Watanzania huungana na kushirikiana kwa dhati kwenye kumpiga mwizi tu ila sio kwenye biashara.

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,228
22,306
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza ni ukweli usiofichika kwamba hapa nchini Tanzania ni ngumu sana biashara iliyofunguliwa kwa ushirikiano wa kuanzia watu wawili ni ngumu sana kudumu. Ukimtoa kumpiga mwizi huwa tuna umoja wa dhati kwenye kushabikia Simba/Yanga. Kwenye ushabiki wa hizi timu unakuta Profesa na darasa la 7 wanaongea lugha moja.

Biashara za kuundwa kwa kuunganisha mitaji huwa zinakuwa na nguvu ya ajabu zikisimamiwa vizuri sasa tatizo ni kina watanzania gani wanaweza unganisha mitaji yao wakadumu kwenye biashara angalau kwa miaka 10? Tukiachilia mbali biashara zetu hizi ndogondogo tumeona hata makampuni makubwa yaliyotajwa kushirikisha watu wengi yalikufa huku sababu zikiwa hazieleweki. Kampuni ya mabasi SCANDNAVIA NI MFANO HAI.

Huku mitaani pia kumekuwa na ugomvi kila sehemu watu wakituhumiana mambo mbalimbali baada ya kufungua biashara ya pamoja. Vikundi vya kukopeshana sitaviongelea kwa leo. Biashara zinazodumu angalau ni zile ambazo zina shareholder mmoja mwenye nguvu sana kuzidi wengine. Lakini shareholders wakilingana tayari ni tatizo.

Nini kifanyike ili tuwe kama waasia au wasomali ili tuwe imara kibiashara?
 
Na kupeana ushirikiano kwenye mada zinazohusu kula tunda kimasihara au chimbo la misambwanda,lakini mada yenye funzo kama hii wala hutowaona utafikiri hawaoni
 
Back
Top Bottom