Kutendwa kumenifanya nisijielewe

Kutendwa kumenifanya nisijielewe

Hivi hapa muafaka ulipatikanaje.......?..... Valentina hebu njoo hapa utupe mlishonyuma..............
 
Last edited by a moderator:
WEWE UNAONYESHA UNAMPENDA JAMAA. HAPA umekuja ili kuhalalisha unachotaka kufanya kwa kupata watu wanaokuunga mkono. mtazamo binafsi ni huu tu. huna haja ya kulalamika kuumizwana hata ukisema haitusaidii sisi maana hatujui sababu zilizomfanya mtu akabadilisha mawazo na kuumizwa ni kukua kwenye mahusiano. pia ipo kasumba ya mwanamke akitolewa udada wake anaona kama kitu cha ajabu. kwa uzoefu wa wengi wanawake wanakuwa ndo wametolewa huwa wanaboa kwenye mapenzi maana huhitaji kufundishwa Zaidi. na karibu kila mtu huwa ana magumu yake kwenye mahusiano na anaumiaga kivyake.
pia inawezekana kuna tabia aliziona kwako jamaa ambazo hazikumshawishi kukuoa. sasa amezunguka na mejiridhisha kuwa wewe una afadhari kuliko wengine na nina Imani kama roho yake haijaoza atakuwa amejifunza vya kutosha. huna haja ya kuomba ushauri kama unampenda. sikiliza moyo wako na jifunze kusamehe ukijua kabisa wanaume kwa wanawake ni wadhaifu ingawa haimaanishi hawapendi wake zao.piausiwe mtu wa kukata tamaa mapema.wengine ni wazuri kwa sababu huwafahamu ila nyumba zinaficha mengi
pia kaa na jamaa na umuulize shida ilikuwa nini na kwanini anarudi kwako sasa. suluhisho sio kumwachia mwenzako ila ni kupigana kama yakobo upate chako kama una uhakika nacho. pia jiangalie na wewe kama papoulipokosea.ishu inavyooneka hata wewe umeshabadilisha wengi na bado hujielewi. bora urudi unakojielewa kwa jamaa
mimi nikigundua mauza uza na makonda kond na mawasiri wasiri hata kama harusi ni kesho naahirisha kwa kumlowasa tu. kwa wakristo kuvunja uchumba sio kosa ila ndoa ikifungwa ni ngumu sana kuivunja isipokuwa kwa uzinzi tu au uanze kumuombea mwenzako afe au mtengane na kila mtu asioe wala kutafuta mwingine. narudia tena ndo sio darura.
 
usithubutu kumrudia dada psee naakuomba,atakuona dhaifu sana kwake. we mpotezee tenaa mblock kila mahali hana adabu mshenzi wa ngozi uyo.
 
Wapendwa ni matumaini yangu mpo wazima na mko vizuri katika majukumu yenu

Leo ninaomba kushare nanyi jambo ambalo limekua likinitatiza kwa muda sasa. Ninatambua kila mmoja wetu ana historia yake ya kimapenzi na wengi tumetendwa na wale ambao tuliwekeza mioyo yetu kwao kwa kuwaamini kwamba wataiendeleza furaha yetu, ila kwasababu mbalimbali au kwa bahati mbaya wengi hatukuweza kufikia matarajio yetu juu ya hao wenzetu.

Binafsi nilikua katika mahusiano na mtu ambae nilimpenda mno narudia tena nilimpenda tena mno. Na ndie mwanaume wangu wa kwanza kukutana nae kimwili.

Naye kwa upande wake alionyesha uaminifu na moyo wakujali,maneno yote mazuri yenye matumaini mtoto wa kike niliambiwa, kifupi tulipanga uhusiano wetu uzae ndoa.

Ilifika hatua mwezi wa sita mwaka jana akaja Arusha kwalengo la kujitambulisha nyumbani kwetu. Lakini ghafla katika hali ambayo sikuitarajia akabadilisha maamuzi yake akanipa visingizio.

Baada ya muda mfupi kabla ya yeye kurejea kwenye makazi yake, nikamfumania akiwa na rafiki yangu wa karibu, rafiki niliye mchukulia kama ndugu yangu na kushare nae baadhi ya mambo.

Waliosalitiwa bila shaka wanaelewa uzito wa maumivu hayo. Ikabidi niwe mpole,na kuwaambia waendelee mbele,siku zilivosonga yule binti akaanza mambo ya dharau kwangu ila namshkuru Mungu nilipata moyo wa kumsamehe na kupuuza dharau zake.

Ilipofika mwezi wa 9 yule binti aliacha kazi kwa shari na kurudi kwao.

Sasa kilichonifanya nije hapa mbele yenu leo, nikwamba yule mwanaume anataka kurudi kwangu na mimi moyo wangu unakua mzito kumrudia, nimetokea kumchukia.

Jambo linalonisumbua zaidi kila ninapoanza mahusiano mapya hua nashindwa kuendelea mbele, hofu ya kwamba huyu atanifanyia kama yule inanijia mara kwa mara na matokeo yake nakua sababu ya kuvunjika uhusiano huo.

Wapendwa nifanye nini kukabiliana na hali hii ya pili? Ninatamani sana hali hii iniondoke. Karibu kwa mchango wako kimawazo.
Kwenye makosa ya kiuandishi mnisamehe maana natumia simu.

pole mamii.. bn there pass tht. I understand unachopitia. pray, forgive, lia ukijiskia try to be busy listen to musicd.. it helps sometimes!
 
kisichokuua kinakukomaza....sjui kivipi ila yataisha tu na maisha yataendelea:confused2:
 
Daah Preta long time nshamsahau jamaa kumoyo. Hata bila uwepo wake kwangu maisha lazima yaendelee. Ushauri wa wengi humu ulinitia nguvu sana ya kusonga mbele. Asanteni sana
 
Last edited by a moderator:
namna gani ulianzisha uhusiano uliovunjiaka na unaanzaje mpya, apo lazima ujipe muda ili ujitadhimini kiundani inaonekana wewe malengo yako ndoa lakini unakutana na watu wanaotaka kula alafu basi
 
Maneno ya wahenga yana maana yake, huu msemo wa "yaliyopita si ndwele tugange yajayo," ndiyo inabidi ufuate. Yaani piga moyo konde na achana kabisa na propaganda za huyo jamaa aliyekusaliti mwanzoni kwani hakuwa na nia nzuri nawe, take it easy na do not rush kuwa katika mahusiano ya haraka eti kwa kuwa unahisi uko lonely, utajiua as guys will take advantage of your situation. Take it day by day na ukubali kuwa majinamizi ya mapenzi si kwa wanaume tu hata wanawake wako hivyo. Jipe moyo na umpe mashaka jamaa yako mpya, usijitolee nafsi yako moja kwa moja kwake. Time na kujiamini will heal you, believe me.
 
Aha haaa haaa ... muda umepita sasa na nimatumaini umeshampata tabibu! Kubwa MUNGU awape uvumilivu na upendo wa hali ya juu, pia awalindie uhusiano wenu ...
 
Valentina, kama uliweza kumuacha aende angali bado unampenda amini kabisa unaweza kuanzisha mahusiano mapya na ykazaa matunda mema kabisa.. shukur umamtambua hyo jamaa na tabia yke ya usaliti.. cha muhimu ni kjiamin tu.... ckwambii ucrud kwa hyo jamaa ila kama ingekuwa Mimi ningejikaza na maisha yngesonga mbele.. kisa cha kuukosesha uso wko tabasamu na kuish bila amani.. chkua htua mwanadada..!
 
^^
Kwanza, sikushauri urudiane na huyo mwanaume, katika maisha yangu nimejifunza kuwa wanaume wengi wanaowarudia wenzi wao si kwa nia ya kuimarisha mahusiano! Naongea hivi nikijifanya kipofu wa jinsi wanawake msivyo na misimamo (si ajabu mkarudiana)
Pili,
Jifunze kuishi maisha mapya! Mchezo wa kutofuatilia mahusiano mwanzo mpaka mwisho utakugharimu sana hasa kama mwanamke! Tazama magumu uliyopitia kama funzo la kumtunza na kulipwa hisani kwa uliyotendewa nyuma.
Usiifunge milango mipya mpaka itakapokupa sababu ya kufanya hivyo
Tatu
Simama imara! Huna haja ya kulia tena
^^
nimependa ushauri wako mkuu.

BTW wengi tunaumizwa kwa kutosimama imara, Mungu hakutuumba ili tuje tulie bali kumtukuza kwa kila sekunde anayotupa nafasi kuishi hapa duniani. Binafsi nimetokea kumchukia huyo rafiki yake wa karibu maana yeye haswa ndo chanzo cha maumivu ya Valentina.

Nikushauri piga moyo konde na chonde chonde usimrudie tena maana huwez jua Mungu alikuwa anakuepusha nini. cha msingi piga goti kwa Mungu na umsihi akupe mwanaume wako wa maisha na pili huna sababu ya kuyafikiria uliyotendewa ukiwa na new rltn.
Kuna msemo waswahili husema wanaume wote ni sawa wamezaliwa na mama mmoja mimi nakataa kabisa, wanaume wanatofautina na kamwe usiweke akilin mwako kuwa utatendwa kila siku. Kumbuka Mungu anakupenda sana na hawezi kamwe kukubali upitie tena magumu uliyopitia kama unamtegemea.

Tena wakati mwingine Mungu huruhusu mapito ili uwe imara zaidi.

nikutakie maisha mema na Mungu awe nawe katika relation ambayo unayo au unayotegemea kuinza.
 
Wapendwa ni matumaini yangu mpo wazima na mko vizuri katika majukumu yenu

Leo ninaomba kushare nanyi jambo ambalo limekua likinitatiza kwa muda sasa. Ninatambua kila mmoja wetu ana historia yake ya kimapenzi na wengi tumetendwa na wale ambao tuliwekeza mioyo yetu kwao kwa kuwaamini kwamba wataiendeleza furaha yetu, ila kwasababu mbalimbali au kwa bahati mbaya wengi hatukuweza kufikia matarajio yetu juu ya hao wenzetu.

Binafsi nilikua katika mahusiano na mtu ambae nilimpenda mno narudia tena nilimpenda tena mno. Na ndie mwanaume wangu wa kwanza kukutana nae kimwili.

Naye kwa upande wake alionyesha uaminifu na moyo wakujali,maneno yote mazuri yenye matumaini mtoto wa kike niliambiwa, kifupi tulipanga uhusiano wetu uzae ndoa.

Ilifika hatua mwezi wa sita mwaka jana akaja Arusha kwalengo la kujitambulisha nyumbani kwetu. Lakini ghafla katika hali ambayo sikuitarajia akabadilisha maamuzi yake akanipa visingizio.

Baada ya muda mfupi kabla ya yeye kurejea kwenye makazi yake, nikamfumania akiwa na rafiki yangu wa karibu, rafiki niliye mchukulia kama ndugu yangu na kushare nae baadhi ya mambo.

Waliosalitiwa bila shaka wanaelewa uzito wa maumivu hayo. Ikabidi niwe mpole,na kuwaambia waendelee mbele,siku zilivosonga yule binti akaanza mambo ya dharau kwangu ila namshkuru Mungu nilipata moyo wa kumsamehe na kupuuza dharau zake.

Ilipofika mwezi wa 9 yule binti aliacha kazi kwa shari na kurudi kwao.

Sasa kilichonifanya nije hapa mbele yenu leo, nikwamba yule mwanaume anataka kurudi kwangu na mimi moyo wangu unakua mzito kumrudia, nimetokea kumchukia.

Jambo linalonisumbua zaidi kila ninapoanza mahusiano mapya hua nashindwa kuendelea mbele, hofu ya kwamba huyu atanifanyia kama yule inanijia mara kwa mara na matokeo yake nakua sababu ya kuvunjika uhusiano huo.

Wapendwa nifanye nini kukabiliana na hali hii ya pili? Ninatamani sana hali hii iniondoke. Karibu kwa mchango wako kimawazo.
Kwenye makosa ya kiuandishi mnisamehe maana natumia simu.
Maamuzi ya hilo ni rahisi kama kweli uko serious na ulichoandika,nayo si mengine bali ni kumtosa kwa sababu kuu mbili;
1.Alishakutenda
2.Umeshasema mwenyewe kwamba unamchukia kwa sasa,na hii ndiyo sababu ya msingi.Hiyo ya kwanza ungeweza kuifumbia macho kama ungekuwa bado unampenda.So usipate tabu wewe tii moyo wako,be patient mungu atakupa mwingine mtakaependana kwa dhati,vinginevyo utajuta mara ya pili.
 
usirudiane nae kwani hujui kilichomtoa huko mpaka atake kurudiana na wewe tena..pili jitahidi kuikubali hali iliyokupata na uisahau kwani wanaume wote siyo wasaliti..muombe mungu sana hakika atakusaidia na kukuonyesha njia iliyo sahihi..!
 
Bora ufanye mahusiano na mtu mwingine mpya kuliko huyo kwakuwa hujui nia na lengo lake la kurudi kwako! Na pindi akikutenda kwa mara ya pili, utakuwa na maswali mengi ya kujiuliza na ambayo yatageuka na kuwa uchuro kwako. TAFAKARI.

Mimi naungana mkono na ushauri wako hapo juu.

kuna usemi usemao, sio kila ex wako akiomba mrudiane ana nia nzuri. Pengine amekuja kuongeza risasi ili aweze kukumaliza vizuri.

Be extra careful kabisa na naamini kwa asilimia zaidi ya 100 kuwa Mungu anakupenda na ana kusudi na yaliyotokea.
 
Pole sana nakushauri usirudiane nae kwani hujui kilichomtoa huko mpaka atake kurudiana na wewe tena..pili jitahidi kuikubali hali iliyokupata na uisahau kwani wanaume wote siyo wasaliti..muombe mungu sana hakika atakusaidia na kukuonyesha njia iliyo sahihi..!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom