Biashara inataka moyo sana

Mukuu123

JF-Expert Member
May 7, 2019
319
1,221
Mimi ni graduate nilipata kazi nikafanya kwa muda wa miaka kama saba hivi kupata mtaji then nikaamua kuanzisha biashara,unajua biashara kuanzisha si kazi ukiwa na mtaji,kazi ngumu kwenye biashara ni kuifanya iendelee kuwepo.

Sasa wakati biashara inaanza mara nyingi inaanza vizuri but ukifika muda unakuta mambo hayaendi kabisa number ya wateja wako basic unakuta ghafla hawapo na hakuna wateja wapya wanaoingia dukani kwako aisee hii kitu usiombe unafanya kila kitu unachoweza kufanya kwa usahihi alafu matokeo hupati apa ndio nikajua kwa nini watu wanaenda kwa waganga.

Mashekhe au kwa wachungaji ili kuweza kupata msaada, kuna kipindi biashara inakua ngumu mpaka unaona bora urudi kwenye mshahara wa laki tano kwa mwezi big up sana kwa wafanya biashara walioweza kukuza mitaji hii kitu siyo rahisi mazee
 
Yote kwa yote usiombe hali hii ikukute ikiwa uliianzisha kwa kukopa hivyo una marejesho kila mwezi..
Unageuka tena hio hio ndio ya kulisha familia, hio hio kodi ya fremu na Pango..

Lazima upate moto, mteja akija asiponunua unaweza umkunje shati humo humo dukani.
 
Na kitu kingine watu wengi biashara tunaanzisha Kwa mawazo yetu kichwani sasa na hii mitaji midogo downfall zikitokea biashara inakua kwenye risk ya kufilisika lakini ukiwa na familia ya watu wafanya biashara ni ngumu kupitia kwenye mashimo sababu waliotangulia washajua michoro yote ya biashara na kuipata faida
 
Sio rafiki kivipi Mbona baadhi ya wafanyabiashara wanapiga pesa ndefu,kupitia biashara hizohizo?
Tulia wewe ,hujui kitu
We unaona hizo biashara zimesimama unadhani hizo biashara ndio zinagenerate faida si ndio ?
Watu wanafanya mambo yao meusi pembeni hizo biashara ni changa la macho tu
Watu wanafanya utakatishaji pesa , ukwepaji kodi , Rushwa , kuuza bidhaa feki , kupunja na kufanya Magumashi kibao
Mfumo wa nchi hii ni wa ovyo mno
Hairuhusu private sector na ujasiriamali kuthrive ,kama unaona hizi ni stories anzisha biashara halafu ulete mrejesho hapa
 
Mziki wa biashara uingie mwenyewe uuone ndio utajua ya kwamba hawa waliofanikiwa kwenye biashara walitumia njia gani it’s not easy possibility ya kuanguka kwenye biashara ni kubwa mnoo kuliko kufanikiwa,mimi na MBA but nahisi ni mweupe kabisa kwenye biashara za uku mtaani
 
Back
Top Bottom