kwani imekuwaje asitangaze saa nne kama tulivyo taarifiwa awali au kajangwani?Baraza la mawaziri litatangazwa muda wa saa tisa mchana leo hii( kwa saa za Tanzania)..Kawaida huwa linatangazwa muda huo
kutokana na tatizo la umeme ktk maeneo mengi jijini dar, naomba wadau mpost hapa jf mara baraza litakapotangazwa, maana hapa nilipo umeme toka jana saa 4 hadi sasa saa 5 asubuhi bado haujarudi, sasa wadau mtujulishe hilo baraza litakapokuwa limetangazwa, naomba kuwasilisha kwenu.
Saa 10:00am, toka viwanja vya Ikulu, DSM.
kutokana na tatizo la umeme ktk maeneo mengi jijini dar, naomba wadau mpost hapa jf mara baraza litakapotangazwa, maana hapa nilipo umeme toka jana saa 4 hadi sasa saa 5 asubuhi bado haujarudi, sasa wadau mtujulishe hilo baraza litakapokuwa limetangazwa, naomba kuwasilisha kwenu.
Kwani CUF nao ni impurity.......??? Upinzani si CDM pekee, kuna TLP vile vileMkuu Invisible, hii ni ndoto kwa CCM kuruhusu foreign impurities kuingia kwenye mtandao wao!!! Hakuna jipya, sana sana ataongeza idadi ya wanawake na kujisifia.
Anyways, tusubiri.
Labda upo kwenye LINE ya JESHIUmeme umeme,mara dawasco mnakaa dar gani! Mbona kwangu masaki mgao wa umeme ni hadithi.
Huwa najiuliza kila siku hii ofisi iliyotoa hii taarifa ni:
a. Ofisi ya Mawasiliano ya Rais - Presidential Communication Office - private and public????
b. Ofisi ya Mawasiliano ya Ikulu - Statehouse Office of Communication
c. Ofisi ya Habari ya Ikulu - Statehouse Public Information Office
d. Ofisi ya Habari za Rais - Office of Presidential News
Kwa ufupi ni ofisi ya mawasiliano au ya habari?
Hakuna jipya hapa kama sikosei kumbukumbu zangu zinaonyesha alishawahi kuishika hiyo Wizara.
Baada ya kukataa kwa muda sasa kutokana na ushauri aliyokuwa anapewa na rafiki zake wakiongonzwa na Seleli aliyesafiri toka Dar kwenda Dodoma kumwambia Sitta asikubali kupewa uwaziri, sasa dhamana ameikubali na kupuuza maneno ya marafiki. Ndiye Waziri wa SHERIA NA KATIBA. Nakutakia kila la kheri na uongoze kwa haki na si majungu.