KwetuKwanza
Member
- Mar 13, 2023
- 34
- 82
Mbunge huyo amefunga TV hizi na Vingamuzi hivi kila eneo ambalo lina mkusanyiko wa watu kwenye Jimbo lake, na taarifa nilizopewa na wenyeji ni kuwa Mbunge huyu kila mwezi analipia vifurushi pamoja na umeme.
Kila eneo Amfunga Scree yenye ukubwa wa Nch. 70 kama sikosei, (Sina uhakika sana kweye hili, lkn niliona eneo Moja pale Kemondo ni screen kubwa kweli.
Watu wamekuwa wakikusanyika kwenye Tv hizo kuangalia michezo mbalimbali hasa ya mpira, Ligi kuu na Ligi za Ulaya, lkn pia hata taarifa za Habari na wanaangalia bure maana zimewekwa katika eneo la wazi.
Kwa siku ambazo zimefanikiwa kukaa Bukoba na kushuhudia huduma hii, watu wamekuwa wakijitokeza kwa kiasi Fulani kuangalia, hasa wakati wa mpira wengi ukusanyika na kuangalia.
Nilijiuliza Maswali kadhaa, Je hili lilikuwa hitaji la wananchi wa jimbo lake?? Je ni Moja ya ilani kwenye Chama chake??? Huyu Mbunge aliwaza Nini??? Ilikuwa Moja ya ahadi yake wakati wa Kampeini??? Wananchi walimuomba??? Aliona wananchi wa Bukoba au kwenye jimbo lake hawana TV majumbani kwao??? Nini alikilenga.
Baadhi ya wananchi ambao niliongea nao, wanasema hawakuwahi kumuomba huduma hiyo kwenye maeneo yao, na wala siyo hitaji lao kwenye maeneo yao, lakini wanasema aliamua yeye mwenyewe na wasema tv hizo zilifungwa kwa sherehe kubwa.
Wengine wanasema ni kama wamedharauliwa sana na Mbunge huyo, " Ametuona sisi kama maskini sana, yaani hatuna tv majumbani kwetu, hatujawahi kuomba hii huduma, hatujui alituwazia nini, ni kama alitudharau watu wa Bukoba.
Nilienda mbali zaidi kuangalia hali ya huduma za kijamii kwenye hayo maeneo ambako amefunga tv hizo na maeneo mengine ambayo hajafunga.
Ni Kama inachekesha lakini inaumiza, unawaza huyu Mbunge aliwaza hitaji la wananchi wake, au anatafuta Nini? Mbunge kabisa unaona eneo Fulani hakuna Barabara, na kazi ipo haipitiki, hakuna zahanati, hakuna maji, akina mama hawana mitaji, vijana hawana mitaji, alafu unakwenda kufunga tv.
Maeneo ambayo amefunga huduma hizo, hakuna huduma Muhimu za kijamii, utakuta sehemu nyingine Barabara hazipitiki, hawana maji, hawana huduma ya Afya, hawana huduma za mawasiliano, wanawake wanalia kupata mitaji na vijana pia.
"Ukiamgalia pesa alizotumia kufunga hizi huduma na anazotumia kulipia umeme na vifurushi, angeliweza kabisa kutupatia mikopo sisi wanawake tukaendeleza biashara zetu hizi ndogo, sisi wanawake tunaangaika sana kupata mitaji, Leo Mbunge unasikia kafunga tv na analipa vifurushi kila mwezi na umeme.
Nilichogundua huyu Mbunge hakuwaza kabisa Maendeleo ya watu, bali aliwaza yeye mwenyewe maisha yake, na inawezekana baadaye akaja kuomba kura kupitia huduma hii.
Unaweza vipi tv, kulipa Vingamuzi kila mwezi na umeme, wakati mama mjamzito anatembea kilometa 20, kufuata huduma ya Afya, mtoto anatembea kilometa 20 kufuata Shule, Vijana, wanawake wako mtaani hawana mitaji????
Nimeweka hapa hii Hoja, Je huyu Mbunge aliwaza Nini kuweka hii huduma kwa wananchi wake?????????