Kutoka Ikulu: Baraza la Mawaziri kutangazwa J'tano (kesho)

Status
Not open for further replies.
mkwere kaingia na keshakaa kwenye kiti na kuwauliza hali "habari ya saa hizi jamani"

sasa anataka waandishi waandike habari zenyewe maana wameandika habari nyingi za uongo
 
anazungumzia kuhusu mabadiliko ya baraza lake na anakusudia kuwa idara ya umwagiliaji kuwa imerudi wizara ya kilimo wakati mwanzo ilikua wizara ya maji

hapa anatoa sababu zilizopelekea mabadiliko hayo
 
Mods unganisha hizi thread zitatutesa kufuatilia, si unajua tena taifa lazima lijengwe, na sisi tumo maofisini.
 
Huyu Mheshimiwa toka enzi ya mwalimu anazunguka kutoka shirika moja kwenda jingine na wizara hivyo hivyo.Nitajie hayo maendeleo aliyoyaleta ktk kila sehemu aliyowahi kufanya kazi ktk utumishi wa uma kuanzia Mkurugenzi wa CDA,Kituo cha uwekezaji na hata hiyo wizara inayosadikika amepewa alishawahi kuiongoza,(hizo ni sehemu chache tu)ktk kipindi zaidi ya miaka 20 kwenye nafasi za juu?Uwezo wa kujenga hoja ni kweli anao lkn kwenye hilo baraza unategemea alete hoja ya katiba mpya wakati akiwa spika hakuona hata umuhimu wa hilo kwa kuruhusu hata hoja ya upinzani ijadiliwe.Hawa wazee inafika wakati wapumzike na wawachie watu wengine wenye mawazo mapya si Kwa Sitta na wengine wote ambao wamekaa muda mrefu kwenye nafasi za juu na bila athari chanya za utendaji wao ukilinganishwa na miaka ya utendaji wao ktk utumishi wa uma.Kwenye Bunge ndiyo alijitahidi kwa kuuma na kupulizia na hiyo ilikuwa mara nyingine ni kwa maslahi yake.Angalia ubadhirifu aliyoufanya wa kujenga ofisi ya spika jimboni na uspika ukaota mbawa?Je hayo ndiyo maendeleo hicho kiasi kingeingizwa kwenye huduma za kimaendeleo ya jamii na wananchi wengi wakafaidika si ingekuwa jambo la busara zaidi?Kama tunaamua kuchagua mabadiliko basi tupige vita hizi recycle type of leadership.......!

Mzee, si miaka 20+ tu ni 30+!!!

Huyu jamaa wakati naliza form four 1987 alikuwa ni mkuu wa mkoa wa Iringa. Hiyo ni miaka 24 iliyopita . Na kabla ya hapo alishakuwa kwenye ulaji tu kipindi!!
 
Kwa timu hii ya mheshimiwa miaka mitano ijayo ni machozi tu. Haya watanzania majuto ni mjukuu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom