Kutoka Dodoma!

....wazee JF NI SUPER ....HUTAAMINI UWT.....NYETI NYINGINE AMBAZO WALISTAHILI WAAZE KUZIPATA WAO KWANZA .....WANATANGULIA KUZIONA HAPA.....SI AJABU KILA SIKU JK ANAPAYUKA KWENYE CORRIDOR ZA IKULU....AKISHANGAA KWA NINI NYETI ZINAFIKA HAPA KWANZA!!!!

...JAMANI JF NI KIMBUNGA CHA TSUNAMI...USIPIME !!!!..UKINGANGANIA UTASOMBWA...WE!
 
Habari ambazo tumezipata kutoka kwenye TBC1; ambazo Katibu Mwenezi wa CCM ameonyeswa amezielezea ni kwamba... hilo jambop limejadiliwa kwenye kikao cha NEC. hata hivyo Katibu huyo mwenezi amesema... wanasubiria vyombo vya usalama viseme what happened... maana ndivyo vyenye authority!

Na maelezo ni kwamba huyo Mbunge ambaye sasa anatoka viti vya mbele vile vya mawaziri... na sasa anatakiwa kupatiwa kiti kingine kule back bencha alikuwa akipitishwa na wahudumu wa ofisi za bunge kuonyeshwa kwenye kikao hiki akae kiti gani...

Kwa maana hiyo basi ni jambo la kawaida kutafuta kiti... unalazimika kupitia kwenye safu mbalimbali na kuangalia kiti au sehemu ambayo ni muafaka kwako..


Kwa hili inaonyesha dataz za JF zimefungwa 3-0
 
Habari kutoka katika vyanzo vyetu zilieleza kwamba watuhumiwa hao wameanza mkakati wa kupoteza ushidi kwa kushirikiana na baadhi wachunguzi wa suala hilo.

"Mmoja wa Ofisa ambaye anatoka katika chombo nyeti ameanza kutaka kumsaidia mtuhumiwa yule kwa kutuambia kwamba hakuna kitu kama hicho, sasa sisi tunajiuliza yeye amepewa jukumu la kuchunguza suala hili sasa inakuaje anatangaza kwamba si kweli wakati uchunguzi haujakamilika?,"alihoji mmoja wa Wabunge.

Tanznia tuna kazi sana, ufisadi mpaka kwenye sehemu nyeti, kazi ipo!!!!!!!!!!!!!!!!!
 

hapo patamu naona wanataka kuuuza soo kimya kimya....sasa Sitta alikiri kupata taarifa za kuwa mbunge huyo KANYUNYIZIA dawa zikoje hizi.Na hao UWT na Polisi wana taarifa zipi? KUNYUNYIZIA TUNGULI AU KUONYESHWA KITI?
 

Penye ukweli uongo utajitenga!yangu macho!MUNGU yupo
 

Kwa kifupi unachosema ni kwamba jamaa hana control na serikali anayoiongoza. Kama hivi ndivyo, ni aibu kubwa, tena Afrika ambapo marais ni kama miungu ya nchi zao!
 

Nakubali hapa tumeshapigwa bao as usual. Niliwaambia hawa jamaa watakubaliana yaishe kwa maslahi ya chama. Si ajabu ilikuwa ni mipango ya kikundi kizito. Hata hivyo so far hatujui ni kitu gani kimefanyika maana vyombo vya habari bado vina uma na kupuuliza. Hawaandika habari mpaka wapewe go ahead, again aibu!!
 
hapo patamu naona wanataka kuuuza soo kimya kimya....sasa Sitta alikiri kupata taarifa za kuwa mbunge huyo KANYUNYIZIA dawa zikoje hizi.Na hao UWT na Polisi wana taarifa zipi? KUNYUNYIZIA TUNGULI AU KUONYESHWA KITI?

Please... be serious... mzee Six hakuwahi kuhakikisha kitu chochote!!!...ameendelea kusema ameambiwa kuna kitu kama hiki... lakini bado vyombo husika vita-prove...

Please do not pre-empty anything... hakuna ambalo liko wazi hadi sasa!!!

Everything pending evidence and confirmation from Police Force and/or UWT...

Ieleweke wazi kwamba Mzee Six, hawezi kutenda haki... kwa hili kwa kuwa hizo TETESI zimemuhisha yeye kama mlengwa...

Huenda hata sasa anaota ndoto mbaya usiku...
 
Chiligati amekiri sasa hivi kuwa aliyeingia Bungeni ni Chenge ingawa hakumtaja kwa jina. Alichosema ni kuwa mbunge mmoja, ambaye alikuwa waziri lakini ameondoka katika wadhifa huo, aliingia bungeni kwa lengo la kutafuta kiti cha kukaa kwa sababu hivi sasa hawezi tena kukaa kwqenye kiti alichokuwa anakaa wakati alipokuwa waziri.
Ukijumlisha 1+2 haupati 12, ni 3 kwani mbunge ambaye ameachia ngazi ya uwaziri hivi karibuni ni andrea pekee. na ndiye ambaye anaopasw akutafuta kiti cha kukalia hivi sasa.
Lakini Chilly boy amekanusha kabisa kwamba mheshimiwa huyu alimwaga uchwi wakati alipokuwa ndani ya Bunge, ingawa amesema kuwa alipita kwenye viti kadhaa, akichungulia vile vinandiko vya majina ya wabunge, ili kuona kiti kilicho wazi ili kesho aje akae.

MY TAKE: Kwa nini asumbuke kutafuta kiti cha kukaa usiku wakati kazi hiyo ingeweza kufanyika kwa dakika chini ya tano tu kesho yake?
 


Wallahi!..I love the diplomacy going on in JF!!
THOSE HARD QUESTIONS..MHHHH!!nani anaulizwa..nani anajibu??
 
Mkuu FM hongera tena, taarifa zilizopenyezwa kwangu hivi punde kutoka ndani ya kikao zinathibitisha yale yote uliyokuwa unatumwagia hapa. Nimeelezwa kuwa hali ilikuwa ngumu ndani ya kikao zilipoibuka pande mbili ambazo muungwana ameshaona zinakigawa chama.
wapo wabunge ambao waliamua kuwatolea uvivu akiwa EL na kundi lake ingawa mzee Monduli naye alisimama kidete kujitetea kuwa alishapendekeza mara mbili mkataba wa Richmond uvunjwe lakini alikataliwa.
lakini walibanwa sana liasi kwamba kimsingi chama kimekubaliana kuwatimua wale waote watakaobainika kuhisika katiak Richmond na EPA. wanasubiri ripoti ya Pinda kuhusu richmond na mwanyika alete yake ya EPSA watu wamwagwe rasmi
 

Mzee Kitila,

Mimi nakuaminia kama mtu makini sana... mbona inaonyesha kama ulikuwa unajua yanayoendelea upande... mmoja na hivyo hizi habari zingine unaziona si za Kweli?

Kwa data zilizotolewa na the so called ... "Wenye Dataz" na hizi za Katibu Mwenezi wa CCM...

Mimi naona zote zina-logic fulani... tofauti tu ni kwamba za wale wa the Dataz... hawana full access.. kama za Katibu Mwenezi wa CCM...

Hivyo... sidhani kama tumefanyiwa usainii... inawezekana "wenye dataz" ndio walikuwa wanaota... ndoto za mchana...
 
KITENDO KILICHOFANYIKA HAKIKUBALIKI kama watashindwa kugundua ni nani basi kutakuwa hakuna haja ya kuweka walinzi hapo na wanaohusika na suala hilo la ulinzi wote wafikishwe mahakamani.Na hizo Cam kama haziruhusiwi kuzimwa basi aliekuwepo zamu siku hiyo akamatwe shati na kuvutwa ukosi alipata wapi ruhusa za kuzima >?< hii inaelekea sio kasheshe ndogo.
Ila tatizo naliona kilichokwenda kufanyika humo ndani ndio mzizi ambao inabidi upatikane bila kuharibiwa, kama hakuna kemiko na sababu ya watu hao kuingia kwenye ukumbi na kukwanga , hao si viongozi bali ni mafisadi ambayo sasa wanazitafuta feza kwa njia za giza ,waondolewe haraka katika safu ya uongozi na wafukuzwe kwenye Chama chao ni aibu kubwa ambayo kuvumiliwa kwake kutakiathiri chama ambacho kimeshaanza kumeguka kwa kuwemo kwa makundi mbali mbali na sasa hili kundi la washirikina.
 

..uongo huu wa kitoto ndio unaozusha maswali mengi, kuliko kujibu maswali mengi.
 


Kama sikosei unayemzungumzia hapa ni mkuu wa zamani wa idara.......huyu mkuu amejilimbikizia mali na fedha nyingi sana na nina uhakika atajaribu kila awezalo kujaribu kujilinda na hao maharamia wenzake...

Lakini tatizo la hawa jamaa hizi 'coalition za convience' huwa hazidumu...kama inavyosemwa umoja wa wachawi...haudumu....I guess this can now be taken literally!

As for wao kumuona JK ni problem...I think its safe to say that fateful day is almost here...unless he wakes up and take care of them before they 'fix him'!
 
..uongo huu wa kitoto ndio unaozusha maswali mengi, kuliko kujibu maswali mengi.

Tuambie kwa nini ni uongo? ukweli ni upi brother?... mimi hadi page ya 26 sijauona... zaidi ya mahisia kibao...

Habari ambazo zinashabihiana ni muhusika kwenye source zote mbili ni huyo huyo!!!

Ambacho hatukijui ni

Kumwagwa kwa unga
au Kuonyeshwa kiti cha kukaa!!!


Sasa mkuu wewe unayejua ukweli tuambie...
 

".....Muongo na Mulozi ni watu wa kuchomwa......" by Franco Luambo Makiadi & OK-Jazz
 

Hivi utaratibu wa kupata viti Bungeni upoje? mimi nikuwa nadhani kwamba wahudumu wa Bunge ndiyo wanaopanga nani akae wapi. Ikiwa Mbunge mwenyewe anatafuta kiti basi si utaratibu mzuri. Hivi Chenge alikuwa hajaingia Bungeni tangu ajiuzuri uwaziri? Ingekuwa na hivyo kungekuwa na haja gani ya kuficha jina na kupeleka kideo kwa RPC na UWT? uummh Chiligati anapiga diplomasia hapo.
 


Okey sawa, ila sasa kwanini Camera za Usalama ziwe zimezimwa? Na kwenye Kiti cha Spika alifuata nini? Na kwanini iwe muda mbali na shughuli za bunge? Acheni msitutoe kwenye RELI hapa. Wewe unafikiri bila kuletwa JF hapa mapema Serikali wangesema nini kinaendelea?

JF bado tunaongoza 3-0 na mpira umekwisha.
 
Sasa mkuu wewe unayejua ukweli tuambie...

..kwanza,ukweli siujui.kwani ripoti ishatoka?. kuufahamu uongo si lazima uujue ukweli, kwanza.

..pili,mi siwezi kukuambia weye na hao wenzako,si tayari mnajua kila kitu ndo maana mnasema habari hizi ni uzushi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…