Kuuliza si ujinga

Kuuliza si ujinga

Ngoma hii ni mali ya jeshi la kimarekani, na nakumbuka wakati trump aliposema afrika ni shit hole alishambuliwa sana kwa kutukanwa na alisema kwa jazma kuwa wanatumia internet yao halafu wanamtukana, angeweza kuifunga.
 
Sisi watu weusi hatupendani na manenooo meeengi kumbe ushuzii na ushubwada tu. Hili swali ni zuri sana likipata mwenye kujua jibu in and out.

Eti internet haina mmiliki ni alafu hapo hapo ni muunganiko wa netwok ? Hizo network from whom ? Mara oooooh mifano tigo, voda ? Kweli tujue kujibu jamani. Hili sio swali la kukurupuka tu.
 
Je hawa service provider hizi mb na gb wanatotuuzia je wao wanazipata wapi
Mkuu kwanza unatakiwa kujua space occupied by a data or information on Internet is measured in terms of gb or mb etc.
Kwa hiyo hawa ISP ( internet service provided) wananunua hiyo bandwidth ( mbps or gb) kutoka kwenye company nyingine au nchi nyingine.
 
Ngoja nilahisishe swali la mtoa mada.

Ni hivi, mimesema internet haimilikiwi na MTU au mamlaka yoyote sasa iweje kuwe na kulipia ili kuipata, yaani ni hivi sisi tunanunua GB na mb kwa service provider nawao wanapata sehemu x, na hao sehemu x watakuwa wanapata sehemu Y hivyo line itaenda mpaka kwa wakwanza kabisa ambaye yeye hanunui kwayoyote, swali je uyo ni nani na kama yupo iyo basi ndiye anaemiliki Internet.

Niongeza unazani Internet imetokea tu from nowhere hapa kuna aliyeileta basi ikiwa hivyo huyo ndie anaemiliki.

Niongeza inasemekana Internet ya NASA ina speed ya 100+G kama sikosei je nani kawawezesha hivyo ikiwa sie tupo kwenye 4G.

NB: hivi vitu vinaitaji mtu mjuzi sio unajua coding tu ndio utajua hivi vitu.
 
Ngoja nijaribu kujibu maswali yako jinsi ninavyoelewa kuhusu internet:

Nani mmiliki mkuu wa internet?, Tunapolipa mitandao ya simu analipwa nani?

Hakuna mmiliki mkuu wa internet bali kuna vyombo mbalimbali vinavyohusika kupangilia mfumo mzima wa internet unatekelezwaje, juu kabisa ipo IANA ambao wao ndio wanaohusika kugawa IP addresses ambazo zinawezesha vifaa viweze kuwasiliana katika network, IANA husaidiana na Regional Internet Registry (RIR) katika kugawanya hizi IP addresses, kuna RIR 5 ambazo zimegawanyika kwenye kanda/mabara tofauti na huduma zote za kugawa IP address katika kanda husika hufanywa na RIR ya kanda hiyo kwa niaba ya IANA. RIR hizo ni:

AFRINIC-Kanda ya Africa
ARIN
APNIC
LACNIC
RIPE NCC

Nitadeal na AFRINIC kwa vile ndo inatuhusu. AFRINIC huchukua IP address ilizopangiwa na kuzivunjwa na kuzigawa katika mafungu na kugawa kwa Autonomous Systems(AS), hizi AS zinaweza kuwa ni makampuni kama vile Google, Microsoft, Amazon au ISP kama vile Vodacom, Tigo , Ttcl etc. Kila Autonomous System hupewa namba yake inayoitofautisha na nyingine iitwayo Autonomous System Number (ASN), AS hupewa mafungu haya ya IP address (ambayo anabidi kulipia kwa RIR) ili ziweze kutumia kufanya mawasiliano katika network ambayo pia huziunganisha AS zingine.
Jinsi gani AS ataziunganisha hizo IP na network itategemea na miundombinu yake mwenyewe na ana uhuru wa kuruhusu au kukataa vifaa vyovyote kadiri aonavyo yeye kutumia miundombinu hiyo. Kwa maana hyo AS anaweza kutumia miundombinu yake kufanya biashara kwa traffic yoyote au kifaa chochote kinachotoumia miundombinu yake kufanya mawasiliano na kifaa kingine kilicho katika AS tofauti, hivi ndivyo makampuni ya simu kama Voda na Tigo yanavyotoza huduma hii na hupima tozo hizo kutokana na kiasi cha data(taarifa) kifaa kinachotuma na kupokea (upload and download), kiasi cha data hupimwa katika bytes,kilobytes(Kb), megabytes(MB), gigabytes(GB) n.k, zipo huduma nyingine zinazoweza kutolewa kwenye AS kama vile hosting n.k. Muunganiko huu wa kimtandao wa Autonomous Systems(AS) katika kanda/mabara tofauti hufanya mtandao huu kusambaa dunia nzima na kuitwa INTERNET na kifaa chochote kitachoweza kuunganishwa na mtandao huu basi kitaweza kuwasiliana na kifaa kingine chochote kilicho katika mtandao huu.

Kwa mitandao ya simu hapa Tanzania ASN number zake ni:
AS37133 Airtel Tanzania
AS37035 MIC TANZANIA LTD (Tigo)
AS36908 Vodacom Tanzania Ltd
AS36930 Zanzibar Telecom(Zantel)

Kwa list nzima nenda hapa

Baadhi ya makampuni ASN zao ni:
Google - AS45566, AS41264, AS36492 n.k..
Microsoft- AS8069, AS26222, AS8072 n.k..

Kwa nini North Korea wanapata Internet?

Kwa sababu nao wana AS iliyopewa fungu la IP address na RIR wao ambaye ni APNIC hata hivyo wana AS moja tu kwa nchi nzima na fungu lao katika AS lina IP address chache mno (1024), kwa sababu hii hata wao wanaweza kuaccess internet hata kama ni kwa mbinde.
AS131279 Ryugyong-dong. Hiyo ndo AS yao ya pekee yenye IP address 1024

Kwa maelezo zaidi kuhusu internet ya North Korea unaweza cheki kwenye wikipedia
 
Noted
 
Ihabarini wakuu Hivi ni nani mmiliki mkuu wa internet .mfano....yaani tunavyomlipa Voda ,tigo ttcl nk na yeye anamlipa nani? Kumuwezasha kupata internet hiyo je na kama inavyosenekana internet inamilikiwa na America(nasa)ambao ndio waanzilishi wa internet mbona wapinzani wake north Korea,kwa kiduku wanapata internet kwanini wasiwazimie
https://www.quora.com/Who-owns-the-Internet
hakuna mmiliki wa internet
ni sawa na kuuliza “nani anamiliki kilimo duniani?”
 
Back
Top Bottom