Kutoka Ikulu: Baraza la Mawaziri kutangazwa J'tano (kesho)

Status
Not open for further replies.
Wanahabari wako Ikulu tangu saa 4:00 asubuhi hii, rais anamalizia kujiangalia kwenye TBC ndipo atoke nje kuja kuitangaza listi yake.
 
baraza lina wafuatao:
Lowasa mambo ya nje
Sita mambo ya ndani
Ngeleja madini
Tibaijuka Ardhi na maendeleo ya makazi
Nahodha- Masuala ya muungano

hizo ndo nimeweza kudodosa!!
Mkuu Vp kwani? Mkwere alidondosha Karatasi na umeiokota wewe nini? Ndo maana anashindwa kutangaza.
 
Wanahabari wako Ikulu tangu saa 4:00 asubuhi hii, rais anamalizia kujiangalia kwenye TBC ndipo atoke nje kuja kuitangaza listi yake.

Kuna kipindi kuhusu JK TBC sasa?

Hivi wanategemea taifa litajengwa vipi na huku watu hawajali ku keep time?
 
Kaka hapo unakosea watu hubadirika Sitta sasa ktk CCM ndiye tunamwona wadilifu na anafuata nyayo za baba wa Taifa hivyo ni bora tuombe mungu tetesi hizi ziwe za kweli kwakuwa Sitta anauwezo wa kujenga hoja ya kubadili katiba na mambo mengi yaliyopitwa na wakati kurekebishwa ila sidhani kama CCM inaweza fanya kosa hilo la kumpa sitta wizara hiyo kwakuwa hata NEC anaweza kuiboresha

Sitta ni mwadilifu na mpenda maendeleo ya nchi yetu na watu wake pia ni mjamaa wa kweli mimi nampenda sitta kuendelea kuwa kiongozi wa kitaifa bila kujali anapitia chama gani kwakuwa Sitta ni Mzalendo na mawazo na matakwa yake yako juu ya hila za chama chake chenye mlengo wa kizandiki
Huyu Mheshimiwa toka enzi ya mwalimu anazunguka kutoka shirika moja kwenda jingine na wizara hivyo hivyo.Nitajie hayo maendeleo aliyoyaleta ktk kila sehemu aliyowahi kufanya kazi ktk utumishi wa uma kuanzia Mkurugenzi wa CDA,Kituo cha uwekezaji na hata hiyo wizara inayosadikika amepewa alishawahi kuiongoza,(hizo ni sehemu chache tu)ktk kipindi zaidi ya miaka 20 kwenye nafasi za juu?Uwezo wa kujenga hoja ni kweli anao lkn kwenye hilo baraza unategemea alete hoja ya katiba mpya wakati akiwa spika hakuona hata umuhimu wa hilo kwa kuruhusu hata hoja ya upinzani ijadiliwe.Hawa wazee inafika wakati wapumzike na wawachie watu wengine wenye mawazo mapya si Kwa Sitta na wengine wote ambao wamekaa muda mrefu kwenye nafasi za juu na bila athari chanya za utendaji wao ukilinganishwa na miaka ya utendaji wao ktk utumishi wa uma.Kwenye Bunge ndiyo alijitahidi kwa kuuma na kupulizia na hiyo ilikuwa mara nyingine ni kwa maslahi yake.Angalia ubadhirifu aliyoufanya wa kujenga ofisi ya spika jimboni na uspika ukaota mbawa?Je hayo ndiyo maendeleo hicho kiasi kingeingizwa kwenye huduma za kimaendeleo ya jamii na wananchi wengi wakafaidika si ingekuwa jambo la busara zaidi?Kama tunaamua kuchagua mabadiliko basi tupige vita hizi recycle type of leadership.......!
 
Uwezekano wa jipya kuwepo ni mkubwa... Najua wengine mtashtuka ikitokea mtu wa kambi ya upinzani ataingia katika baraza jipya

Kuna utaratibu wowote unaomruhusu kuteua watu kutoka opposition kuwa mawaziri? utaratibu wa Chama ukoje? anateua kwa utashi wake au kwa kufuata mwongozo cha chama wa kuteua mawaziri na watu kwenye nyadhifa nyingine?
 
Kama mkuu bado anajiangalia kwenye TBC, wanahabari waliopo hapo Ikulu wanafanya nini? Au wamepewa kahawa wajburudishe na rasilimali zetu wadanganyika?

Si waondoke wakatafute habari zenye tija zaidi kwa watanzania?
 
Anaogopa nina kutangaza? Au amechakachua sasa anaogopa maswali baadaye? Nasikia anaandika jina mara anafuta sijui ndiyo nini.
 
Redio na tv sasa ziko live from ikulu but jamaa mkwere hajatokea
 
tic toc... Lowassa apotezwe Mh Waziri Mkuu aliye jichakachua kwa kutumia chujio la richmonduli
 
Pinda na Bilal wameingia kwenye ukumbi


bado mkwere anajipanga na kutuacha watanzania tumbo joto
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom