Papaa pedeshee
JF-Expert Member
- Nov 7, 2021
- 234
- 337
Ndugu wana JF habari ya majukumu?
Napenda kutoa taarifa juu ya kusudio la kuuza kiwanja namba 10 D-centre Mwangaza lililopo Dodoma mara tu baada ya kukamilisha upatikanaji wa Hati ya eneo hilo ifikapo mwakani mwezi Januari au Februari kwakuwa eneo lilikuwa limetwaliwa na wenye nguvu almaarufu vigogo tena wakiwa Serikalini lakini bahati nzuri MUNGU wetu wa familia amekuwa juu yetu na mambo yanakwenda vizuri sana.
Kiufupi eneo hilo lilikuwa lina offer na likimilikiwa na aliyekuwa bingwa wa magonjwa ya Moyo nchini na mmiliki wa Taasisi ya magonjwa ya moyo (THI) Dr. Masau aliyefariki 2013, hivyo eneo linatambulika kwa jina la Dr. Ferdinard Masau Heart Institute company ltd.
Eneo hilo limetenganishwa na barabara ya lami iendayo kisasa hadi UDOM huku linapakana na nyumba 300 wanazokaa watumishi wa serikali, upande mwingine magharibi linapakana na kigango cha kanisa katoliki na sambamba pia na shule ya Raisei primary English medium school kwa upande mwingine.
Halikadhalika upande wa juu yake kuna apartment na makazi ya watu, huku ukiangalia SGR ikipita na kukiwa na kituo chake umbali kadhaa tokea eneo la kiwanja.
Hivyo kiwanja kilitolewa kwa ajili ya Taasisi na hivyo tunakusudia kubadilisha matumizi yake hapo baadaye.
Kuhusu bei; eneo linakadiriwa kubwa na thamani isiyopungua 300M. Hata hivyo tathmini itafanyika kabla ya kuuza eneo hilo.
Kwa leo sitaweka picha kutokana na simu yangu kupata shida kidogo lakini wakati ukifika nitaweka kila kilicho muhimu kuwepo, hivyo kwa leo pokeeni kama taarifa tu wana JF.
Nb. Eneo linafaa pia kwa matumizi ya petro station na majengo ya kibiashara.
Naomba kuwasilisha.