Serikali zenye bando za gharama kubwa zinazalisha vijana maskini kwa kuwanyima intaneti isiyo na kikomo

instagram

JF-Expert Member
May 27, 2014
2,091
4,716
INFORMATION IS POWER

Miaka yote mkoloni ametumia udhaifu wa information kuwatawala waafrika na viongozi wa kiafrika bila kujua wameingia kwenye mtego wa mabeberu kwa kuwaminya wananchi wao taarifa.

Tangu Uhuru africa tumebaki nyuma kwa kukosa vitabu vyenye ubora kulinganisha na wenzetu wazungu ambapo shule zetu zimekuwa zikitumia vitabu vilivyopitwa na wakati na visivyoendana na Research and Development updates zinazotolewa na kufadhiliwa kwa mabillioni ya pesa na makampuni makubwa na vyuo vikuu na taasisi mbali mbali zinazofadhiliwa na serikali na mabilionea kwenye nyanja mbalimbali.

Tangu kuingia kwa internet waafrika tumekuwa na nafasi ya ku leverage ukosefu wa vitabu vya kisasa, na machapisho ya R&D ya gunduzi mbalimbali za kisasa na tutorials za kisasa ambazo zinapatikana kwa urahisi zaidi online kwa vijana wenye nia na uwezo wa kupambana katika nyanja mbalimbali za maendeleo ya kidunia kama wenzao katika nchi za mabeberu.

Leo hii serikali za kiafrika zinaona internet kama vyombo vya ngono, wapinzani na wanaharakati kiasi kwamba serikali zetu ziko busy kubana matumizi ya internet kwa wananchi wao na kupelekea wananchi hao kubakia kuwa watumiaji wa apps tu za mabeberu za TikTok na Instagram na Facebook na kuwaingizia faida mabebeberu na wananchi kuendelea kuwa mambumbumbu wa information za faida kupitia internet.

Hapo mwanzo internet ilikuwa unalipia kwa mwezi kupitia ISP (internet service providers) unapata unlimited internet ya kuweza kufanya mambo yako yote kupitia ISP kama TTCL broadband ambayo ulikuwa unalipia elfu 50 nazani kwa mwezi unapata unlimited internet.

Mabeberu baada ya kuona walitunyima vitabu na machapisho yenye ubora na sasa tunayapata kupitia internet, wakashawishi serikali zetu zije na internet bundles ili mwafrika asiwe na unlimited internet aishie tu kuwa mtumiaji wa apps za mabeberu za WhatsApp, Instagram, na Facebook na TikTok na kuwaingizia mabeberu faida na siyo kuwa na unlimited internet ambayo vijana wetu wangeshinda online mda wote kujifunza programming, na ku access video tutorials za engineering, Astronomy, na kufanya mambo mengi ya e-commerce na online business.

Mabeberu walijua kwamba ukimpa mwafrika bundles ataishia kuangalia apps za mabeberu basi hatokuwa na nafasi ya kufanya mambo makubwa ya maendeleo online.

Leo hii unampa mtanzania bundle la MB 100 kwa shilling 500 unategemea kijana ataingia YouTube atafute tutorials za phyton au C++?. Ataishia tu kuingia instagram na kuangalia page za jumalokole na dr kumbuka basi bundle limeisha.

Na siyo kwamba vijana wanatumia hizi bundle vibaya bali ni hulka ya binadamu unavyompa limited access ya internet atakuwa na shauku ya kujua umbea kwanza unaendeleaje mjini kabla hajaanza kutumia internet kujifunza mambo mengine ya maendeleo na ndiyo maana hata Leon Musk yupo Twitter ana Tweet na ana tengeneza maroketi ya kwenda angani.

Sasa unavyompa kijana wa kitanzania bundle la GB 1 kwa elfu 2. Lazima ataangalia umbea wa mjini na akimaliza ataingia tutorials kujifunza mambo ya kujenga maroketi na bando litaisha kabla hajaanza.

Kwaiyo vijana wetu wamekuwa hawana option Bali kuwa watumiaji tu wa internet apps za mabeberu na siyo kwenye kujifunza mambo ya kuwaongezea ufahamu sawa na vijana wengine nchi za ulaya na zingine ambazo vijana wana unlimited internet access ambako wanashinda na kutumia ubongo wao kuchambua na kujifunza mambo mbalimbali na kuleta maendeleo katika nchi zao na sisi tunabakia kuwa watumiaji wa gunduzi mbalimbali zinazotokana na maarifa kwa taarifa wanazozipata vijana wa kwenye nchi ambazo wanakuwa na unlimited internet.

Cha kushangaza serikali yetu ilikuwa na mradi wa mkongo wa broadband wenye lengo la kuboresha upatikinaji wa internet kwa wananchi tofauti yake internet ndiyo imezidi kuwa ghali na speed imezidi kudhoofika kila siku zinapozidi kwenda na kusababisha vijana wa kitanzania kuzidi kuwa watumwa kwenye swala la maarifa(mental slavery).

Na cha kushangaza zaidi ukienda maeneo ya mjini ambako wakazi wake kwa asilimia kubwa siyo watanzania wenye asili ya kiafrika kuna unlimited internet kutoka kwa makampuni binafsi mbalimbali kwa gharama nafuu zaidi kama Simbanet, Zuku internet, ambazo wanalipia elfu 60 kwa mwezi na wanapata unlimited internet yenye speed kubwa sana kwa wakazi wa maeneo ya masaki, upanga, kariakoo basi ukija huku kajamba nani ambako watanzania wenye asili ya afrika wanaishi hakuna coverage ya hizi kampuni. Tunaishia tu kupata internet za Tigo, Voda, halotel nk kwa MB 100 kwa shilling 500 ili tuka like picha mbilitatu kwenye apps za mabeberu alafu inatosha tusiende zaidi ya matumizi hayo ili tusipate maarifa zaidi ya tubaki kuwa watumiaji tu wa bidhaa za mabeberu.

Cha ajabu serikali yetu inacheza wimbo wa mabeberu kwa kuwanyima wananchi wake internet kwa kuzani kuwa internet ni ya wapinzani na wanaharakati wanaopinga na kukosoa serikali bila kujua kwamba kwenye internet kuna maarifa mengi sana ambayo tulikuwa hatuyapati enzi za vitabu, badala ya kupambana kuthibiti sites za ngono serikali iangalie mbali zaidi kwani internet ina faida nyingi zaidi ya kuangalia ngono.

Hata benki kuu yetu bado inacheza wimbo wa mabeberu kwa kushindwa kuruhusu swala la malipo kwa internet kwani kuna vijana wangeweza kufanya kupitia malipo ya online benki kuu ingewezesha mfumo wa malipo ya online na watanzania wengi wangekuwa na unlimited internet access biashara za mtandao zingekuwa kubwa sana na ajira za vijana zingekuwa kwa kasi, kwani vijana wengi wangeshinda mitandaoni kujifunza na kugundua mbinu mbali mbali za kuboresha maisha kwa namna ya kufanya malipo na manunuzi online tofauti na sasa ambapo vijana hawana access ya kutosha ya internet wanaishia kucheki umbea insta na kubeti kwenye apps za mabeberu.

Vijana kama walivyo mashuleni siyo wote wanafanana akili useme kwamba wote watacheki ngono tu ndiyo mana hata shule kuna vichwa hadi chuo kuna wenye GPA ya 4.7 na wenye Disko, ukiwatupa online mda wote kuna vijana watatoka na madini ya kutosha kwa maendeleo ya taifa na hatutawapata vijana hao kwa bundle za MB 100 kwa shilling 500.
 
Tatizo la wanasiasa wanadhani bkuwa kila mtu aliyepo online kazi yake ni kuwatukana.

Meko alifuta Twitter kwa sababu ya mtu mmoja kigogo bila kujua kuwa kuna #TOT mawaziri wake walikuwepo.

Twitter gulio mauzo mengi tu
 
Tatizo la wanasiasa wanadhani bkuwa kila mtu aliyepo online kazi yake ni kuwatukana.

Meko alifuta Twitter kwa sababu ya mtu mmoja kigogo bila kujua kuwa kuna #TOT mawaziri wake walikuwepo.

Twitter gulio mauzo mengi tu
Hadi tutakapopata viongozi ambao ni tech savvy tutabaki kuwa Nyuma kama taifa katika maendeleo, kwani katika dunia ya sasahivi mwenye technology ndiyo mwenye power.

Na kama waafrika tutaendelea kuwa na viongozi wenye akili mgando iko siku tutafutwa kwenye uso wa dunia hii kwa sababu mwenye technology akiamua kukufanya chochote anaweza.

Kama Africa hatutawekeza kwenye Nyuklia na IT iko siku wengine wataamua kukaa kikao na kuamua kuwa sisi waafrika hatuna maana yoyote ya kuendelea kuwamalizia hewa hapa duniani basi wakaamua kutupiga manyuklia tutokomee tuwape nafasi wabaki wao.
 
Waafrika ndivyo tuliuvyo! Tunajua kula samaki hatujui namna ya kumvua. Na yeyote anaye inuka kujifunza mbinu za kuwavua samaki hao ili asiendelea kula samaki wa asante bwana beberu, ndugu zake wanamvunja mikono na miguu. Mwafrika anafurahia sana akuone, wewe mwafrika mwenzie ukivua chupi hata mara elfu moja kuliko akuone ukijaribu kuvua samaki hata mara moja.
 
Back
Top Bottom