Kuunganisha Nguvu kwa wenye matching aidea

Poa tunasubiri taarifa mkuu Malila,Vp kagari kadogo kama starlet kanaweza kufika huko? au unahitaji 4wheel? zote ni gari ndogo
 
Hiyo ni SACCOS na si Benki make mtaji wa kuanzisha Benk kwa sasa ni More than one Bilioni kwa mujibu wa BOT, na kuna SACCOS zinamitaji ya kuwa Benki lakini still ni SACCOS,
Na hao 50 wote ni share holders. make kama ni share holders basi wanaelekea kwenye PUBLIC COMPANY, ila ni kazi nzuri

Mkuu utaratibu wa kuanzisha Community Bank hauna vigezo hivyo. I bet hao jamaa wanaozungumziwa na MamaEE wanataka kuanzisha community bank
 
Mkuu logistic ziko vipi kwa yule mwenye interest?

Hili pande ni mali ya kijiji, ukilitaka ni suala la kuamua ili nikupeleke ukalione na kulifanyia uchunguzi, nimejikatia kipande changu tayari. Kijiji si warasimu hata chembe, panafaa kwa ufugaji zaidi na kilimo cha tikiti. Usafiri wa kufika huko ni daladala tokea Mbagala au binafsi. Bei ni Tsh 300,000/ kwa eka, pungufu unaongea.
 
Asante kwa info Malila ila sijakuelewa ukisema mabasi unapandia mbagala, Kidugalo iko wapi sio umesema Chalinze, hebu naomba be specific, wilaya na mkoa. Naona mwingine yuko interested hapa basi tutajipanga tukaone uko na kufikia bei....
 
what a thread, Komado, MamaEE, LAT keep on feeding us!

Unajua hata wamachinga, ukakuta kuna mabanda 15 kila mmoja ana uza nguo za kike ya yamefuatana, au mabegi, au wanatembeza mtaani. wangefungua duka moja la vikorombwezo vyote wanavyouza kwenye maduka yao, wanalipa kodi ya pango moja, wanaajiri watumishi 3 au 4, wanalipa kodi ya TRA moja, wanatumia leseni moja, wanatumia TIN moja.... na wanagawana faida kwa kulingana na kiasi cha mtaji ulichowekeza.. and of couse return ni kubwa kutokana na kununua in bulk and minimal operational costs

watembeza bidhaa mtaani... watu 10 tu wanweza kufungua duka na wakafanya kazi kwa kurelax zaidi ya stress walizonazo na kwa kuwa wataajiri mtumishi watapata muda wa ziada wa kufanya shughuli nyingine za kuwaingizia kipato na kuongezeka

Tatizo in wrong intuitions tulizo nazo waTZ zinatutesa... wazo la kuanzisha JE lilivyoletwa ndo nilijua Wtz tuna shida kubwa.. watu walikuwa sooo negative na sasa je!??? hahaha ngoja ncheke mie niongeze maisha! huu ni mfano mdogo tuu wa mambo kuwa yanawezekana, Changamoto za uaminifu ndo kazi za kufanya.... we work on challenges! hakuna chanamoto hakuna kazi za kufanya... so kama unaogopa changamoto unaogopa kazi, na kama unaogopa kazi wewe ni masikini wa mwili wako mwenyewe
 
Asante kwa info Malila ila sijakuelewa ukisema mabasi unapandia mbagala, Kidugalo iko wapi sio umesema Chalinze, hebu naomba be specific, wilaya na mkoa. Naona mwingine yuko interested hapa basi tutajipanga tukaone uko na kufikia bei....

Issue hapa zinaongelewa kwa wingi,
Kama unataka kwenda kwenye pande lenye maji, huko ni Mkuranga kijiji cha Msorwa/Shungubweni ndio usafiri uko pale Mbagala. Kama unataka kwenda Kidugalo usafiri uko UBT au pale Mlandizi stand ya kwenda Mzenga. Gari dogo kama Starlet kwa sasa linafika bila shida kwa sababu barabara ni nzuri sana. Kidugalo ni wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani

Njia rahisi ywa kwenda Kidugalo ni kupanda basi pale Buguruni,lakini mabasi ya pale yamechoka sana,halafu yanabeba mizigo ya wakulima mingi sana, unafika uko hoi kwa vumbi na kajasho.
 
MKUU umeongea ukweli mtupu mi naamini kabisa mkikutana watu wenye ideas zinazofanana mkaunganisha nguvu kifedha na kimawazo umaskini utbaji kua historia...tukiendelea kuogopana sababu ya uaminifu mdogo tutaendelea kusubiri mpaka yesu anarudi,tatizo letu ni ubinafsi na kutaka sifa.za kijinga ili uonekane unakomaa kivyako wakati ukweli ni kua unajiumiza unakuta unatumia nguvu nyingi kwa muda mrefu kustruggle mwisho wa siku unajikita unarudi nyuma badala ya kusonga mbele....UMOJA NI NGUVU cha msingi ni makubaliano yenye nia moja ya kutaka kufanikisha malengo mliyo jiwekea.
 
Watu tunakufa maskini hivi hivi kwa ubinafsi wetu na uwoga wa kutoaminiana na kuthubutu,kama kweli mnajiorganize watu wawili watatu au wanne mnadevelop ideas zenu na mtaji lazma mtatoboa tu cha msingi ni kujiwekea terms and conditions....
 
Dah mkui hii thread nisha isahau kabisa, shukurani kwa kuileta, ni kweli mkuu kuunganisha nguvu kwa huku ni ishu ngumu sana na kila mtu anaona afe kivyake.
 
Back
Top Bottom