Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,153
- 137,160
Duh! Tabu tupu!
mie nina mifano kibao ya sisi wanawake kusababisha mitafaruku kwenye hizi familia za upande wa waume zetu, nina ndugu yangu kasambaratisha kabisa hiyo familia ya mumewe, mume mpaka kwenda kumuona mama yake haendi tena, mama kamsema kwa hilo akimwambia au mke wako amekubadilisha ukawa hivi? mbona hukuwa hivi mwanangu? mume alikasirishwa na hilo na mpaka leo hajakanyaga kwa mama yake mzazi, na alienda kumwelezea mkewe na mkewe hata salamu kwa mama hatoi, "wamenuniana" kwa kiwango fulani wake tunasababisha mitafaruku kwenye hizi familia za waume zetu, kwanini wewe uolewe ndio hizo tofauti zianze kuonekana? wape nafasi zao, waishi kama walivyokuwa wanaishi, atunze/hudumie familia yao kama alivyokuwa anafanya, usijitie kimbelembele sana kurekebisha kwa watu wakati labda kwenu yamekushinda, kila familia na iheshiwe kwa pande zote mbili.

nadhani kwa wengi tumebadilisha, nikiwepo mie, lakini mie nimembadilisha yeye sio mpaka familia yake, nikiletewa ya kwao natoa ushauri tu akiona poa sawa, akiona afanye ajuavyo poa tu, ili mradi natimiziwa nitakacho na familia yangu mengineyo ya familia yake aendelee nayo tu.
Off course na deal na yeye tu.
Of course.
Ha ha , sawa ticha.
Huko kwako vipi? Wifi analeta mtafaruku?
huyo dada anaweza kuwa victim tu, sababu hakubaliki kwenye familia.kwa mfano tukija kwenye ishu hii ya kina p2, unaona kabisa ni mwanamke anaeleta mtafaruku kwa hawa vijana, nilisoma blog moja ya naija, kaka mtu hakuhudhuria kwenye sherehe ya mmoja wa wadogo zake coz kaka mtu analalamika kama mama yao angekuwa hai asingemuoa huyo dada, ni kwamba hii ilikuwa toka wakati mama yao yupo hai alijua hapendeki kwenye familia, sasa hivi ataacha kuingia kwa mbwembwe zote wakati anajua kabisa hapendeki?
tatizo hata ukiwa kwenye your lane watakufwata huko huko.......Nah, she stays in her lane and knows how to play her position.
Dada kubwa karibu!
Mno!
Hii mada hii!
Tukiolewa huwa tunabebeshwa makubwa sana nafkir kuliko uwezo hata ya waliotutangulia kwenye familia hizo
Kwa mfano familia isiyojebgwa kweny misingi ya upendo tu toka wanazaliwa na kulelewa na wazazi wao,kweli akiolewa binti wale ndugu wasipojaliana lawama ni kwa mke?.(hapa naongea kama mke)
.
Halaaaafu mwanaume uliye na misingi yako ya kibaba inakuwaje unakubali kubadilishwa uelekeo wako kwa ndugu zako na mke(hapa naongea kama wifi.)
Kabla sijaliongelea hili na-declare interest kuwa mimi ni MKE (WIFE).
Kuna ambao watadhani kuwa huu ni utetezi kwa sababu (huenda) nami nikakumbwa na hiki kimbunga siku moja.
Kutoka ndani ya moyo wangu nachukia sana sentensi kama hizi. Mara nyingi familia zinapoingia kwenye migogoro basi mtu wa kwanza kutupiwa lawama huwa ni mke wa mmoja au zaidi walioingia katika familia hiyo. Na mbaya zaidi mama katika familia hiyo anaweza kuwa mstari wa mbele kushikilia hilo, anasahau kabisa kuwa naye alikuwa mke kwenye hiyo familia. Huwa inasikitisha sana na sijui kwa nini watu wanawaza hivyo.
Napenda niwaeleze ndugu wa waume zetu kuwa sisi (wake) tunatambua umuhimu wa familia za waume zetu kuwa na umoja. Msifikirie kuwa kila kibaya ambacho mume anachokifanya kwa familia basi shinikizo linatoka kwa mkewe. Kuna wake ambao ni Blessings katika familia za waume zao, tusiendelee kuwakwaza kwa maneno kama haya.
Nawatakia uvumilivu wake wenzangu pindi tunaposikia maneno kama haya. Mungu anaona nia zetu NJEMA.
Mubarikiwe sana
wake hawasababishi mitafaruku Nyamayao mara nyingi wakwe wanasahau kuwa kijana anapooa lazima kuna vitu vitabadilika kama alikuwa akikwama anaomba ushauri kwa babaye au kwa mamaye sasa akioa kapata ubavu hawezi tena kukimbilia huko lazima akikwama aanzie kwa mkewe na hapo wakwe hawakubali huu ukweli kuwa sasa wao ni chaguo la pili
Ni vizuri unaelewa kuwa una mke mwema. Ni jukumu lako kumlinda na hao ndugu.
Juzi kati kulitokea kisanga fulani kutoka kwenye familia iliyo karibu sana na sisi. Mke tunamfahamu kwa karibu sana, na mume pia. Mambo mengi huwa yanasababishwa na mume na sisi huwa tunakaa sana na huyo kaka kuongea naye. lakini cha ajabu, shutuma na matusi yoote toka kwenye familia ya mume yalielekezwa kwa mke.
Off course na deal na yeye tu. Ila kuna mambo mengine ukimbadili mtu, moja kwa moja unawagusa wengine, mfano budgeting malengo ya kila mwaka.
Kuna saa inabidi tu, no way out.
huyo dada anaweza kuwa victim tu, sababu hakubaliki kwenye familia.
Inawezekana kabisa huyo dada kaolewa na kuwa ndani kama mke ambaye hapendwi, lakini hana mchango wowote kwenye ugomvi wa wanandugu. Kaka hampendi shem, mume anampenda, chochote kitakachofanywa na nduguye itasemwa ni sababu mke hapendeki....... ni kizaazaa.
Mdogo wangu asante sana.....Dada kubwa karibu!
Mno!
Hii mada hii!
Tukiolewa huwa tunabebeshwa makubwa sana nafkir kuliko uwezo hata ya waliotutangulia kwenye familia hizo
Kwa mfano familia isiyojebgwa kweny misingi ya upendo tu toka wanazaliwa na kulelewa na wazazi wao,kweli akiolewa binti wale ndugu wasipojaliana lawama ni kwa mke?.(hapa naongea kama mke)
.
Halaaaafu mwanaume uliye na misingi yako ya kibaba inakuwaje unakubali kubadilishwa uelekeo wako kwa ndugu zako na mke(hapa naongea kama wifi.)
ila sasa zamani hizo walikuwa wanashindwa kulaumiana, sasa wanakuwa wamepata mchawi wa kumsingiziaHa ha ha ha, unamaanisha familia inakuwa ilishasambaratika hata kabla ya mke kuolewa? Hii ina ukweli bana.
Mmiliki ndo nani? kuna mmiliki wa mtu?...hii yote inatokana na dhana ya kwamba nani ana haki zaidi juu yako (Mume)...
1. Mama mzazi anajiona yeye kalea mimba, amezaa na kuteseka na ulezi wa kichanga mpaka kufikia kutembea, kusema na mwishowe kujitegemea...
2. Madada (Mawifi) hawa huona wao ni ndugu toka nitoke....wamezaliwa tumbo moja na ndugu yao, wanajihisi wanauchungu wa damu kuliko weye Mke mtu baki tu ambaye hata ukiachika ataolewa mwingine...
3. Mke, ....huyu anajiona yeye ndiye aliyechaguliwa kuwa mama wa watoto wa huyo Bwana Mkubwa, Mwenza na mengineyo mengi yakiwemo faragha faraghani....!
Ni ubinafsi na "wivu" wa kijinga tu ambao wanawake wengi wamejaaliwa nao!
watu kutojua mipaka yao.
Au mnasemaje Dark City swahiba,.. King'asti, AshaDii, MwanajamiiOne, TIMING, et al?