Sababu 30 Zinazopelekea Mmiliki Wa Kiwanja/Shamba/Jengo Kuuza Kwa Bei Nafuu

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
156
240
Kuuza Kiwanja/Shamba/Jengo Kwa Hamasa Kubwa

Hamasa ya muuzaji ni kile kinachomsukuma mmiliki auze ndani ya siku anazotegemea. Hamasa inaweza kuwa moja ya mambo yafuatayo:-

✓ Kutalakiana kwenye ndoa.

✓ Migogoro ya ubia miongoni mwa wamiliki wa kiwanja, au jengo.

✓ Kupoteza ajira.

✓ Kuhamishwa kituo cha kazi.

✓ Kusimamishwa kazi na malipo kupunguzwa au kusimamishwa.

✓ Kutokea kwa kifo au vifo.

✓ Uwepo wa shauri (kesi) mahakamani.

✓ Kuwekeza kutoka nje ya mkoa au nje ya nchi (long-distance real estate investing/out of state real estate investing).

✓ Kupata nafasi ya kwenda kusoma nchi za nje.

✓ Uhitaji wa kulipia ada na michango ya shule, vyuo na vyuo vikuu.

✓ Hisia kali juu ya hali mbaya au hali nzuri sana ya soko la ardhi na majengo.

✓ Maneno ya umma ambayo yanaathiri maamuzi ya mmiliki wa kiwanja au nyumba.

✓ Changamoto za kisiasa.

✓ Changamoto za kidini au kidhehebu.

✓ Changamoto za kudorora kwa uchumi wa familia au mmiliki husika wa kiwanja au jengo husika.

✓ Kushindwa kukamilisha ujenzi wa nyumba nyingine ya kuishi au ya uwekezaji.

✓ Nyumba au kiwanja kuonekana kukosa manufaa makubwa kwa mmiliki wake.

✓ Kushindwa kukamilisha marejesho ya mkopo wa watumishi, mkopo wa biashara au mkopo wa majengo.

✓ Migogoro katika familia.

✓ Migogoro kwenye ukoo.

✓ Kufilisika kwa mmiliki wa kiwanja au jengo.

✓ Kuzeeka kwa mmiliki wa mali inayouzwa.

✓ Kukosa maarifa sahihi ya soko mahalia (local real estate markets).

✓ Halmashauri ya wilaya kuhitaji fedha za malengo fulani.

✓ Wananchi wa kata kuhitaji fedha kwa ajili ya malengo fulani.

✓ Wanakijiji kuwa na uhitaji mkubwa wa fedha kwa ajili ya kutatua changamoto zao.

✓ Maendeleo ya kifedha kwa mmiliki wa kiwanja, shamba au jengo.

✓ Ongezeko la matukio ya kihalifu katika mtaa husika. unatakiwa uwe na njia za kukabiliana na uhalifu uliopo eneo husika.

✓ Tetesi za kutokea kwa vita.

✓ Milipuko ya magonjwa tatanishi.

Hutakiwi kuwa kwenye hamasa za aina hii kama wewe ni muuzaji wa kiwanja au shamba. Ukiuza kiwanja au jengo wakati upo kwenye hamasa hizi, huwezi kutengeneza fedha wakati wa kuuza kiwanja au nyumba.

Kutengeneza fedha wakati wa kuuza kiwanja au nyumba maana yake ni kuwa unauza kwa bei ghali kidogo kutokana na njia za kuongeza thamani ulizotumia.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Mbobezi majengo.

Whatsapp; +255 752 413 711
 
Back
Top Bottom