Kutokana na ukosefu sugu wa vitendea kazi Jeshi la Zimamoto napendekeza liunganishwe na kiwe kitengo ndani ya jeshi la polisi

Siku za nyuma kidogo nilipiga simu jeshi la zimamoto na katika maongezi yetu na askari aliyekuwa mapokezi nikamuuliza ni kwanini huwa wanachelewa kufika eneo la tukio panapotokea ajali ya moto na hata wakifika huwa hakuna msaada wanaotoa.

Alichonieleza ni kuwa sio kama wanapenda kufanya hivyo bali hawana vitendea kazi vya kutosha na hivyo vilivyopo huwa mara nyingi huwa vipo kwenye garage na malipo huwa ni changamoto sana kiasi kwamba huwa wanashindwa kurespond majanga yanapotokea.

USHAURI
Najua fika jeshi la zimamoto limeanzishwa kwa Sheria za Bunge, napendekeza serikali ilivunje mara moja jeshi ili na kurudishwa kuwa kitengo cha jeshi la polisi maana naona fika askari wa jeshi ili la zimamoto huwa wapo idle sana kiasi kwamba wanaishi kwa mazoea maana hakuna kazi wanazofanya.

Tumeshuudia mkoani Kilimanjaro zaidi ya marambili soko la mbuyuni kuungua ila mara zote hizo jeshi la zimamoto mkoa wa Kilamanjaro huwa limeshindwa kutekeleza majukumu yake na mbadala wake kitengo cha zima moto kiwanda cha sukari TPC ndio huwa msaada.

Kurudishwa na kuwa kitengo ndani ya Jeshi la polisi kunaweza kuboresha ufanisi na kama hakuna majanga ya moto askari hawa wanaweza fanya majukumu mengine kama kuimarisha usala wa raia na mali zao.

Nawasilisha.
Kwahiyo Zimamoto likiunganishwa na Polisi ndo vitendea kazi vitapatikana? Hoja hapa ni kuongeza vifaa/vitendea kazi,
 
Umchelewa it is too late. Sijaona sababu ya maana kwanini livunjwe?
Zimamoto limeisha kwenda mbali mno, majukumu yao na police hayafanani tena, unahitaji ku retrain jeshi zima ku fit police again. Serikal haito ingia gharama hizo.

Zima moto wamekuwa ni kama step child wa serikali, jeshi liwezeshwe kwenye vifaa na mafunzo
💪
 
Kwahiyo Zimamoto likiunganishwa na Polisi ndo vitendea kazi vitapatikana? Hoja hapa ni kuongeza vifaa/vitendea kazi,
namaanisha kikiwa ni kitengo ndani ya jeshi la polisi watafanya majukumu mengine wakati majanga yanapokuwa hayapo.Pia vitendea kazi vipo ila kuna kauzembe ndani ya ili jeshi
 
Ushauri mzuri hii. Kwa upande wangu ningependekeza liongezewe nguvu na lisiwe la zimamoto tu, bali liwe la Kukabiliana na Majanga aina yote.
kimuundo linaitwa Jeshi la zima moto na uokoaji, ambapo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeundwa na kufanya kazi chini ya sheria namba 14 ya mwaka 2007 “FIRE AND RESCUE FORCE ACT
 
Wana vifaaa au unataka wanunue vifaa kwa mishahara yao? we mjinga mno, hili swali kawaulize wanunua V8
vifaa vipo japo kuna kasumba ya kufanyia maitanance hivyo vifaa yakiwemo magari.Ndio maana nimeshauri livunjwe na kuwa kitengo kidogo
 
kimuundo linaitwa Jeshi la zima moto na uokoaji, ambapo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeundwa na kufanya kazi chini ya sheria namba 14 ya mwaka 2007 “FIRE AND RESCUE FORCE ACT
Shukrani Mkuu Andrew. Ningetamani kujua Majanga kwa mfano say mradi mpya kama Stiegler au SGR responsibility ya distaster management bado iko chini ya Jeshi hili?
 
Inawezekana nikanekana sina adabu ila nawaambia,hakuna tasisi yoyote nchi hii ambayo inafanya kazi kama inavyotakiwa.

Kila sehemu utakapokuta mapungufu utapewa msururu wa changamoto zinazosababisha,maana hakuna mifumo imara wa uwajibishaji.

Taasisi za watu binafsi/mashirika/na makampuni ya biashara,hutoa uongozi kwa watu smart na wanaoweza kuongeza tija na ufanisi ili kukuza faida na kampuni kwa ujumla,hakuna anayeajiriwa sababu ni mzuri ktk kusifu.

Watu smart wanapigwa majungu wanafichwa ubarozini au kustaafishwa kabisa,tunaacha mzezeta.
 
Si lilikuwa ni idara ya Polisi kabla ya JPM kulifanya Jeshi Kamili, ili kuondoa mgogoro wa kugombea u-IGP kwa kina Chagonja na Andengenye na wenzao!!

Akampa Changonja u-RAS Katavi na Andengenye akampa ukuu wa Jeshi la Zimamoto ambako Andengenye alinunua vifaa vya kuzimia moto kwa fedha kubwa 'pasipo' ushiriki wala ridhaa ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na akaondolewa kwenye nafasi yeye pamoja na Kangi Lugora, aliyekuwa Waziri wa mambo ya ndani wakati huo.

Kulirudisha polisi ni wazo jema, ila kuwanunulia vifaa vya uokozi ni jambo jema zaidi.
Haikuwahi kuwa ndani ya Jeshi la Polisi bali lilikuwa chini ya Halmashauri na gari zao zilikuwa zikitumia namba za SM.
Maoni ya kutaka kiwe kitengo ndani ya Jeshi la Polisi sio ufumbuzi bali ni kukwepa utatuzi wa tatizo.
Muhimu ni kuboresha vitendea kazi na kuongeza rasilimali watu katika Jeshi la Zimamoto na uokoaji ili kuliongezea ufanisi katika utendaji wake.
 
Watu Binafsi waruhusiwe kufungua Fire Brigade zao hao watakuwa Fasta kuja kuzima Moto.
Hakuna sheria inayokataza watu binafsi au kampuni kuanzisha vitengo vyenye majukumu hayo ya kuzima moto na uokoaji, ndiyo maana kuna kampuni kadhaa binafsi za ulinzi wana package hiyo katika huduma zao. i.e Garda world etc.
 
Moto hautokei Kila siku ila Viongozi wanasafari Kila siku za kutuletea maendeleo,hivyo V8 kwanza matinga ya kuzima moto baadae.
 
Hakuna sheria inayokataza watu binafsi au kampuni kuanzisha vitengo vyenye majukumu hayo ya kuzima moto na uokoaji, ndiyo maana kuna kampuni kadhaa binafsi za ulinzi wana package hiyo katika huduma zao. i.e Garda wold etc.
Sasa itabidi Manispaa na Halmashauri ziwe zinalipa kila mara moto unapozimishwa.
 
Haikuwahi kuwa ndani ya Jeshi la Polisi bali lilikuwa chini ya Halmashauri na gari zao zilikuwa zikitumia namba za SM.
Maoni ya kutaka kiwe kitengo ndani ya Jeshi la Polisi sio ufumbuzi bali ni kukwepa utatuzi wa tatizo.
Muhimu ni kuboresha vitendea kazi na kuongeza rasilimali watu katika Jeshi la Zimamoto na uokoaji ili kuliongezea ufanisi katika utendaji wake.
Hapana mkuu, kwamba ilikua chini ya Halmashauri ninaona kama unajielekeza vibaya. Ilikuwa chini ya jeshi la Polisi na hata faini ya kukosa stika ya zimamoto ilikuwa inatozwa na jeshi la Polisi na sio Halmashauri.

Halmashauri zilikuwa zinanunua magari yao ya zimamoto pale pasipokuwa na idara ya zimamoto ya Polisi, kwa kuwa zimamoto walikuwaga vituo vikuu tu vya polisi (central posts), yaani mikoani kama ilivyokua kwa FFU (hawa nafikiri mpaka sasa wapo makao makuu ya mkoa tu).

Hayo magari yenye SM, yalikuwa yanamilikiwa na Halmashauri kwa Wilaya zilizo nje ya makao makuu ya mkoa. Wasingeweza kusubiri gari lifike kutoka mkoani wakati nyumba inateketea, ndipo wakapanga bajeti za zimamoto nk
 
Back
Top Bottom