Kutoka ndani ya moyo wangu

Kutoka ndani ya moyo wangu

...umeongea jambo la maana sana,
ni jukumu letu wanaume 'kumlinda' mke na hao ndugu.
Wakati huo huo, ni jukumu letu pia kulinda hadhi ya familia kwa huyo mke,
sio mwanaume unakuwa haujitambui,...unapelekeshwa tu kama bendera fata upepo!

Kwenye ndoa hakuna classes kusema ati mama mzazi ndio 1st Class, 2nd Class mawifi, na 3rd Class Mkeo
au Vice Versa...! Kwenye ndoa kila mtu ana mipaka yake, na hiyo mipaka izingatiwe na kuheshimiwa hata ikibidi
kwa 'kununiana!'
upo sahihi kabisa rafiki,
hako kapicha kameniacha hoi....... hapo sijui pande ipi itaelemewa, na nani?
Waume mna kazi kweli. Ukijitambua na kujua majukumu yako mambo yako yatakuwa bomba, ila ukifwata upepo basi hali ndo inakuwa kama hivi.
 
yap, ni kizaazaa kiukweli, yote yawezekana, lakini kutokana na hili mwanamke ulishindwa kucheza nafasi yako kunusuru haya yasitokee? nimesoma pia wamehama kwenye villa waliyokuwa wanaishi pamoja, sasa wewe mwanamke unaejua una ishu na hii familia ungecheza part yako kuweka mambo sawa ili wao ndio wajione wajinga, sidhani kama kuna mwanamke aliyeolewa hajapitia kashkash za ndoa, kama wapo wamebarikiwa, mie nilipitia na wifi/mama mkwe, mgogoro haswaaaa, lakini nilipambana baba mkwe wangu ni bonge la muelewa alinisaidia sana katika kizaazaa nilichopitia, hapo ningesema ninunue kesi ingekuwa mtafaruku mkubwa sana,msukuma alikuwa hakubaliani na mama/dada yake hata kidogo, na kama sio mimi kumtuliza ingeshazaa mtafakuru haswaa, nililaumiwa kwa kila namna lakini nilipambana na sasa hivi ni marafiki zangu wakubwa sana, tunapopitia changamoto kwenye ndoa tusizikuze/chochea, bali tuangalie namna ya kupambana nazo.
kuna wamama hawana say kwenye familia.....
mume akisema leo woooteeeee tunavaa bukta kwenda mazoezi basi ndo hivyo inavyokuwa, hata kama wewe si mtu wa mazoezi. Mke wa Peter anachukiwa tu, na wanadhani labda kwa sababu ya umri wake kumzidi mume basi yeye ndo msemaji wa familia. Inawezekana kabisa Lola hana say kwa Peter, kwa hiyo hata swala la kuhama asingekuwa na uwezo wa kubishia.
Kuna mkaka alihama nyumba akamwacha mke na watoto ndani sababu mke alikuwa anakataa kuhama. ni stori ndefu, lakini mwisho wa siku bibie mwenyewe alifungasha virago na kumfwata huko alikoenda
 
Mmiliki ndo nani? kuna mmiliki wa mtu?
hata mke/mume siyo mmiliki wa mwenzi wake, mmiliki ni Mungu pekee ndo maana anakuleta na kukuchukua siku anayoitaka yeye.
Malezi yanakuwepo kwa zamu. Mama anaanza..... baba/dada/shangazi n.k wanaendelea...... mume/mke anamalizia. tumia ujuzi wako woote kumlea mtu anapokuwa mikononi mwako, akiondoka kubali kuwa sasa ni zamu ya wengine kulea.
Kuna kaswali najiulizaga, hivi wazazi wa wanawake huwa hawana uchungu na watoto wao? mbona hakuna migogoro hii ya kijinga inayotoka huko? binti akishaolewa wazazi hujiweka kando kabisaaaaaa.
Lile swala la kuacha baba yako na mama yako na kuambatana na mwenzio huwa ni kwa wamama tu?

umenikumbusha mbali, enzi nikikorofishana na msukuma nilikuwa nakimbilia kupumzika kwa mama nyamayao, basi nikifika kule nampa stori weee, anaishilia kusema yaani jamani sijui kwanini hamkuwa wanaume wanangu, mana nina nyie wawili tu lakini hizo familia za waume zenu wapo wanne kuendelea mbona hawanionei huruma na wanangu? hahahaha akimaanisha tungekuwa wanaume tusingekuwa tunakimbia kimbia vile, malalamishi/masimango huku kule, mweeh, lakini kila kitu kina muda wake, wengine tumepitia hiyo michakato sasa hivi tupo shwari kabisa, tumebakia kuwa wasikilizaji/watazamaji.
 
hilo linawezekana sana pia, naona Jude mwenyewe ameshindwa kuweka mambo sawa mana na yeye ni mmoja wa mlalamishi kuhusu kuolewa kwa Lola, anasema mbona hakumuoa Lola wakati mama yao yupo hai, kitu kinachoonyesha kwamba familia ilikuwa haimkubali Lola kuanzia mwanzo, lakini hii mitafaruku ya familia hii aisee, kama inaweza kuombewa/kuepukwa na iepukwe kwa gharama yoyote ile, imagine P2 walivyotoka mbali, walivyojitahidi kupata mafanikio waliyonayo mpaka kufikia hapo, leo "mtafaruku" unasambaratisha familia.
 
Umeona eeeh! nasi tunapendwa sana kwetu na wazazi wetu wanatamani sana wangeendelea kubaki na sisi. Nikiangalia mamangu kwa sasa yupo peke yake (baada ya baba kufariki) amebaki kuokota tu watoto wa barabarani akae nao. unafikiri asingetamani angalau mmoja wetu abaki naye?
 
huo ni upepo tu, utapita......
Ila Jude ana uhakika gani kama Peter asingemuoa mkewe mamake angeendelea kuishi?
wamama wangapi wamekataa wanawe kuoa mwanamke fulani na still wakaoa na wao wapo hai?
Muda wao wa kuona haukuwa tayari hata kama walishaanza kuzaa watoto
 
Kabla sijaliongelea hili na-declare interest kuwa mimi ni MKE (WIFE).
Kuna ambao watadhani kuwa huu ni utetezi kwa sababu (huenda) nami nikakumbwa na hiki kimbunga siku moja.
Kutoka ndani ya moyo wangu nachukia sana sentensi kama hizi. Mara nyingi familia zinapoingia kwenye migogoro basi mtu wa kwanza kutupiwa lawama huwa ni mke wa mmoja au zaidi walioingia katika familia hiyo. Na mbaya zaidi mama katika familia hiyo anaweza kuwa mstari wa mbele kushikilia hilo, anasahau kabisa kuwa naye alikuwa mke kwenye hiyo familia. Huwa inasikitisha sana na sijui kwa nini watu wanawaza hivyo.
Napenda niwaeleze ndugu wa waume zetu kuwa sisi (wake) tunatambua umuhimu wa familia za waume zetu kuwa na umoja. Msifikirie kuwa kila kibaya ambacho mume anachokifanya kwa familia basi shinikizo linatoka kwa mkewe. Kuna wake ambao ni Blessings katika familia za waume zao, tusiendelee kuwakwaza kwa maneno kama haya.
Nawatakia uvumilivu wake wenzangu pindi tunaposikia maneno kama haya. Mungu anaona nia zetu NJEMA.
Mubarikiwe sana

mimi huwa namwambia wife bila wewe siwezi fanikiwa na nikweli Mungu ametubariki kwa kila eneo. Na ndio mpango wa Mungu mke ana sehemu kubwa sana kwa mafanikio ya mme wake. Na sisi tunaoamini katika Yesu mke akilia, akikwazika, akisikitika, akinuna mwanaume tambua hutafanikiwa hata iweje. wanawake Mungu awabariki sana maana bila nyie sisi hatujakamilika na itabaki hivyo milele!!
 
AMINA!!!!!!
Ila na ndugu zako wanafahamu hilo?
Je unapokuwa na mgongano kidogo na ndugu zako (wazazi, siblings, ndugu), mkeo hashutumiwi kuwa ni chanzo?
 
Katika hali ya kawaida wanawake wana nature ya ugomvi ugomvi;

Ukichukua mifano michache ifuatayo utaona picha

1. Dada na dada wakikaa pamoja mwezi hauishi kabla hajamaindiana (ugomvi mkubwa unaweza kuanzishwa kwa kitu kidogo), wakati kaka na kaka wanaweza kumaliza hata mwaka hawajagombana.

2. Mara nyingi bosi wa kike haelewani na subordinates wa kike kama bosi wa kiume anavyoelewana na subordinates wake wa kike

3. Framework ya interpretation ya mwanamke mmoja ni tofauti na ya mwanamke mwingine kwa asilimia kubwa sana na ziko very complicated, kiasi kwamba neno moja linaweza kutafsiriwa zaidi ya mara 5 tofauti

4. Wanawake kwa wanawake wanaoneana wivu sana kuliko, na hii ndio chanzo cha na 1 na 2 ikibidi hata 3, neno la kawaida au tabasamu linaweza likaleta tafsiri ya dharau, kujiona etc na hiki ndio chanzo cha magomvi mengi na kutafuta kukomoana
 
Mabaya huwa anabeba mke mazuri yote anabeba mume

Ila kuna wake vichomi na wake baraka

Vivyk hivyo kuna waume vichomi na waume baraka

Ila kiafrica mke utabeba lawama tu
Ukizingatia ukiolewa ukoo mzima wanadhani wamekuoa

Na kwenye familia usiombee kuolewa na familia ambayo mume ndo mwenye kipato lazima uwe mbaya

Au kama ndo familia inawatazama
Au familia ambayo wamezoea kupanga vitu kifamilia wanasahau mume anapooa sasa anapanga familia yake; wao wanadhani bado atawashirikisha kwenye mambo yake yote hata ya chumbani

Inabidi kujua mipaka pale mtu anapooa au kuolewa la sivyo mke atabeba lawama tu
 
Umeona eeeh! nasi tunapendwa sana kwetu na wazazi wetu wanatamani sana wangeendelea kubaki na sisi. Nikiangalia mamangu kwa sasa yupo peke yake (baada ya baba kufariki) amebaki kuokota tu watoto wa barabarani akae nao. unafikiri asingetamani angalau mmoja wetu abaki naye?

halafu sasa ukienda kwenu kusalimia ukikaa week moja simu mfululizo, ooh naona nije kukuchukua sasa mana umezamia, oohh unamuachaje mume wako siku zote hizo unategemea nini? ngoja uwe umeenda kwao sasa, simu ni za salamu basiii, naona kwa wanawake wengi inatutokea hii kitu,wacha tu, ukibaki nyumbani jamii watakunyooshea vidole huolewi, mwanaume akae kwao mpaka 40's na bila kuoa jamii inaona poa tu, wanawake tunasumbuka sana.
 
huo ni upepo tu, utapita......
Ila Jude ana uhakika gani kama Peter asingemuoa mkewe mamake angeendelea kuishi?
wamama wangapi wamekataa wanawe kuoa mwanamke fulani na still wakaoa na wao wapo hai?
Muda wao wa kuona haukuwa tayari hata kama walishaanza kuzaa watoto

sasa hii ya kifamilia zaidi, huwezi kujua mama alikuwa anaongea mangapi na firstborn wake.
 
AMINA!!!!!!
Ila na ndugu zako wanafahamu hilo?
Je unapokuwa na mgongano kidogo na ndugu zako (wazazi, siblings, ndugu), mkeo hashutumiwi kuwa ni chanzo?

wanajua sana! im very tough. issue inabakia wewe mwanaume unasimama wapi. yani mme akiwa bendera fuata upepo mke anapata shida sana. mke wangu ni mpole sana na wala sio muongeaji sasa akikutana na ndugu mdomo mdomo ni shughuli sana sasa hapo mme ndo usimame. ili ufanikiwe inabidi muwe na by-laws za nyumbani and should be adhered
 
Topic nzuri, naifuatilia kwa karibu beste.

Wakwe ni janga la dunia, ingawa kwa nchi maskini linakuwa kubwa zaidi.
 
...hii yote inatokana na dhana ya kwamba nani ana haki zaidi juu yako (Mume)...

1. Mama mzazi anajiona yeye kalea mimba, amezaa na kuteseka na ulezi wa kichanga mpaka kufikia kutembea, kusema na mwishowe kujitegemea...
2. Madada (Mawifi) hawa huona wao ni ndugu toka nitoke....wamezaliwa tumbo moja na ndugu yao, wanajihisi wanauchungu wa damu kuliko weye Mke mtu baki tu ambaye hata ukiachika ataolewa mwingine...
3. Mke, ....huyu anajiona yeye ndiye aliyechaguliwa kuwa mama wa watoto wa huyo Bwana Mkubwa, Mwenza na mengineyo mengi yakiwemo faragha faraghani....!

Ni ubinafsi na "wivu" wa kijinga tu ambao wanawake wengi wamejaaliwa nao!
watu kutojua mipaka yao.
Mmiliki ndo nani? kuna mmiliki wa mtu?
hata mke/mume siyo mmiliki wa mwenzi wake, mmiliki ni Mungu pekee ndo maana anakuleta na kukuchukua siku anayoitaka yeye.
Malezi yanakuwepo kwa zamu. Mama anaanza..... baba/dada/shangazi n.k wanaendelea...... mume/mke anamalizia. tumia ujuzi wako woote kumlea mtu anapokuwa mikononi mwako, akiondoka kubali kuwa sasa ni zamu ya wengine kulea.
Kuna kaswali najiulizaga, hivi wazazi wa wanawake huwa hawana uchungu na watoto wao? mbona hakuna migogoro hii ya kijinga inayotoka huko? binti akishaolewa wazazi hujiweka kando kabisaaaaaa.
Lile swala la kuacha baba yako na mama yako na kuambatana na mwenzio huwa ni kwa wamama tu?

.....Enheee! Umeona sasa...!? Misuguano ya kifikra huanza namna hii.

....mimi nimetumia neno HAKI kwa maana ya Rights,
wewe umetafsiri na kumaanisha UMILIKI kwa maana ya OWNERSHIP au sio?
Once watapoweza kutofautisha "dhana" hizi mbili na wote kujitambua haki za msingi
hakutakuwa na mivutano namna hii....

Ni kiasi cha kujitambua tu.
 
Samahani kwa kupoteza ulichomaanisha. Ila sikuwa nakubishia nilikuwa najaribu kufafanua tu
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
wanajua sana! im very tough. issue inabakia wewe mwanaume unasimama wapi. yani mme akiwa bendera fuata upepo mke anapata shida sana. mke wangu ni mpole sana na wala sio muongeaji sasa akikutana na ndugu mdomo mdomo ni shughuli sana sasa hapo mme ndo usimame. ili ufanikiwe inabidi muwe na by-laws za nyumbani and should be adhered

Kuwa tough ni one thing, hiyo haizuii kumsingizia mkeo kuwa chanzo cha mgogoro, hata kama utamtetea baadae
 
Back
Top Bottom