Kuunda Mkoa wa Chato ni kupoteza historia ya Wahaya, Mkoa wa Chato hauna maslahi kwa urithi wa utamaduni wa Mtanzania

Mikoa haiundwi kuhifadhi mipaka ya kikabila bali kusogeza huduma kwa watu. Kupasuliwa Kagera kwenda mkoa mwingine hakumfanyi Muhaya kuwa Mbondei..atabaki na uhaya wake.
Mikoa mwanzoni iliundwa kwa kufuata mila na desturi za makabila yanayoshea mambo.acha ubishi,
 
Unaweza kukarabati shule bila kutukana watu au kula rambirambi

By the way kukarabati shule ni jukumu la serikali siyo hisani, maana serikali inakusanaya kodi hata kutoka mkoani Kagera pia
Ndio mtindo wake wa maongezi hakuwa malaika. Kila rais anao upande mwema na mbaya, na ndio ukamilifu wa binadamu ulivyo.
 
One of the stupidest move if it will materialize.
Hoja ya mkoa wa chato ilikuwa na element zote za ubinafsi zilizolenga kutawala milele..
 
Ila Magufuli alikua na roho ya ajabu sana,sishangai moyo wake kuwekewa umeme..."TOO SELFISH" ukifatilia historia ya kuanzishwa kwa wilaya ya Chato ni scenerio ile ile,alitumia ubabe na roho mbaya kulazimisha makao makuu yajengwe kwao.
Mikoa ya Katavi na Manyara ilianzaje? Wilaya za Mlele na Chalinze zilianzaje? Unajua Uwanja wa Ndege wa Songwe Mbeya ulijengwa kwa shinikizo la nani? Au mnnafikiri ninyi ndio mnajua sana kuliko wengine?
 
Labda kama kusaka 10% lkn hakuna tija kuunzisha mkoa hali nchi Ina shida nyingi kubwa,je kagera ni kubwa kuliko tabora,lindi, morogoro?.Hizo pesa za kuchezea kwann zisiende maliza tatizo la foleni tunduma kwa kuboresha miundo mbinu.Gari zinafunga foleni zaidi ya kilometa 20 ndipo ziweze kuvuka boda,
 
Kuhamia dodoma, kujenga ikulu mpya, kujenga Chato airport, kuanzisha mkoa mpya wa Chato ni matumizi mabaya Sana ya Kodi zetu havina tija kiuchumi labda tu kama matatizo yetu yangekuwa yamekwisha
 
Mikoa ya Katavi na Manyara ilianzaje? Wilaya za Mlele na Chalinze zilianzaje? Unajua Uwanja wa Ndege wa Songwe Mbeya ulijengwa kwa shinikizo la nani? Au mnnafikiri ninyi ndio mnajua sana kuliko wengine?
Mbeya ni lzm uwepo uwanja kiuchumi ni sahihi
 
Magufuli alitaka kuunda mkoa nyumbani kwake kwa utashi tu binafsi bila kujali vigezo vyenye mantiki vya kuunda mkoa huo.

Yaani katika muendelezo wake wa "unyumbani" akavunja protokali zote za kimantiki na kivigezo katika kuubda mkoa mpya.

Leo hii mkoa wa Geita ni miongoni mwa mikoa michanga kabisa ambayo haina umri hata wa miaka 20, lakini cha ajabu yanaletwa mapendekezo ya kukata eneo kutoka mkoa huo kwenda kuunda mkoa mwingine—Ili iweje?

Lakini kibaya zaidi, Leo tunakwenda kukata eneo la mkoa ambao by all standards ni mkoa kongwe, wenye historia ndefu, Mkoa wa Kagera, uliobeba historia ya nchi hii kwa utamaduni wake mzuri, historia ya falme zake, lugha yake n. k tunakwenda kumegua eneo katika huo mkoa na kuunda mwingine tu ili kumpa mwendazake hitajio la moyo wake, bila kuangalia cultural-social dynamics za watu.

Tunajua Magufuli hakuwahi kuwapenda Wahaya, hata alipokuwa Waziri aliplay key role kwenye kuimega Chato kutoka mkoa wa Kagera.
Sasa hilo halikuishia hapo, leo tunakwenda kuimega Ngara na Biharamulo tena na kuiundia mkoa ili iweje?

Kama mnadhani kuunda mkoa ni kusogeza huduma kwa wananchi, basi uongezeeni bajeti mkoa wa Kagera na usogezeeni huduma ili huduma ziendelee kupatikana humohumo badala ya Kuumega mkoa huo.

Chato haina vigezo vya kuwa mkoa tunalazimisha mambo kumuenzi Marehemu bila kujali misingi ya utamaduni na historia za maingiliano ya watu wa maeneo husika.

Samia Iache Kagera kama ilivyo, ila Isogezee huduma zaidi!
Huku tunapambana muungano usivunjike upande mwingine wanataka kugawanya mikoa
Siwaelewi,
 
Hiyo title inamtazamo finyu sana! Baada ya miaka 50+ ijayo hakutakuwa na mtu anayejiita pure kabila flani kwa sbb ya muingiliano (inter-trible marriages)! Faida ya kuwa na mkoa wa Chato unazidi vijihasara hivi vidogo visivyokuwa na faida yoyote kwa maisha ya kila siku ya watz! Chato itakuwa mkoa soon!
Na huo ndio ukweli "ukweli lazima usemwe"
 
Ila lugha yao wanayoongea ni kama wahaya sema wamebase sana kwenye urundi.
Mmmmh hapana Wahaya lugha yao haiingiliana kabisa na wasubu au waangaza...tena ungeenda nje kidogo yaani Kihaya kinaingiliana sana na Kiganda na Kinyankore (Uganda) kuliko kisubi au kihangaza
 
Unaweza kukarabati shule bila kutukana watu au kula rambirambi

By the way kukarabati shule ni jukumu la serikali siyo hisani, maana serikali inakusanaya kodi hata kutoka mkoani Kagera pia
Huyo alisikia zile taarifa za kwenye makaratasi kuwa serikali imechangia katika gharama za ukarabati wa shule ya Ihungo....hakuna kitu ambacho hakikujulikana....hayati alikuwa na chuki za waziwazi kwa Wahaya jamani msibishi sana ....na ile Meli kama ingekuwa haihudumii maeneo ya Mwanza pia isingekarabatiwa kamwe....
 
Lakini kibaya zaidi, Leo tunakwenda kukata eneo la mkoa ambao by all standards ni mkoa kongwe, wenye historia ndefu, Mkoa wa Kagera, uliobeba historia ya nchi hii
Kwani ni mkoa upi haujabeba historia ya Tanzania? Watu wana-suggest kumegwa kwa mikoa ya Morogoro na Tabora ina maana haina umuhimu kwa taifa kama Kagera?
 
Hadi Muleba itamegwa. Chezea malaika mkuu! Na mbaya zaidi jinamizi la huyu mtu lipo nyuma ya mama Samia.

Hatari sana. Mikoa ya kumegwa ni Tabora na Morogoro sio Geita.
 
kukarabati shule ni jukumu la serikali siyo hisani, maana serikali inakusanaya kodi hata kutoka mkoani Kagera pia
Sio kila jambo ni serikali tuuuu hapana mkuu, wananchi pia wanaweza kuanzisha harambee kwa lengo la kufanya shughuli za maendeleo ndani ya eneo lao kama vile kukarabati majengo ya shule na vituo vya afya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom