandishi au maelezo ya maandishi ya kuridhisha kwa mamlaka ya utoaji leseni kuhusu kulipa au kutolipa kodi ya Mapato

-TAARIFA KUHUSU MAOMBI YA LESENI

Baada ya kupokea maombi ya leseni, mamlaka husika inayotoa leseni inawajibika kuwataarifu wafuatao

1. TAARIFA IPELEKWE POLISI

-Afisa wa cheo cha juu wa polisi ambaye itabidi ayapitishe maombi husika baada kwa kuwa wao ndio wanaohusika na masuala ya Usalama katika maeneo husika,hivyo pamoja na mambo mengine,watatoa ushauri kuhusu hali ya usalama endapo baa husika itafunguliwa.Afisa muhusika ataripoti kimaandishi kwa mamlaka inayohusika na utoaji wa leseni kuhusiana na mambo husika.Lakini mamlaka inayotoa leseni inao uwezo wa kumuhitaji Afisa wa Polisi muhusika aje mbele yake siku ambayo maombi ya leseni yanaposikilizwa.

*Hii itasaidia kupunguza uhalifu na uovu mwingine kwa kuwa watakuwa na taarifa za awali kuhusu eneo husika.

-Vilevile Mamlaka ya leseni inao uwezo wa kuomba Ushauri wa mamlaka ya juu wa Polisi.

2. TAARIFA IPELEKWE KWA AFISA TABIBU

-Kwa kuwa maeneo yenye mikusanyiko ya watu yanahitaji tahadhari ya Afya, maombi ya leseni lazima yapitie taratibu za afya.

Afisa wa Utabibu wa eneo husika au Afisa tabibu anayekaimu nafasi ya Afisa tabibu,huyu naye lazima apitishe baada ya kuangalia mazingira ya afya ya eneo husika,pengine ikijumuisha ufanyaji wa ukaguzi wa masuala ya afya kama maliwato,maji na mengineyo.

Mamlaka ya leseni inaweza kupokea ripoti ambayo itapelekwa kwake na Afisa Tabibu au msaidizi wake. Pamoja na hayo vilevile Mamlaka ya leseni inao uwezo wa kutaka ushauri wa Afisa wa Juu wa Afya

-Na kabla ya kusikiliza maombi hayo, mamlaka husika inatakiwa kuyabandika maombi katika ofisi yake kwa muda wa siku 14

-Mamlaka ya leseni inaweza kupokea ripoti ambayo itapelekwa kwake na Afisa Tabibu au msaidizi wake. ]

3. MWENYEKITI WA KAMATI YA MAENDELEO YA KATA

4. AFISA ARDHI

5. AFISA BIASHARA

TISI YA KUSIKILIZA MAOMBI YA LESENI
-Mamlaka ya Utoaji wa leseni itatoa notisi ya siku kumi na nne kuhusu siku ya kusikiliza maombi ya leseni.Hii husaidia muomba leseni na watu wengine kijiandaa kuleta hoja zao

7. JE MWANANCHI AU MTU YEYOTE ANAWEZA KUWEKA PINGAMIZI DHIDI YA KUTOLEWA KWA LESENI YA VILEO

Ndio-Fungu la 39

Katiba ya Jamhuri ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Ibara ya 16(1) inasema kwamba kila mtu ana haki ya kuheshimiwa na kupata hifadhi ya nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na unyumba wake, na pia heshima na hifadhi ya maskani yake na mawasiliano yake binafsi.

Ibara ya 30 [1] Inasema kwamba inasema kwamba haki na Uhuru wa Binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na Uhuru wa watu wengine au maslahi ya Umma.

Kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu kutaka au kuomba kufungua baa katika maeneo ambayo aidha yako karibu na shule, hospitali bila kujali kwamba kuna wagonjwa, au karibu na makazi ya watu hivyo kuwafanya waathirike moja kwa moja na kelele za muziki au za wanywaji wa vileo.

Vile vile baa nyingi katika mikoa yenye shughuli nyingi zimevamiwa na makahaba ambao hujiuza na kufanya shughuli zao katika baa hizo na baadhi ya shughuli hizo huvuka mipaka na kufika katika makazi ya watu ambao huishi na watoto wao. Kutokana na mambo wanayoyafanya makahaba hao, familia nyingi hufadhaika.

Mambo mengine yanayotokea kwenye biashara hii ni ufunguaji wa biashara za vileo ovyo ovyo, huku zikipiga muziki Mzito usiku kucha, Madisko yanayopigwa maeneo yasiyo rasmi i.e ya wazi usiku kucha.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 26(2) Inasema kwamba kila mtu ana haki, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria, kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha hifadhi ya Katiba na sheria za nchi.

Hivyo basi sheria hii inawapa nafasi ya kupinga mtu Fulani kupewa leseni mpya au ku-renew leseni yake.Hii husaidia kuondoa kero .Huivyo basi sheria imetoa nafasi ya kuweka pingamizi kwa mamlaka za utoaji wa leseni dhidi ya muombaji husika.

Mtu yeyote ambaye anapinga utolewaji wa leseni atafanya pingamizi lake hilo liwe katika maandishi na ataliopeleka kwa katibu wa mamlaka hiyo ya utoaji wa leseni kabla ya siku ya kusikilizwa kwa maombi hayo ya leseni, na baada ya kuwekwa kwa pingamizi hilo, taarifa ya kimaandishi ya sababu za kupinga utolewaji wa leseni atapatiwa mtu huyo anayeomba kupewa leseni siku tatu kabla ya kusikilizwa kwa maombi ya leseni

Lakini pingamizi linaweza kuletwa hata siku hiyo ya kusikilizwa kwa maombi ya leseni

KUBADILISHWA KWA MAOMBI YA LESENI
Mamlaka husika ina uwezo wa kumruhusu muomba leseni ayabadilishe maombi yake kama itaonekana inafaa na mamlaka husika itamruhusu abadilishe.Mamlaka hiyo ya leseni itatoa taarifa kwa Umma juu ya mabadiliko ya maombi kama itakavyoonekana inafaa.

RUFAA-section 42

Sheria inampa nafasi ya kukata rufaa mtu yeyote ambaye hajaridhishwa na uamuzi wa mamlaka ya leseni.Hivyo basi mwananchi na muomba leseni wote wana haki ya kukata Rufaa.

A] Mtu yeyote ambaye haukuridhishwa na uamuzi wowote uliotolewa chini ya sheria hii na Mamlaka ya leseni ya Kijiji atatakiwa akate Rufaa ndani ya siku thelathini kutoka tarehe uamuzi ulipotoka kwenda kwenye Mamlaka ya Rufaa ya Wilaya kilipo kijiji hicho.

Wajumbe wa kamati ya Rufaa ya Wilaya ni wafuatao

-Mkuu wa Wilaya ambaye atkuwa ndie mwenyekiti

-Mkuu wa Polisi wa Wilaya

-Mganga mkuu wa Wilaya

-Afisa Usalama wa Wilaya

-Mhasibu wa Wilaya ambaye ndiye atakuwa katibu wa kamati

-Wajumbe wengine wawili walioteuliwa na halmashauri ya wilaya

B] Mtu yeyote ambaye hajaridhishwa na maamuzi ya Mamlaka ya leseni ya Eneo la mjini naye anatakiwa ndani ya siku thelathini akate Rufaa kwenda kwenye Mamlaka ya rufaa ya Mkoa husika

Wajumbe wa kamati ya mkoa ya Rufaa wanajumuisha

-Mkuu wa mkoa ambaye atakuwa mwenyekiti

-Kamanda wa Polisi wa Mkoa

-Mganga Mkuu wa Mkoa

-Afisa Usalama wa Mkoa

-Mhasibu wa Mkoa ambaye ndiye atakuwa katibu wa kamati

-Wajumbe wengine wawili watakaoteuliwa na Kamati ya maendeleo ya Mkoa

c] RUFAA KWA WAZIRI

Waziri ana mamlaka ya kusikiliza Rufaa kutoka mamlaka ya Miji kuhusu maamuzi yake yoyote na anaweza kuukubali,kuukataa au kuubadilisha uamuzi huo

LESENI
Leseni zote zitatolewa na Mwenyekiti waq mamlaka ya leseni ya vileo

SHERIA HAIRUHUSU LESENI ITOLEWE AU KUHAMISHIWA KWA

-Mtu mwenye miaka chini ya isshirini na moja

-Mtu aliyetangazwa mufilisi

-Mtu yeyote ambaye leseni yake alinyanganywa mpaka miaka miwili ipite

-Mtu yoyote ambaye kwa kipindi chochote alishawahi kufungwa kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita

-Kwa mtu yeyote ambaye alipatikana na hatia ya kuuza kileo bila leseni

KUONGEZEWA MUDA WA KUUZA VILEO

Mamlaka husika ya utoaji leseni ina uwezo wa kuongeza muda wa kuuza vileo katika mazingira maalumu,na mamlaka ya leseni inao uwezo wa kumpa mwenyekiti au mmoja wa wajumbe wa mamlaka ya leseni kuongeza muda wa leseni ambaye atashughulikia kazi hizo.

8. JE WAZIRI MWENYE DHAMANA ANA MAMLAKA YAPI YA KUDHIBITI BIASHARA YA VILEO

1. KUPUNGUZA MUDA WA KUUZA VILEO

Waziri anaweza,kwa amri iliyotolewa kwenye gazeti la serlkali,akapunguza masaa ya kuuza vileo katika eneo lolote la biashara Tanzania na baada ya Amri hiyo kutolewa,masaa yaliyotajwa katika amri hiyo yatakuwa ndio masaa halali ya

kuuza vileo.

Ss 64 inasema kwamba endapo Waziri atatoa amri ya kupunguza masaa ya kuuza vileo, anaweza kuelekeza mamlaka ya leseni husika yenye mamlaka katika eneo husika kurudisha fedha za mtu aliyeomba leseni. Kama ambavyo itaonekana inafaa.

2. KUFUTA LESENI
Kama Waziri akiridhika kwamba mtu aliyepewa leseni

a) Amepatikana na hatia chini ya kifungu cha sheria namba 76 cha sheria hii ambacho kinapiga marufuku maeneo yaliyopewa leseni za kuuza vileo kufanywa danguro

b) Anaruhusu eneo lake lililopwewa leseni ya biashara mara kwa mara litumke kama sehemu ya makutano au sehemu wanayoenda mara kwa mara watu wanaodhaniwa kuwa ni/wana sifa ya ukahaba ya makahaba au watu wanaovaa mavazi yasiyofaa au

c) Anaruhusu eneo lake lililopewa leseni mara kwa mara litumike kama eneo la kukutana au kutembelewa mara kwa mara na watu ambao wanajumuisha au wanasadikiwa kujumisha hatari kwa usalama, amani anutulivu wa Jamhuri ya Muungano

Anaweza, Kwa amri iliyotolewa kwa mkono wake, kufuta leseni ya muhusika.

Kufutwa Kwa leseni huko na Waziri, kutakuwa kwa mwisho na hakutakuwa na haki ya rufaa isipokuwa Waziri husika anaweza kuweka masharti kama atakavyoona inafaa kuweka, kumrudishia leseni mtu yeyote aliyefutiwa leseni chini ya kifungu hiki.

KUONYESHA LESENI YA BIASHARA
Ss 73Mtu yeyote ambaye amepewa leseni anatakiwa aonyeshe katika eneo la kuingilia katika eneo lake la biashara katika njia njia kama alivyoelekezwa na mamlaka ya leseni husika aonyeshe jina lake yakifuatiwa na neon”anmeruhusiwa” na maneno ya kutosheleza ambayo kwa mawazo ya mamlaka ya utioaji leseni,yataonyesha hali ya leseni yake na kama leseni yake inmruhusu kuuza vileo ili wanunuzi wavinywe hapohapo au waondoke navyo,na mtu yeyote aliyepewa leseni akishindwa kufanya hivyo atakuwa ametenda kosa la jinai.

9. JE SHERIA IMEWAANGALIAJE WATU WA UMRI WA CHINI ILI WASIATHIRIKE NA MASUALA YA VILEO

Section 69-70

A.] KUMUUZIA VILEO MTU WA UMRI WA CHINI YA MIAKA 16

Sheria inasema kwamba ni kosa la jinai kumuuzia kileo mtu yeyote mwenye Umri chini ya miaka 16 na atakayefanya hivyo atakuwa ametenda kosa la jinai.Sheria hii inaendeleza mgongano na sheria nyingine zinazomuelezea mtoto kwamba ni Mtu wa umri gani.

B.] KUMUAJIRI MTU ALIYE CHINI YA MIAKA 16
Mtu aliyepewa leseni ambaye atamuajiri mtu aliye chini ya umri wa miaka 16

-kuuza au kusimamia au kuangalia uuzaji wa vileo

-kutunza au kuangalia kileo chochote katika eneo lake anatenda kosa la jinai

C]. KURUHUSU MTU ALIYE CHINI YA MIAKA 16 KUKAA ENEO LINALOUZWA VILEO.
-Mtu yeyote aliyepewa leseni akimruhusu mtu ambaye anaonekana yuko chini ya umri wa miaka 16 kuwa katika eneo lake lililopewa leseni katika chumba,Ua uwanja au eneo lolote ambalo vileo vinahudumiwa kwa ajiri ya kunywa anatenda kosa la jinai lakini sharti hili halitawagusa watu wa migahawa ,vyumba vya kula vya hotel,vyumba vya mapumziko vya hotel au chumba cha kula ambapo vileo vinatumiwa katika eneo lililopewa leseni ambalo sio mgahawa,chumba cha chakula au chumba cha mapumziko au eneo lolote katka chumba au eneo lolote katika eneo lililopewa leseni ya kuuza vileo,anakuwa ametenda kosa la jinai.

10. JE, SHERIA INARUHUSU ULEVI ULIOKITHIRI KATIKA MAENEO YALIYOPEWA LESENI YA KUUZA VILEO

Makosa chini ya fungu hili -KURUHUSU ULEVI WA KUPINDUKIA

-KUMUUZIA MTU ALIYELEWA

-KUMPA KILEO ZAIDI MTU ALIYELEWA

-KUMHAMASISHA AU KUMSISITIZA AENDELEE KUNYWA

-KUFANYA VURUGU KTK ENEO LINALOUZWA VILEO

Katika jukumu lake la kulinda afya za wananchi na vilevile kudhibiti ulevi uliokithiri, sheria imempa jukumu mmiliki wa leseni ya kuuza vileo kwa wateja wanaotaka kuvinywa palepale wasilewe kupita kiasi.Ukizingatia kwamba ulevi ndio chanzo cha ajali nyingi za barabarani, ugomvi mitaani,baa na hata kwenye ndoa.Vilevile janga la sasa la maambikizi ya ukimwi ambalo kwa mtu aliyelewa kupita kiasi hushindwa kufanya maamuzi sahihi na hivyo kupata maambukizi.

Hivyo basi wale ambao wamezoea kukaa katika baa kuanzia asubuhi mpaka jioni na wakiwa wamelewa chakari au wale ambao wamelala kwenye meza za baa kwa sababu ya ulevi wanamtia matatani mwenye baa husika na hivyo anawajibika kwa kuwafanya wawe walevi.

Hivyo basi kwa mujibu wa fungu la sheria la 74 la sheria hii kuruhusu ulevi wa kupindukia katika eneo aliloruhusiwa kuuza vileo anafanya kosa la jinai.

Fungu hilo hilo la sheria linasema kwamba mmiliki wa leseni ya kuuza vileo ili vinyewe hapo hapo atakuwa anafanya kosa la jinai endapo atamuuzia au kumpa kileo zaidi mtu ambaye anamuona ameshalewa au kwa njia moja au nyingine anamhamasisha au kumsisitiza mtu yeyote aendelee kunywa pombe ilihali amelewa anakuwa ametenda kosa la jinai.

Hivyo basi ni kosa la jinai kumpa pombe mtu ambaye amekwishalewa.Kuna dalili mbalimbali za kuonyesha kwamba mtu fulani ambaye ni mteja wa vileo katika eneo lako amelewa.Dalili hizo zinajumuisha mteja kusinzia kwenye meza na hata kuyumbayumba,au kutoa hotuba kwa watu wasiomsikiliza na vitendo vinavyohusiana na hivyo.

Sheria hii vilevile inazuia mtu anayemili8ki leseni ya kuuza vileo kuruhusu vitendo vya vurugu kwenye eneo lake aliloruhusiwa kuuza vileo

Sheria itampa nafuu muhusika dhidi ya tuhuma hizo kama atathibitisha kwamba yeye mwenyewe au watumishi na wasaidizi wake walichukua hatua za kuzuia ulevi huo.

Ss 74.Mtu yeyote aliyepewa leseni ambaye ataruhusu ulevi wa kupindukia(drunkenness) au vitendo vya vurugu katika eneo lake la biashara lililopewa leseni au ambaye anamuuzia au kumpa kileo kwa mtu ambaye ameshalewa,au kwa njia moja au nyingine anamhamasisha au kumsisitiza mtu yeyote anywe kileo anatenda kosa la jinai.Na kama mashauri ya jinai katika kifungu hiki yatathibitisha kwamba mtu huyo alikuwa amelewa katika eneo hilo lililopewa leseni,mtu aliyepewa leseni atakuwa ametenda kosa la jinai la kumpa pombe kwa mtu ambaye alikuwa amekwisha lewa vinginevyo athibitishe kwamba alichukua hatua yeye mwenyewe au kupitia kwa watu aliyewaajiri kuzuia ulevi huo

11. JE MTU ALIYEPEWA LESENI YA KUUZA VILEO ANA UWEZO WA KUZUIA WALEVI NA WATU WENGINE KWA MFANO WALIVAA MAVAZI YASIYO YA STAHA WASIINGIE KWENYE ENEO LAKE LA BIASHARA

INDECENT-Si adabu, heshima, ustahi, siofaa, chafu, utovu wa adabu, heshima ustahi, jambo lisilofaa:

Ndio.-Maadili na heshima-Lakini hata wahudumu wao wanavaa vibaya: Tungeanza na wahudumu wao wawe wanafuata sheria halafu ndio wateja.Kwa kuwa imekuwa kana kwamba ndio qualification ya mhudumu kuvaa nguo isiyo na staha kabla ya kutoa huduma.kwa kuwa kama hana mavazi ya staha atamtoa vipi asiye na mavazi ya staha.

KUVAA VAZI LA STAHA KABLA YA KWENDA SEHEMU INAYOUZWA VILEO NI LAZIMA
Ili kuepukana na madhara yatakayosababisha na kifungu hicho hapo juu, Kifungu cha 75 cha sheria kinampa mamlaka mmiliki wa leseni ya vileo endapo anajua tabia ya mteja wa wake kutokana na kumfahamu.

A] Kukataa kumruhusu mteja husika asiingie kwenye eneo lake la kuuzia vileo

B] Anaweza kukataa kumuhudumia muhusika

C] Vilevile ana uwezo wa kumuondoa katika eneo lake la kuuzia vileo kwa kutumia nguvu kiasi mtu yeyote mlevi au mleta vurugu au mwenye vurugu katika eneo husika

D] Sheria vilevile katika kifungu hiki inampa nguvu mmiliki wa leseni kumzuia mtu ambaye haruhusiwi kuuziwa pombe hawa wanajumuisha watoto walio chini ya umri wa miaka 16

E] Sheria vilevile inamruhusu mmiliki wa leseni ya vileo kumzuia mtu ambaye amevaa mavazi yasio ya staha asiingie katika eneon lake la biashara.Hii inajumuisha wanawake na wanaumme la msingi tu ni kwamba wawe wamevaa mavazi yasiyo ya staha

Kumekuwa na malalamiko kwamba baadhi ya watanzania hasa wa jinsia ya kike wamekuwa wakizuiwa kuingia kwenye mahoteli ya kitalii, inawezekana mojawapo ya sababu ni hii ingawaji si wote wanaozuiwa huwa wanakuwa wamevaa mavazi yasiyo na staha

F]Sheria vilevile inampa mamlaka mmiliki wa leseni ya vileo kumzuia mtu yeyote asiingie katika eneo lake kama anaamini kwamba mtu huyo ana nia ya kulitumia eneo lake kwa ajili ya kukutana na watu ili ya kupanga mambo ambayo yatasababisha au yanaweza kusababisha hatari kwa usalama,amani na utangamano katika jamhuri ya muungano.

Kifungu cha 75.cha sheria hii kinamtaka Mtu aliyepewa lesseni,muwakilishi wake,au mfanyakazi wake anaweza kukataa kumhudumia au kumruhusu aingie katika eneo lililopewa leseni ya vileo na vile vile ana uwezo wa kumuondoa kutoka eneo lililopewa leseni,kwa kutumia nguvu kadri inavyopasa mtu yeyote ambaye ni mlevi(drunken) au mwenye vurugu au anayeleta vurugu

au ambaye haruhusiwi kuuziwa pombe au ambaye amevaa mavazi yasiyo ya staha au ambaye mtu aliyepewa leseni anaamini kwamba mtu huyo anatumia au anaweza akatumia eneo lake lililopewa leseni kama eneo la kukutania na mtu au watu wengine kwa ajili ya mambo ambayo yatasababisha au yanaweza kusababisha hatari kwa usalama ,amani na utangamano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kama mtu huyo baada ya kuombwa na mtu mwenye leseni ya vileo au mtu yeyote anayefanya kazi chini ya mtu mwenye leseni ya vileo au Afisa wa polisi,atakataa,au atashindwa kuondoka katika eneo hilo linalouzwa vileo atakuwa ametenda kosa la jinai na akipatikana na hatia atalipa faini ya shilingi mia tano na itakuwa kazi ya Afisa wa Polisi kwa maombi ya mwenye leseni ya kuuza vileo au mfanyakazi wake,kumuondoa au kusaidia katika kumuondoa mtu huuyo kutoka katika eneo husika kwa kutumia nguvu ya kadri.

12. KUMEKUWA NA TABIA YA BAADHI YA MAENEO YA VILEO KUTUMIKA KAMA MADANGURO, SHERIA INASEMAJE KUHUSU HILO?
Tanzania ni nchi ambayo ina maadili yake ambayo yanalindwa na sheria.Mojawapo ya maadili hayo ni yale yanayokataza ufanyaji wa biashara ya ukahaba.Hivyo basi mtu yeyote atakayetoa mazingira Fulani ili kuwezesha biashara hiyo ifanyike anakuwa ametenda kosa kisheria.

[Ss 76] Mtu yeyote aliyepewa leseni ya kuuza vileo endapo ataruhusu eneo lake litumike kama danguro au eneo la kukutana mara kwa mara au kutembelewa mara kwa mara na watu wenye sifa/wanaodhaniwa za umalaya atakuwa ametenda kosa la jinai na kama mtu aliyepewa leseni atapatikana na hatia Mahakama inaweza kuamuru leseni yake anyang’anywe.Hapa Dar es Salaam na hata mikoani kuna maeneo yaliyopewa leseni ya kuuza vileo ambayo yanafahamika wazi kwamba ndio makutano makuu ya makahaba.Wenye mabaa wanajua hilo, vyombo vya serikali vinajua hilo hasa serikali za mitaa lakini hakuna hatua zinazochukuliwa na inasubiriwa mpaka kiongozi wa juu aseme.

Wananchi wasiogope kwenda kwenye ofisi za serikali za mitaa kulalamika kwa kuwa hizo ni ofisi zao, ni ofisi za umma na wana kila haki ya kwenda pale na kusikilizwa.Na ikishindikana wasisite kwenda ngazi za juu.Au hata kuripoti ktuo cha polisi kwa kuwa hilo ni kosa la jinai na mahakama inaweza kumfutia leseni au na pia kumpa adhabu nyingine.

Wasikubali kuona watoto wao wakiharibikiwa maadili kwa kuona mambo machafu has yanayohusiana na biashara ya ukahaba.

13. SHERIA INASEMAJE KUHUSU KUUZIA VILEO MAAFISA WA POLISI
Mtu yeyote aliyepewa leseni ya vileo haruhusiwi isipokuwa tu kwa mamlaka ya ya askari wa polisi mwenye cheo cha Assistant superintended wa polisi au mtu mwenye cheo cha juu kuzidi hapo

Atamruhusu askari yeyote wa polisi ambaye cheo chake ni chini ya Assistany superintended akiwa katika shughuli za kazi kuingia au kubaki katika eneo lake la kuuzia vileo isipokuwa kwa lengo la kutunza amani au kutimiza majukumu ya kazi zake

-Atamuuzia vileo au viburudisho askari huyo

Mtu yeyote mwenye leseni akikiuka masharti ya kifungu hiki atakuwa anavunja sheria na atapigwa faini ya shillingi mia tano.

14. JE, VYOMBO VYA DOLA VINA MAMLAKA YAPI YA KUDHIBITI WATU WANAOVUNJA SHERIA HI

Hii inaweza kufanywa na

-polisi yoyote

-Ofisa wa Afya

-Mkaguzi wa afya

-Afisa tawala

-au afisa wa serikali ya mtaa aliyeruhusiwa A] MAMLAKA YA KUINGIA NA KUFANYA UKAGUZI

Hawa wote wanaweza kuingia na kufanya ukaguzi muda wowote kukagua eneo linalohusika na vileo kwa ajili ya kuzuia uhalifu au kupeleleza uhalifu au kuangalia hali ya afya na matengenezo ya sehemu zilizoharibika na uendeshaji wa biashara kwa ujumla na wana uwezo wa kuomba leseni kwa ili waione.

-Mtu yeyote atakayewazuia kufanya hayo hapo juu atakuwa ametenda kosa la jinai

Hivyo basi,kwa kuwa watu hawa wamepewa jukumu na Katiba pamoja na Sheria,na wajibu huo wameachiwa waushughulikie.Hawatarajiwi kuacha sheria ivunjwe bila kuchukua hatua,vinginevyo uongozi wa Umma utakuwa umewashinda na ikibidi wafanye shughuli nyingine tu.Kiongozi aliyepewa sheria aisimamie,sheria hiyo aliyopewa aisimamie inavunjwa mbele ya macho yake tena kila siku,basi ameshindwa kusimamia sheria hiyo na kwa kuwa kazi yake ni kuisimamia sheria hiyo,basi na kazi imemshinda.

Hatutarajii mpaka mkuu wa Mkoa au Waziri,japo wana mamlaka hayo,ndio waje wazuie suala hili wakati kuna watu kama Maafisa wa serikali ya Mtaa tunaoishi nao wanashindwa kuchukua hatua,kuna askari polisi hadi wale wa patrol,kuna maofisa afya kila kona.Hawa wanaonyesha udhaifu katika uongozi wao na wanachangia serikali kuu ionekane ina udhaifu.

b] MAMLAKA YA KUFUNGA ENEO LA KUUZIA VILEO ENDAPO KUTATOKEA VURUGU

-Afisa tawala yeyote au

-Afisa wa PolisiMahala popote ambapo panatokea vurugu au vurugu inatarajia kutokea anaweza kuamuru kwamba maeneo la kuuzia vileo yafungwe yote au sehemu tu tu ya maeneo ya kuuzia vileo hapo au mhala karibu na hapo yafungwe kwa muda ambao utajionyesha katika amri hiyo

Lakini sheria hii katika fungu hilo hilo hairuhusu kufunga eneo lolote la biashara kwa zaidi ya siku thelathini bila idhini ya Waziri.

C] MAMLAKA YA KUNYANG’ANYA LESENI
Mahakama kama itajiridhisha kwamba mtu aliyepewa leseni ameshapatikana na hatia mahakamani mara mbili au zaidi kwa kosa lile lile inaweza kuamuru anyan’ganywe leseni

-Kama mtu aliyepewa leseni chini ya sheria hii au sheria nyingine yoyote amefungwa jela bila kupewa mbadala wa faini kwa kipindi kinachozidi siku 14, mahakama ina uwezo wa kuamuru leseni yake anyang’anywe.

D] MAMLAKA YA KUNYAN’GANYA VILEO

Baada ya kumsikiliza muhusika mhakama ina uwezo wa kuamuru vileo hivyo vitaifishwe

15. JE MTU ANAYEMZUIA MTEJA KUINGIA KATIKA ENEO ANALOFANYA BIASHARA YA VILEO MTU ALIYEVAA MAVAZI YASIYO NA STAHA ANAKUWA AMEVUNJA KATIBA NA KUFANYA UBAGUZI

Suala hili limekuwa likizua malumbano katika jamii na kumekuwa na hoja kwamba watu wa nchi za magharibi wamekuwa wakiruhusiwa kiungia katika baadhi ya maeneo,kwa mfano hoteli kubwa za kitalii wakati wale wenye asili ya kiafrika wamekuwa wakizuiwa na walinzi magetini kwa kuelezwa kwamba hawaruhusiwi.Hii huleta malalamiko ya Ubaguzi wa rangi.Sheria hii ya vileo inasemaje kuhusu hilo.

Sheria hii katika fungu la 75 inampa nguvu mmiliki wa leseni ya kuuza vileo kumzuia mtu yeyote aliyevaa mavazi yasiyo ya Staha kuingia katika eneo lake la kuuzia vileo,au kukataa kumhudumia au hata kumuondoa katika eneo hilo.Nasisitiza tena kwamba ni mtu yoyote.

Ibara ya 13[2] ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema kwamba ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake.

Sasa suala linalofuata ni je Katiba inasemaje? Ibara hiyo hiyo imefafanua ubaguzi kwa kusema kwamba

13[5]”kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara hii,neno “kubagua” maana yake ni kutimiza haja,haki au mahitaji mengineyo kwa watu mbalimbali kwa kuzingatia utaifa wao,kabila,pahala walipotokea,maoni yao kisiasa,rangi,dini,au hali yao ya maisha kwa namna ambayo watu wa aina Fulani wanafanywa au kuhesabiwa kuwa dhaifu au duni na kuwekewa vikwazo au masharti ya vipingamizi ambapo watu wa aina nyingine wanatendewa tofauti au wanapewa fursa au faida iliyoko nje ya masharti au sifa za lazima.

-Sheria hii haina ubaguzi kwa kuwa inasema kwamba mtu yeyote ambaye amevaa mavazi yasiyo na staha bila kujali utaifa wao,kabila,pahala walipotokea,maoni yao kisiasa,rangi,dini,au hali yao kimaisha wanaweza kuzuiwa kuingia,kukataliwa huduma.Hivyo basi awe mzungu,mwarabu,mwafrika,mchina.

-Je wanaowazuia watu wenye asili ya kiafrika wanakuwa wamefanya kosa

Wanakuwa wamefanya kosa pale tu wanapowazuia bila kuzingatia sheria hii.Kama wamevaa mavazi ya Staha na sio Malaya au watu wa vurugu wanatakiwa waruhusiwe na kuwazuia ni kufanya kosa la ubaguzi ambalo wanaotendewa wanashauriwa wafungue mashtaka mahakamani ili wajipatie fidia.

-Lakini kuna tatizo ambalo linaletwa na hawa wanaofanya biashara ya ukahaba ambao nao sheria hii [Ss 76] Inambana mtu anayemiliki leseni ya kuuza vileo asiwaruhusu wakae katika eneo lake.Hawa nao wanaweza kuja na mavazi ya staha lakini wakawa wamekuja kufanya biashara ya kuuza miili.Hivyo basi ni jukumu la mwenye kumiliki leseni, endapo anamtilia mashaka muhusika, amuuliza kwanza.
 
Asante kwa elimu.NAomba kufahamu sheria inasemaje kuhusu mtu anayezidisha muda wa kunywa yani anakunywa hadi aleajiri adhabu ipoje kwa mtu huyu?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom