Jakaya Mrisho Kikwete ateka maonesho ya Sabasaba. Wananchi Wamuombea Maisha marefu

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,279
9,719
Ndugu zangu watanzania,

Rais mstaafu wa awamu ya Nne mh Jakaya Mrisho Kikwete amedhihirisha kuwa alikuwa Ni chaguo la Mungu kuliongoza Taifa Hili katika awamu ya Nne,Amedhihirisha ya kuwa Ni kipenzi Cha watanzania,Ni faraja ya Taifa ,Ni Dhahabu itembeayo,Ni chemchemi jangwani na Ni Nuru Gizani. Nimewahi kuwaambieni humu kuwa ni yeye aliyenishawishi kujiunga na kuipenda CCM Tangia mwaka 2005 nilipokuwa katika mkoa wa Rukwa wilaya ya sumbawanga vijijini mji mdogo wa laela alipokuja katika kampeni za kuomba ridhaa ya Urais wa Taifa letu.

Kiongozi huyu mashuhuri na maarufu kabisa Barani Afrika,kiongozi wa kwanza wa kiafrika kutinga ikulu ya white house nchini marekani kuonana na kufanya mazungumzo na mstaafu Barack Obama,kiongozi anayependwa na mamillion ya watanzania wa Rika na makundi yote,kiongozi asiye na makuu ,kiongozi aliyeimarisha demokrasia ya kupigiwa mfano katika Taifa letu, kiongozi aliyekuza uchumi wa Taifa letu,kiongozi aliye fanya vijana wengi nikiwepo Mimi kutoka familia maskini kupata Elimu mpaka chuo kikuu bila shida,kiongozi mwenye moyo wa upendo, huruma,hekima na busara ya Hali ya juu Sana anaendelea kuishi katika mioyo ya mamilioni ya watanzania.

Rais Kikwete anaendelea kutazamwa na watanzania kama akina George Washington na John Adams kutoka nchini marekani,Rais huyu ambaye hata watoto wake Ni wenye heshima na unyenyekevu wa Hali ya juu Sana, ndio maana huwezi ukasikia mh Ridhiwan Kikwete akiropoka au kutoa lugha zisizo na staha kwa watanzania. Kikwete Jakaya Mrisho anapendwa Sana na watanzania ndio maana asipoonekana hadharani watanzania wanamuuliza Sana na kuwa na shauku ya kutaka kujuwa aliko.

Mzee Jakaya Kikwete ameonyesha namna watanzania walivyo guswa na uongozi wake katika awamu yake,kwa kuwa Ni katika awamu yake tulishuhudia mambo makubwa ya kimaendeleo yakifanyika nchini,Ni wakati huo shule nyingi za sekondari zilijengwa,hospitali nyingi kuanzia zahanati,vituo vya Afya mpaka hospitali za Kanda zilijengwa na kuboreshwa,Ni wakati huo ajira zilimwagwa mitaani kwa vijana bila kikomo,Ni wakati huo biashara nyingi zilifunguliwa nchini,Ni wakati huo vijana walipewa nafasi za kiuongozi ndani ya chama na serikali ili wajiandae kuwapokea wazee watakapo kuwa wanastaafu .

Ni wakati huo vyuo vikuu vingi vilijengwa na kudahili wanafunzi na Serikali kuwapatia mikopo wanafunzi wote wenye sifa,Ni wakati huo watumishi wa umma walipandishiwa mishahara Yao ,Ni wakati wake Taifa letu lilipokea wageni wote na viongozi wakubwa kutoka Mataifa yote makubwa ,Ni wakati huo wa mh Kikwete Taifa letu liliheshimika kimataifa ,Ni wakati huo kwa ushawishi wa Rais Kikwete tulitoa Naibu katibu mkuu wa umoja wa mataifa mh Dr asha Rose migiro na Ni wakati huo wengi tuliona nyota ya mama yetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani iking'ara kiutendaji,Ni wakati huo ambapo watu walikuwa huru kuzungumza bila hofu Wala wasiwasi,Ni wakati huo watu na waandishi wa habari waliandika Sana magazeti kwa Uhuru kabisa na ni wakati huo niliipenda Sana siasa na kushiriki sana mijadala ya kisiasa mitaani.

Rais Kikwete Anaishi na anaendelea kuwa katika mioyo ya watanzania , anaendelea kuwa kivutio popote awapo, anaendelea kuwa mwanasiasa wa kupigiwa mfano hapa nchini, anaendelea kutazamwa kwa namna ya kipekee kabisa na watanzania.

Hongera Sana mh Jakaya Mrisho Kikwete Rais wetu mstaafu,binafsi nakushukuru Sana kwa uongozi wako uliotukuka kwa Taifa letu,wengine pasipo wewe tusingefika na kutimiza Ndoto zetu za kielimu,uligusa maisha ya wengi ndio sababu unaendelea kupendwa Sana na watanzania ndio maana unaendelea kuheshimika Sana ndani na nje ya Taifa letu,ndio maana unaendelea kuulizwa Sana usipoonekana hadharani,ndio maana unaendelea kuwa shujaa wa Taifa letu katika secta ya umma na binafsi.

Wewe ni kiongozi wa kweli na uliye kuwa chaguo la Mungu ,wewe Ni kiongozi uliyefanikiwa kutengeneza viongozi mbalimbali hapa nchini. Ni kupitia mikono yako mzee wetu wengi wamefika na kushika nafasi za juu kiuongozi, Ni wewe uliwapa nafasi ya kukua na kuonyesha uwezo wao pasipo kuwazuia Wala kuwashika miguu,Ni wewe mzee wetu uliye wapa njia ya kupita viongozi wetu mbalimbali waliopo Sasa na waliotangulia mbele za haki wakaweza kuonyesha vipawa vyao vya uongozi,wewe Ni kiongozi uliyekamilika kwa kuwa umetuachia viongozi mahiri na wazalendo kwa Taifa letu.

Asante Sana mh Jakaya Mrisho Kikwete Rais wetu mstaafu kwa utumishi wako kwa Taifa letu,Asante kwa moyo wako mkubwa wa uvumilivu na subira hata pale utupiwapo mawe, siku zote hujarudisha mawe Bali umeyaokota na kujengea msingi imara kwa Taifa letu na ustawi wa watanzania. Mwenyezi Mungu akujalie maisha marefu yenye heri na Baraka. Asante

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Namna Gani hujui chochote
George bush ndo aliaza nae ,na siku alipofika ikulu hiyo ,wasaidizi wa bush wakamwambia bush kunamgeni hapa ,akawaukiza nani ,wakajibu kikwe...
Uwe unasoma kwa kutulia,Sasa George Bush Tangia lini amekuwa ni kiongozi wa nchi yoyote ya Afrika? Mimi nimesema kiongozi wa kwanza kutoka Bara la Afrika halafu wewe unaanza kuleta habari za Bush. Au umelewa Pombe ndugu yangu
 
Unatumia muda mwingi kutetea CCM chama Cha wezi wa rasilimali za nchi
CCM ni chama safi na makini. Ni chama chenye Sera na ajenda zinazogusa maisha ya watanzania na kilichodhamiria kuleta matumaini katika maisha ya watanzania.
 
Ndio maana unaweka namba za simu kila post. Jenga hoja chief, cement bei kali sina time ya kupoteza kubishana na wewe.
Fanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa uone Kama hutapata hela ya cement. Acha kupiga mdomo tu wakati wote,fanya kazi ilimradi Ni halali na inakubalika katika jamii pasipo kuchagua kazi ,.
 
Fanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa uone Kama hutapata hela ya cement. Acha kupiga mdomo tu wakati wote,fanya kazi ilimradi Ni halali na inakubalika katika jamii pasipo kuchagua kazi ,.
Hahahaha endelea kuwa chawa kiraka, wenzako wala wewe waliwa. Bye.
 
Unaandika kama umekatika kichwa vile, toka uhuru watu wale wale na bado tunajenga matundu ya vyoo kwa misaada.. F#@ u
Tulipokuwa tuna pata Uhuru tulikuwa watu million 12 na Sasa Tupo watu million 61,Sasa kwa akili yako unataka matundu ya choo yasiongezeke wakati hata kwenye familia yako tu mmeongezeka?
 
Back
Top Bottom