Kuuliza si ujinga

Kuuliza si ujinga

Kijana Jr

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2016
Posts
564
Reaction score
889
Ihabarini wakuu Hivi ni nani mmiliki mkuu wa internet .mfano....yaani tunavyomlipa Voda ,tigo ttcl nk na yeye anamlipa nani? Kumuwezasha kupata internet hiyo je na kama inavyosenekana internet inamilikiwa na America(nasa)ambao ndio waanzilishi wa internet mbona wapinzani wake north Korea,kwa kiduku wanapata internet kwanini wasiwazimie
 
Internet haimilikiwi na mtu/ taasisi/ kitu chochote duniani Ila Kuna board maalumu kwa ajili ya kusimamia ubora na viwango vya Internet.
Internet is free Zone.
INTERNET NI MUUNGANIKO WA NETWORKS TOFAUTI ILI KUPATA NA KUSAMBAZA TAARIFA KUPITIA WEB.
 
Hakuna aneimiliki internet, ila kuna anaekuwezesha kuipata, ambayo ndiyo hiyo mitandao ya simu.
 
Je hawa service provider hizi mb na gb wanatotuuzia je wao wanazipata wapi
Kuongezea mkuu kuna makampuni yanayogundua hizi technology na kuwauzia mitandao ya simu. Mfano Huawei, Ericson, Nokia, Zte etc

Hayo makampuni yanagundua miundombinu kama vile vifaa vinavyofungwa kwenye minara ya simu, software za uendeshaji, etc kisha wanauza kwa mitandao ya simu ambao wao wanatusambazia sisi.

Hapa tunazungumzia mobile data, internet inaweza kutumika kwa mifumo mingi kuna wengine wanatumia fiber, wengine satelite etc kote huko utakuta kuna wagunduzi wake nako ambao wanatengeneza na kuwauzia ISP.
 
hivyo ni vipimo tu. kama vile ilivyo kilo ya nyama au unga.
kwenye internet tuna bytes, kilobytes,megabytes,gigabytes na terrabytes

wakati vipimo vyakawaida tuna milgram, gram,kilogram, n.k
kama ilivyo kwenye vipimo vya urefu
kuna milmita,sentimita n.k
Hujajibu swali?
Wanapata wapi?
 
Hujajibu swali?
Wanapata wapi?
Mkuu kichwa chako kigumu sana inaonekana. Embu mpitie chief mkwawa hapo juu naona kakujibu vizuri. Na kuna jamaa mapema tu kakujibu vizuri.
Hii hapa

INTERNET NI MUUNGANIKO WA NETWORKS TOFAUTI ILI KUPATA NA KUSAMBAZA TAARIFA KUPITIA WEB.

Sasa utaipataje huduma hiyo ndio unaitaji mtu mwenye nyenzo ambaye anakuwezesha kuipata. Hapo ndio kuna tigo aitel n.k na wao pia wanachukua hiyo huduma mahali kama alivosema chief mkwawa.
 
Mkuu kichwa chako kigumu sana inaonekana. Embu mpitie chief mkwawa hapo juu naona kakujibu vizuri. Na kuna jamaa mapema tu kakujibu vizuri.
Wewe Ubongo wako ndio mgumu. Kichwa kuwa kigumu ni sawa kwa kila mtu.
Wajibu wengine ujifanye wewe ndio umejibu.
 
Back
Top Bottom