Kutendwa kumenifanya nisijielewe

Kutendwa kumenifanya nisijielewe

kuna mtu alininong'onezaga kuwa mtu mwenye mpenzi mmoja akitendwa inauma sana! Nilikuwa mgumu kushangaa... Em nijipe muda kutafakari hako kausemi,labda nitaelewaga baadaye
Swts mdogo wangu natamani hiyo avatar yako!
niazimepo mwayego!
 
Last edited by a moderator:
Valentina kwanza pole sana mama halafu pili usije thubutu kurudiana na mwanaume huyo jiulize kama aliweza kukusaliti mara ile ya kwanza ambapo mapenzi ndo yalikuwa moto moto mapenzi ya mwanzoni atashindwa nini kukusaliti wakati huu ambapo ameshawahi kukusalitit mara ya kwanza?

wanasema what goes around comes around asikudanganye huyo mwanaume,weka msimamo imara mwambie no tena big no na uendelee hivyo hivyo ajue kuwa hutaki tena kuwa naye.


kaa chini urelax usiingie kwenye mapenzi haraka haraka tena chukua muda kumjua mtu kiundani hope one day utampata wako wa moyo mtakayefaana na kisha kufikia ndoa,coz wanasema muda ni jibu so em jipe muda kidogo mama.
 
Last edited by a moderator:
In short usikubali kurudiana nae maana tayari ameshaonesha hana upendo wa dhati kwako!
(ukimrudia usije kulalamika tena hapa)
halafu muombe Mungu akusaidie kwenye hali kama hiyo!
Kingine nafikiri ungesubiri kwanza moyo wako upone ndo uanze uhusiano mwingine!

Me nadhani hicho ndicho cha msingi ktk maisha kama haya
 
We kua nae halafu uje umsaliti kama alivyokufanyiaa au tupa kuleee
 
Wapendwa ni matumaini yangu mu wazima na mko vizuri katika majukumu yenu:

Leo ninaomba kushare nanyi jambo ambalo limekua likinitatiza kwa muda sasa. Ninatambua kila mmoja wetu ana historia yake ya kimapenzi na wengi tumetendwa na wale ambao tuliwekeza mioyo yetu kwao kwa kuwaamini kwamba wataiendeleza furaha yetu, ila kwasababu mbalimbali au kwa bahati mbaya wengi hatukuweza kufikia matarajio yetu juu ya hao wenzetu....

Binafsi nilikua katika mahusiano na mtu ambae nilimpenda mno narudia tena nilimpenda tena mno. Na ndie mwanaume wangu wa kwanza ku........
Nae kwa upande wake alionyesha uaminifu na moyo wakujali,maneno yote mazuri yenye matumaini mtoto wa kike niliambiwa,Kifupi tulipanga uhusiano wetu uzae ndoa.

Ilifika hatua mwezi wa sita mwaka jana akaja Arusha kwalengo la kujitambulisha nyumbani kwetu. Lakini gafla katika hali ambayo sikuitarajia akabadilisha maamuzi yake akanipa visingizio. Baada ya muda mfupi kabla ya yeye kurejea kwenye makazi yake,nikamfumania akiwa na rafiki yangu wa karibu,rafiki niliye mchukulia kama ndugu yangu na kushare nae baadhi ya mambo.

Waliosalitiwa bila shaka wanaelewa uzito wa maumivu hayo. Ikabidi niwe mpole,na kuwaambia waendelee mbele,siku zilivosonga yule binti akaanza mambo ya dharau kwangu ila namshkuru Mungu nilipata moyo wa kumsamehe na kupuuza dharau zake. Ilipofika mwezi wa 9 yule binti aliacha kazi kwa shari na kurudi kwao.
Sasa kilichonifanya nije hapa mbele yenu leo,nikwamba yule mwanaume anataka kurudi kwangu na mimi moyo wangu unakua mzito kumrudia,nimetokea kumchukia.

Jambo linalonisumbua zaidi kila ninapoanza mahusiano mapya hua nashindwa kuendlea mbele,hofu ya kwamba huyu atanifanyia kama yule inanijia mara kwa mara na matokeo yake nakua sababu ya kuvunjika uhusiano huo.
Wapendwa nifanye nini kukabiliana na hali hii ya pili? Ninatamani sana hali hii iniondoke. Karibu kwa mchango wako kimawazo.
Kwenye makosa ya kiuandishi mnisamehe mana natumia cm.

heeee,vijana kwa sasa suala la kutendwa lishakua janga la kitaifa,pole sana,za kuambiwa changanya na za kwako,sie wengine kunguru waoga,tunakimbiza mbawa zetu
 
Binamutz hiyo sehemu unayoipenda ndio kilio cha dunia natamani hata isingekuwepo imekuwa chungu kumeza
 
achana nae 2 dada angu mwisho ataweza kukuletea magonjwa uje kujutia useme bora usingemrudia ndio hivyo ninge haitangulii!achanae atakupa 2 pressure my dia pole sana!
 
Songa mbele best wangu,jipange,fanya kazi kwa bidii,tafta pesa kwanza ujenge maendeleo,utampata tu atakayekupenda tofauti na huyo wa mwanzo,achana nae kumbka mda haurudi nyuma otherwise utakuja juta tena,mapenzi yapo tu rafk yangu,asikupe tena stress huyo,jifunze kutokana na makosa,settle kwanza ufanye mambo ya muhimu zaid
 
Samahani lakini,

Toka mwezi wa sita mwaka jana mpaka leo hii,Ni mahusiano Mangapi umeyaanzisha na vidume ikakubidi uyakatisha kuogopa kutendwa kama alivyo kutenda wakwanza huyo????
 
Jamani kimbia mbio huyo akirudi atakusaliti tena. Cha msingi fungua moyo wako uruhusu mwingine aingie kwa wansume wote sio sawa wapo ambao mungu amewajalia wanaijua thamani ya mwanamke
 
Samahani lakini,

Toka mwezi wa sita mwaka jana mpaka leo hii,Ni mahusiano Mangapi umeyaanzisha na vidume ikakubidi uyakatisha kuogopa kutendwa kama alivyo kutenda wakwanza huyo????

Wawili hua naishia njiani ndani ya mwezi mmoja.
 
Back
Top Bottom