UmkhontoweSizwe
Platinum Member
- Dec 19, 2008
- 8,543
- 7,755
Ndugu zangu watanzania wenzangu,
Ninajua tunapitia kwenye kipindi kigumu sasa tunapojadili juu ya huu mkataba unaolenga kuuza bandari zetu na kuturejesha utumwani kwa waarabu.
Ninachojiuliza mpaka sasa ni wapi alipo Jakaya Mrisho Kikwete? Kuna mtu amesikia kauli yoyote toka kwake?
Mimi binafsi sijasikia akisema chochote juu ya sakata hili. Ina maana yeye halimgusi, au halimhusu?
Jakaya Mrisho Kikwete ndiye taswira au kioo cha ccm kwa sasa. Yeye anasimama kwenye nafasi ya Baba wa taifa mwl Nyerere, na pia mwanamapinduzi John Pombe Magufuli; anayo nafasi kubwa ya kuonyesha njia kwetu kama taifa kujua kule tunakoelekea.
Swali langu: Je, kuna mtu amesikia sauti ya JK juu ya hili? Amesimama upande gani?
Je, anasubiri tuuzwe kwanza kwa waarabu ndipo ajitokeze?
Napenda nimpe taarifa: asiposimama sasa kukemea na kuitetea nchi yake (Tanganyika/Tanzania), damu ya watanzania itadaiwa mikononi mwake na uzao wake daima milele.
Aliyesikia kauli ya kikwete atujuze.