Wapendwa katika Bwana wana MMU: Nitumie nafasi hii kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa wote mlionishauri katika jambo hili hadharan na hata pm. Mungu azidi kuwapa hekima na maisha marefu yenye kila aina ya furaha.
Kwasasa naishi kwa amani kabisa bila hata huyo jamaa na hata ile hasira niliyokua nayo mwanzo haipo tena. MMU imenifanya nijione niko strong kupitia ushauri wenu. Na ningependa hata wale wanaopitia maumivu ya kimapenzi kwasasa wapige moyo konde waone kwamba kuna maisha mengine mbele ya hao ma x zao. Tujifunze kukubali matokea na kusonga mbele,maisha yako yanakutegemea wewe mwenyewe uyajenge wala usisubiri mwingine akujengee.
Amen Amen sweetheartnimependa ushauri wako mkuu.
BTW wengi tunaumizwa kwa kutosimama imara, Mungu hakutuumba ili tuje tulie bali kumtukuza kwa kila sekunde anayotupa nafasi kuishi hapa duniani. Binafsi nimetokea kumchukia huyo rafiki yake wa karibu maana yeye haswa ndo chanzo cha maumivu ya Valentina.
Nikushauri piga moyo konde na chonde chonde usimrudie tena maana huwez jua Mungu alikuwa anakuepusha nini. cha msingi piga goti kwa Mungu na umsihi akupe mwanaume wako wa maisha na pili huna sababu ya kuyafikiria uliyotendewa ukiwa na new rltn.
Kuna msemo waswahili husema wanaume wote ni sawa wamezaliwa na mama mmoja mimi nakataa kabisa, wanaume wanatofautina na kamwe usiweke akilin mwako kuwa utatendwa kila siku. Kumbuka Mungu anakupenda sana na hawezi kamwe kukubali upitie tena magumu uliyopitia kama unamtegemea.
Tena wakati mwingine Mungu huruhusu mapito ili uwe imara zaidi.
nikutakie maisha mema na Mungu awe nawe katika relation ambayo unayo au unayotegemea kuinza.
Yaani unatoa ushauri halafu hapo hapo unaanza kutongoza?...nina moyo kama wako dada naomba ni pm.
Dah.! Long tym. Mambo vip 'Valentina'
Kwasasa nipo nipo kwenye uhusiano mwingine naenjoy
Wapendwa ni matumaini yangu mpo wazima na mko vizuri katika majukumu yenu
Leo ninaomba kushare nanyi jambo ambalo limekua likinitatiza kwa muda sasa. Ninatambua kila mmoja wetu ana historia yake ya kimapenzi na wengi tumetendwa na wale ambao tuliwekeza mioyo yetu kwao kwa kuwaamini kwamba wataiendeleza furaha yetu, ila kwasababu mbalimbali au kwa bahati mbaya wengi hatukuweza kufikia matarajio yetu juu ya hao wenzetu.
Binafsi nilikua katika mahusiano na mtu ambae nilimpenda mno narudia tena nilimpenda tena mno. Na ndie mwanaume wangu wa kwanza kukutana nae kimwili.
Naye kwa upande wake alionyesha uaminifu na moyo wakujali,maneno yote mazuri yenye matumaini mtoto wa kike niliambiwa, kifupi tulipanga uhusiano wetu uzae ndoa.
Ilifika hatua mwezi wa sita mwaka jana akaja Arusha kwalengo la kujitambulisha nyumbani kwetu. Lakini ghafla katika hali ambayo sikuitarajia akabadilisha maamuzi yake akanipa visingizio.
Baada ya muda mfupi kabla ya yeye kurejea kwenye makazi yake, nikamfumania akiwa na rafiki yangu wa karibu, rafiki niliye mchukulia kama ndugu yangu na kushare nae baadhi ya mambo.
Waliosalitiwa bila shaka wanaelewa uzito wa maumivu hayo. Ikabidi niwe mpole,na kuwaambia waendelee mbele,siku zilivosonga yule binti akaanza mambo ya dharau kwangu ila namshkuru Mungu nilipata moyo wa kumsamehe na kupuuza dharau zake.
Ilipofika mwezi wa 9 yule binti aliacha kazi kwa shari na kurudi kwao.
Sasa kilichonifanya nije hapa mbele yenu leo, nikwamba yule mwanaume anataka kurudi kwangu na mimi moyo wangu unakua mzito kumrudia, nimetokea kumchukia.
Jambo linalonisumbua zaidi kila ninapoanza mahusiano mapya hua nashindwa kuendelea mbele, hofu ya kwamba huyu atanifanyia kama yule inanijia mara kwa mara na matokeo yake nakua sababu ya kuvunjika uhusiano huo.
Wapendwa nifanye nini kukabiliana na hali hii ya pili? Ninatamani sana hali hii iniondoke. Karibu kwa mchango wako kimawazo.
Kwenye makosa ya kiuandishi mnisamehe maana natumia simu.
ndio maana nakupenda dottoMe kwanza nakupongeza Kwa moyo wa kuwa mpole, na kuwaruhusu waendelee na ka mchezo. kudadadekii...!!!!! me ningedeadisha mtu hapo. yani nikufumanie then nikuache bili ngeo hapana!!!!
Pili. Usithubutu kurudiana na huyo malaya atakuja kukuua. yatakuja kukupata makubwa zaidi ya hayo yalokupata.
Tatu. Sasa acha uoga ondoa hofu soon kuna penzi moja la ukweli linakuja mbele yako. ondoa ile dhana kuwa eti wanaume wote ni sawa. hapana ni tofauti sana. so plz just patient