Kutoka ndani ya moyo wangu

Kutoka ndani ya moyo wangu

ha haaaa, kero za Muungano naona tukiamua zinatekelezeka ila za kwenye ndoa ni kizungumkuti, lol!
watu kila siku wanalia na mengine, yaani wanakatisha tamaa

Ila ndo tumshirikishe, tumtwishe Mungu fadhaa zetu. mimi naamini ndoa ambayo haina Mungu(Yesu) inaweza kuwa mbaya zaidi linapokuja suala la mgongano wa masirahi kulinganisha yenye imani hiyo. huu nao ni mjadala mwingine!!
 
Ni kweli huu ni mjadala mwingine, jitahidi basi utuanzishie........
Ila umesema sawa kabisa, Mungu anatakiwa sana kuwepo katika maisha yetu ya ndoa......
Binadamu tunaanguka, lakini ukiwa na Mungu unajua jinsi gani usimame tena
 
shida watu wa hapa hawapendi sana story za mambo hayo wanataka malavidavi zaidi. tukikutana mtu mmoja mmoja kama hivi ndo tunapeana habari hizi
 
Kabla sijaliongelea hili na-declare interest kuwa mimi ni MKE (WIFE).
Kuna ambao watadhani kuwa huu ni utetezi kwa sababu (huenda) nami nikakumbwa na hiki kimbunga siku moja.
Kutoka ndani ya moyo wangu nachukia sana sentensi kama hizi. Mara nyingi familia zinapoingia kwenye migogoro basi mtu wa kwanza kutupiwa lawama huwa ni mke wa mmoja au zaidi walioingia katika familia hiyo. Na mbaya zaidi mama katika familia hiyo anaweza kuwa mstari wa mbele kushikilia hilo, anasahau kabisa kuwa naye alikuwa mke kwenye hiyo familia. Huwa inasikitisha sana na sijui kwa nini watu wanawaza hivyo.
Napenda niwaeleze ndugu wa waume zetu kuwa sisi (wake) tunatambua umuhimu wa familia za waume zetu kuwa na umoja. Msifikirie kuwa kila kibaya ambacho mume anachokifanya kwa familia basi shinikizo linatoka kwa mkewe. Kuna wake ambao ni Blessings katika familia za waume zao, tusiendelee kuwakwaza kwa maneno kama haya.
Nawatakia uvumilivu wake wenzangu pindi tunaposikia maneno kama haya. Mungu anaona nia zetu NJEMA.
Mubarikiwe sana

Na ukiona mwanamke mwenye akili timamu na anayejitambua anapoamua kuwa "mgomvi" katika familia hiyo jua kuwa kuna kitu amekiona kinachotishia 'uhai' wa ndoa yake. Sikatai wapo wale ambao hutokea tu kuwachukia ndugu wa mumewe (kwa wivu wa kijinga tu). Lakini wapo ambao wanachokozwa kupita mipaka..........
 
ha haaa, kuna siku niliwahi kumwuliza wifi (aliolewa na kakangu) hizi tabia umejifunza wapi?
Nilimfahamu vizuri akiwa gf wa kaka, alipoolewa akawa mtu tofauti kabisa, nilimshangaa sana. Unaanzaje tu kuchukia ndugu wa mume bila sababu?
 
Da Mkubwa binadamu tupo wa aina tofauti sana. Kuna wale waliojaaliwa utashi wa kujitambua na kuzitambua nafasi zao katika jamii mbalimbali.Wengine hujaaliwa kwa kujaliwa tu but wengine kwa kuwa exposed katika mazingira na tashti mbalimbali kama kufundwa, kusoma vitabu vya mahusiano na kadhalika. Sasa unapompata mtu ambaye yeye hatambui nafasi ya ndugu wa mumewe/mkewe kwa mwenzi wake (na bahati mbaya naye akakutana na ndugu hao ambao hawajitambui na kuzielewa nafasi zao kwa ndugu yao aliyeoa/olewa) ndio kivumbi na jasho hutokea. Kama wifi alishaanza kuona mahusiano ya mumewe na nyie yanamtishia either muda wa yeye kukaa na mume, marupurupu ya mishahara ya kaka (hata kama zamani haikuwa inampa shida) na pengine zamani alielewa kabisa kuwa ni wajibu wa kaka yenu... ni wazi kuwa hajajitambua yeye kama mke ana nafasi gani kwa mumewe na nyie au mume ana nafasi gani kwenu. Lakini pia kama na nyie mliendelea kumtreat kaka yenu kama alivyokuwa hajaoa bado ni wazi kuwa hamkuwa mmejitambua nafasi zenu baada ya kaka kuoa ndio maana mkagundua kuwa wifi kabadilika................
 
Kama ukichunguza sana mama wakwe wengi mtoto wao wa kiume akishaoa huwa wanakaa pembeni sana katika maisha yake. Tofauti na zamani kwa sababu wanajua kuwa ni sawa na kuingilia nyumba ya mtu............... ndoa ya mwanao wa kiume ni sawa na nymba ya jirani yako....hata kama unamfahamu na kumpenda vipi akishaoa tu mwanao wa kiume kubali kuziachilia hisia zako nyingine ili mkewe atake care.......... lakini kuna wamama wengine ndio kwanza anahisi kuwa mwanae anateseka, mke hawezi kumlea mwanae, atampa tabu..... ni kweli kuwa mke hatoweza kumtunza kama wewe ulivyo mtunza lakini na wewe kuna ambavyo hukuwezamtimizia ndio maana akaenda utafuta wa kuishi naye. Kubali. Mwe.......
 
Mdogo wangu, mimi nilikuwa na nguvu ya kulitambua na kumwuliza hivyo maana mimi nilitangulia kuolewa miezi michache kabla yake. Nilikuwa naishi mkoa tofauti nao, na sikuwa nategemea lolote toka kwa kaka. Lakini kuna kituko alikitoa siku mimi na mume wangu tulitembelea mkoa waliokuwa wakiishi nilibaki nashangaa tu.
 
ha haaaaa, kama nakuona....... hii counseling nampa mamangu kila siku, maana ana mtoto wa kiume mmoja na anampenda saana, na sasa anakaribia kuoa, basi nakazana naye kumwandaa kisaikolojia asije akatuletea shida bure. sijui siku nikualike uongee naye? maana mimi mwanaye anaona kama namwonea vile, anadhani labda naona wivu maana anampenda sana mwanaye
 
Hahah pole Da Mkubwa basi huyo hakuitambua nafasi ya ndugu za mume kwa mumewe ..... hivi kweli utawezashindana an watu ambao wameishi na mumeo wanamjua toka akilamba makamasi na wewe ulieanza kumfahamu juu juu tu? Kisa, unayajua maungio na kutumia via vyake vya uzazi? Kha! Wanawake wengine tunajitutumuaga bure tu, .......................... Mimi sijabahatika kumpata wifi (wa kuolewa na kaka zangu) lakini hata hao magirlfriend huwa ninawaelewesha kabisa wajue kuwa mie nina mipaka kwa kaka zangu... kuna maeneo ambayo katu hata niyashuhudie yametokea sitatia pua yangu, labda wifi anifuate aniombe mwenyewe.................... ah. kisa cha kuja kuletewa boksa uifue wewe, si matusi hayo? mawifi wenyewe ndo hawa design za kina kantangaze mbona utashaa!!
 
Hahah taratibu Da Mkubwa si wajua tena mtoto kwa mama hakui ye ataona we mwanae tu, utamfundisha nini? Tena juu ya ndoa? ilhali ye ndo alotangulia kuliona jua? HAhah wataka radhi weye,..........
 
La maana ni kila mtu kujua mipaka yake na kuheshimiana...... uwe dada/mama au muolewaji. Kila mtu ana nafasi na umuhimu wake kwa huyo mtu.
 
Hahah taratibu Da Mkubwa si wajua tena mtoto kwa mama hakui ye ataona we mwanae tu, utamfundisha nini? Tena juu ya ndoa? ilhali ye ndo alotangulia kuliona jua? HAhah wataka radhi weye,..........
si unajua mimi ndo dada mkubwa, dad alishatangulia, huyu akija kupata pressure kizaazaa kitanirudia, ndo maana namwandaa kabisa ili asijeona ameibeba dunia kwa kichwa......
 
Back
Top Bottom