Mnavyolaumu huu uchaguzi utafikiri hizo chaguzi zilizopita zilikuwa za haki na uwazi,miaka yote tunalalamika kuhusu ccm kutumia dola kung'ang'ania kubaki maarakani na hao wazee wote wakiwepo pamoja na huyo marehemu. Hata huu uchaguzi ni kazi ya ccm hiyo.
Wote hatuwezi kuikubali CCM na wote hatuwezi kuwa wapinzani. Ni baadhi ni watawala ( wananufaika sana) na baadhi ni wapinzani wanaumizwa sana na kunufaika kidogo wanapopata nafsi mana nao pia wanapangiwa maslahi yao na watawala.
Hivi Lisu angekua ni mbunge wa CCM halafu apigwe risasi bungeni ingekuaje labda.?
Hatulalamiki Bali tunaizungumzia nchi yetu ili iwe na kesho njema zaidi yenye upendo na amani na Uhuru wa watu kujadili maendeleo yao badala ya kujadili maumivu na dhulma kila kukicha.
Huoni kuwa kuna matatizo kuwanyima watu wa nchi moja haki kwa sababu tu ya vyama ambavyo hata vikifa bado haviui mtu . Yani unaua watu kwa sababu ya chama ambacho hakiumwi wala hakiwezi kupelekwa ICC.
Kenya KANU ya baba yake Uhuru ilikufa lakini Leo Uhuru ni Rais wa Kenya. Sasa wangeendelea kuuana kwa sababu ya kulinda KANU si wangekua ndio wale Sithole country.
Tutafakari mambo kwa upana wake na tuweke ubinafsi na maslahi yetu pembeni . Wanaojenga nchi ni watu hivyo kuwagawa watu ni kuua nchi.
Hebu fikiri kule Kenya Wapinzani wangeamua kuleta mgomo wa kulipa Kodi ingekuaje! Yani watu wajitoe mhanga kule Kenya kuwa hawapandi magari ili wasinunue mafuta , hawapani bodaboda , wananunua baskeli kama China.
Hawanywi bia zaidi ya moja, wanatumia umeme kwa bajeti . Hawaweki vocha mana mawasiliano yanafanya uchochezi. Wanachemsha maji badala ya kununua maji ya chupa n.k. Je, Kenya ingesonga mbele kwa kasi na kuwa ndiyo nchi ya kwanza Afrika mashariki na Kati Japo ina rasilimali chache za asili ukilinganisha na Kongo na hata Uganda achilia mbali Nchi yetu Tanzania?
Tufanye kila namna ya kuwaunganisha watu.
Kuwaacha wakurugenzi waharibu uchaguzi bila kuwachukulia hatua za kinidhamu na hata kuwashataki ni kuwagawa watu na ni hatari kwa taifa. Tujiulize wananufaika na nini wanapokiuka Taratibu na sheria za nchi wakati wameapa kuzilinda?
Yani mtu anashika Korani au Biblia anaapa na kusema Mungu nieaidie halafu anakwenda kudhululumu watu.
Matokeo yake tunakua na kizazi cha watu wenye dhulma na Katili kama Mkuu wa mkoa mmoja zamani alikua katili sana na kuchoma nyumba za watu cha ajabu Leo ana mtoto katili zaidi anatembea na Bunduli kama Jambazi.
Baba yake angekemewa huenda angetubu. Sasa mwisho wake itakua ni kuwindana na kulipizana visasi.