Kutoka ndani ya moyo wangu

Kutoka ndani ya moyo wangu

Lakini kwanini hii migogoro itokee baada tu ya mke kuingia kwenye hizi familia???Mara nyingi mtu akioa, wanamke anataka yeye tuu ndio apewe atension, kunakuwa na shinikizo la kukata mawasiliano yote hata na familia yake. Hapo ndipo wanawake wanapokosea.
 
Kabla sijaliongelea hili na-declare interest kuwa mimi ni MKE (WIFE).
Kuna ambao watadhani kuwa huu ni utetezi kwa sababu (huenda) nami nikakumbwa na hiki kimbunga siku moja.
Kutoka ndani ya moyo wangu nachukia sana sentensi kama hizi. Mara nyingi familia zinapoingia kwenye migogoro basi mtu wa kwanza kutupiwa lawama huwa ni mke wa mmoja au zaidi walioingia katika familia hiyo. Na mbaya zaidi mama katika familia hiyo anaweza kuwa mstari wa mbele kushikilia hilo, anasahau kabisa kuwa naye alikuwa mke kwenye hiyo familia. Huwa inasikitisha sana na sijui kwa nini watu wanawaza hivyo.
Napenda niwaeleze ndugu wa waume zetu kuwa sisi (wake) tunatambua umuhimu wa familia za waume zetu kuwa na umoja. Msifikirie kuwa kila kibaya ambacho mume anachokifanya kwa familia basi shinikizo linatoka kwa mkewe. Kuna wake ambao ni Blessings katika familia za waume zao, tusiendelee kuwakwaza kwa maneno kama haya.
Nawatakia uvumilivu wake wenzangu pindi tunaposikia maneno kama haya. Mungu anaona nia zetu NJEMA.
Mubarikiwe sana

(kwenye red!), sijui ni kwa nini lakini wanawake wengi mna "chuki" (sipendi kulitumia hilo neno lakini nimekosa neno mbadala) na mama mkwe! wewe mwenyewe ni mwanamke, kwa lugha nyingine utakuwa mkwe wa mtu kwa wakati fulani! mara wifi, dont you have brothers?!! WANAWAKE MNA MATATIZO YENU.
 
Amina.......
Tatizo mara nyingi zinapotokea changamoto huwa tunahukumu kabla hatujasikilizia kuona hizo hekima za watu wetu

Macho yao wenye hekima yamo kichwani mwao.....ndiyo maana Mfalme Sulemani aliwapo nafasi ya kujitetea wale akina mama waliogombania mtoto ndiyo akatoa hukumu ya haki......hukumu ya haki hupatikana baada ya kusikiliza pande zote."........haki na hukumu zinahudhuria mbele zako"

 
Lakini kwanini hii migogoro itokee baada tu ya mke kuingia kwenye hizi familia???Mara nyingi mtu akioa, wanamke anataka yeye tuu ndio apewe atension, kunakuwa na shinikizo la kukata mawasiliano yote hata na familia yake. Hapo ndipo wanawake wanapokosea.
msome SMU
Pia kumbuka kuwa mtu akishaoa anaanzisha familia yake. Majukumu mengi ya familia ni yake yeye kama kichwa cha familia.
Juzi niliwahi kumwuliza kaka mmoja, hivi wewe familia yako ni ipi?
mkeo na watoto au baba,mama,dada,kaka na wengine?
hata mimi kwa sasa familia yangu ni mume wangu na wanangu. Mama na wadogo zangu ni ndugu zangu tu, siwezi wahesabu kama part ya familia yangu
 
Last edited by a moderator:
(kwenye red!), sijui ni kwa nini lakini wanawake wengi mna "chuki" (sipendi kulitumia hilo neno lakini nimekosa neno mbadala) na mama mkwe! wewe mwenyewe ni mwanamke, kwa lugha nyingine utakuwa mkwe wa mtu kwa wakati fulani! mara wifi, dont you have brothers?!! WANAWAKE MNA MATATIZO YENU.
Binafsi sina chuki na mama mkwe wangu, tunaelewana vizuri sana, na kati ya nyumba za wanawe anazopenda kukaa sana ni kwangu.
Kama utanisoma vizuri nimeshangaa tu kwa nini wamama huwa tunasahau kama na sisi tulikuwa wake tu pindi tunapokuwa wakwe. Nina wavulana wawili. Niamini kati ya maombi yangu ya kila siku kwa Mungu ni kunijalia niwapende sana Wake wa wanangu watakapofikia kuoa.
Nina kaka mmoja, mimi ni rafiki sana wa wifi yangu
 
Kwa kweli hapa umeongea jambo la busara. Mtu kubadilika baada ya kuoa ama kuolewa ni kitu cha kawaida, watu wako dynamic.

Mie mwenyewe nahisi naonekana janga kwa ukoo wa watu kwa sababu kuna vitu nimehakiki anabadilika ili kwendana na kasi ya utandawazi. Najua kwa sasa nawakwazaga sana, ila wataelewa baadae sana.

Wana ukoo wanamjua mtoto wao alivyokuwa kabla ya kuoa. Kwa hivyo ni rahisi ku-associate mabadiliko ya tabia ya mtoto wao na mke aliyemuoa. Yapo kwa kweli, lakini pia yapo yasio ya kweli kwenye suala hili. Kwa hivyo ni vigumu kufanya generalisation (for or against).

Lakini cha msingi ni kuwa binaadamu ni dynamic na hivyo kubadilika ni sehemu ya maisha ili kuendana na mazingira na wakati. Kutegemea mtu aendelee ku behave vile vile (kwenye mambo yote) kama ilivyokuwa kabla ya kuoa, naamini sio realistic.

Ndoa zina mambo mengi sana na majukumu yanabadilika/yanaongezeka kadri umri unavyoongezeka. Wengi wetu bado hatujaikubali sana dhana ya "kutoka" kwa wazazi wetu na "kuambatana" na wake zetu. Wengi wetu tumeshindwa "kutoka" au wanaukoo hawataki "tutoke" na ndiyo sababu migogoro na malalamiko kama haya (kati ya ndugu/wazazi na mke) inaendelea kuwepo.
 
Mie I will never keep low, na keep my position basi, mengine inabidi na wao waji-adjust tu to their positions.

Kwa nini niwe mie tu najali nisiwaumize na wao wasijali? Mahusiano yeyote ni pande 2 kuridhiana na ku compromise japo kidogo.

Ukiwa low ndo kabisaaaaaa...................
 
Ni kweli ndugu yangu wanakosa mtu wa kumtupia hivyo inashia kwa wake jamani ni uonevu hujue rafiki
trust me, mambo mengi huwa yanasababishwa na wanaume wenyewe, siyo kwa makusudi ila kwa kukosea tu kama binadamu wa kawaida, lakini lawama zooooteeeee kwa wake zao. Mi naona huwa wanatafuta mnyonge wao
 
Tatizo lenu mnapenda kujitokeza mbele sana Kuonesha nguvu zenu kwa mume..stay low muache mume awe mbele

mie nina mifano kibao ya sisi wanawake kusababisha mitafaruku kwenye hizi familia za upande wa waume zetu, nina ndugu yangu kasambaratisha kabisa hiyo familia ya mumewe, mume mpaka kwenda kumuona mama yake haendi tena, mama kamsema kwa hilo akimwambia au mke wako amekubadilisha ukawa hivi? mbona hukuwa hivi mwanangu? mume alikasirishwa na hilo na mpaka leo hajakanyaga kwa mama yake mzazi, na alienda kumwelezea mkewe na mkewe hata salamu kwa mama hatoi, "wamenuniana" kwa kiwango fulani wake tunasababisha mitafaruku kwenye hizi familia za waume zetu, kwanini wewe uolewe ndio hizo tofauti zianze kuonekana? wape nafasi zao, waishi kama walivyokuwa wanaishi, atunze/hudumie familia yao kama alivyokuwa anafanya, usijitie kimbelembele sana kurekebisha kwa watu wakati labda kwenu yamekushinda, kila familia na iheshiwe kwa pande zote mbili.
 
Kwa kweli hapa umeongea jambo la busara. Mtu kubadilika baada ya kuoa ama kuolewa ni kitu cha kawaida, watu wako dynamic.

Mie mwenyewe nahisi naonekana janga kwa ukoo wa watu kwa sababu kuna vitu nimehakiki anabadilika ili kwendana na kasi ya utandawazi. Najua kwa sasa nawakwazaga sana, ila wataelewa baadae sana.

nadhani kwa wengi tumebadilisha, nikiwepo mie, lakini mie nimembadilisha yeye sio mpaka familia yake, nikiletewa ya kwao natoa ushauri tu akiona poa sawa, akiona afanye ajuavyo poa tu, ili mradi natimiziwa nitakacho na familia yangu mengineyo ya familia yake aendelee nayo tu.
 
Ukiwa low ndo kabisaaaaaa...................

hii kitu ni ngumu aisee, hutakiwi kuwa low, unatakiwa kucheza na gap, kile unachokiona unafanya haki/wema kutoka rohoni kwako kabisa, bila kuonea/kunyanyasa/kusimanga mtu na ukifanye, kikitafsiriwa vibaya hutojali mana umefanya kwa moyo mmoja na huwezi kuendana na mawazo/maoni ya kila mtu, kuna wakati namwambia msukuma kwamba nafanya kila la heri lililopo ndani ya uwezo wangu, likisomeka vibaya sitojali mana "siwezi kumpendeza kila mtu mie sio pesa na siwezi kumchukiza kila mtu mie sio kifo"
 
duh wanawake tunakazi aiseeee

kwa mfano tukija kwenye ishu hii ya kina p2, unaona kabisa ni mwanamke anaeleta mtafaruku kwa hawa vijana, nilisoma blog moja ya naija, kaka mtu hakuhudhuria kwenye sherehe ya mmoja wa wadogo zake coz kaka mtu analalamika kama mama yao angekuwa hai asingemuoa huyo dada, ni kwamba hii ilikuwa toka wakati mama yao yupo hai alijua hapendeki kwenye familia, sasa hivi ataacha kuingia kwa mbwembwe zote wakati anajua kabisa hapendeki?
 
Back
Top Bottom