Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa anataka kuniuzia kiwanja changu mwenyewe

Ngurukia

JF-Expert Member
Feb 25, 2023
1,484
6,228
Nina kiwanja changu kama nusu eka nilichonunua 2012 maeneo ya Chanika. Nilikizungushia fence ya waya na mara moja moja nilikuwa natuma mtu apasafishe.

Takriban miaka 6 nilikuwa nje ya Dar kikazi. Nimerudi mwisho wa mwezi wa 9 ila ilikuwa sijapata fursa ya kwenda kwenye kiwanja changu.

Jana nilikutana na jamaa yangu ambae ni dalali. Katika kupiga story akaniambia kuna kiwanja kikubwa kinauzwa Chanika. Baada ya kutaja eneo nikamwambia hata mimi nina eneo langu huko. Tukakubaliana leo tuende kuangalia kiwanja chake anachouza na mimi nipitie kwangu.

Tulianzia kwa Mwenyekiti wa Serikali za mitaa maana kwa mujibu wa dalali ndiye muhusika mkuu.

Kupelekwa kwenye kiwanja ni eneo langu. Sijataka kusema chochote nikamuacha aongee tu. Anadai kiwanja ni cha baba wa mkewe kampa mwanae hivyo wameamua kuuza.

Kumuhoji kuhusu nyaraka akadai anao mkataba wa mauziano wa serikali za mitaa. Nimeona copy una tarehe ya 2014. Mimi nina leseni ya makazi na tayari hati ipo katika process. Zoezi la hati lilifanywa shirikishi kwa wakazi wa eneo lote hilo.

Nilichoamua, kesho naamkia polisi kumshitaki jamaa kwa utapeli maana nina rekodi ya sauti ya maongezi yake yote. Nitahakikisha mpaka wamtie ndani.

Angalizo kwa walimwengu, wekeni mazoea ya kutembelea viwanja vyenu, msitelekeze kwa muda mrefu bila kwenda. Hakikisheni kila document ipo up to date na la muhimu zaidi epukeni sana kununua viwanja kiholela bila kujiridhisha ardhi kwanza.
 
Ndio dawa yao, na hakikisha unamnyoosha ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia za kishenzi kama hizo

Na hao wenyeviti ndio kabisaa, wanajua mwakani kwenye uchaguzi huwa wanaweza wasirudi

kwa mnaonunua viwanja sasa kuweni makini sana hasa viwanja vinavyosimamiwa na serikali za mtaa hasa mwakani kabla ya uchaguzi wao, hapo kujilipua na kupigwa ni kwingi sana
 
Mweleweshe ila usimuweke ndani Mwambie tu aache ujanja ujanja
Unadhani angefanikiwa kukiuza angekubali kueleweshwa tu.

Mungu amesimamia haki yangu kwa kunibainishia kabla madhara hayajatokea.

Kwa ujasiri aliokuwa nao, nina hakika keshafanya sana huu mchezo. Na mtu kama huyu ili aache ni lazima kwanza asiwe na hayo madaraka yanayompa ujasiri na lazima awajibishwe ili kama kuna walioathirika kwa utapeli wake wapate haki yao.
 
Uyooo
Unadhani angefanikiwa kukiuza angekubali kueleweshwa tu.

Mungu amesimamia haki yangu kwa kunibainishia kabla madhara hayajatokea.

Kwa ujasiri aliokuwa nao, nina hakika keshafanya sana huu mchezo. Na mtu kama huyu ili aache ni lazima kwanza asiwe na hayo madaraka yanayompa ujasiri na lazima awajibishwe ili kama kuna walioathirika kwa utapeli wake wapate haki yao.
Uyo ndo tapel mwenyewe sema anakuchoraa tu kesho atakuzimia simu believe me
 
Utakuta mwenyekiti nayeye yupo JF,ushamsanua😂😂.
Nililiwaza hili kabla ila nina hakika hayupo kwa sababu kadhaa,

Nilipoomba picha ya eneo jana kwa dalali akasema mwenyekiti anatumia simu ndogo na hajui mambo whatsapp.
Leo nilipokutana nae nilimuuliza kama alishawahi kupost kiwanja kama anauza akasema hata hajui wanapost vipi. Na kweli niliona tecno zake za button mbili.

Na hata ikitokea akaona, kwa hatua niliyofokia ya kuwa na rekodi ya maongezi yake na video akinionyesha kiwanja hawezi kuchoropoka.
 
Back
Top Bottom