Kusimamishwa kazi kwa Ole Sabaya, liwe somo kwa wale viongozi wanaopenda kutumia ubabe na kutotii sheria za nchi

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,657
2,000
Miongoni ya habari ambazo zimepokelewa kwa shangwe kubwa hapa nchini, ni hii ya kusimamishwa kazi kwa aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Ole Sabaya

Kulikuwa na malalamiko mengi sana toka kwa wananchi, kwa kipindi kirefu kuwa huyu jamaa, anatumia ubabe, tena kwa kutumia vyombo vya dola, kuwadhulumu wananchi wasio na hatia.

Malalamiko kama kutumia silaha za moto kwa kuwanyang'anya wafanyibiashara pesa zao, zimekuwa ni tuhuma zilizozoeleka masikioni mwa wananchi, kumhusu huyo, Ole Sabaya, aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai

Hatimaye kilio hicho kimesikika kwenye mamlaka ya uteuzi, ambapo Rais wa Jamhuri ya Tanzania na Amiri Jeshi mkuu, Samia Suluhu Hassan, amelazimika kuchukua uamuzi mgumu wa kumsimamisha kazi, ili kupisha uchunguzi.

Nimediriki kuuita ni uamuzi mgumu aliochukua Rais Samia Suluhu, kwa kuwa ilizoeleka wakati wa utawala uliopita wa mwendazake, kutosikiliza kabisa vilio vya wananchi, kuhusu wateule wake.

Kwa hiyo hii iwape funzo wateule wa Rais, kuwa enzi zimebadilika na mwendazake, ambaye ndiye alikuwa "akiwakingia" kifua, sasa hayupo na tuna kiongozi mpya, ambaye kwa kipindi kifupi, alichoongoza nchi hii, ingawa yeye mwenyewe amekuwa akikaririwa akisema kuwa yeye na Magufuli ni kitu kimoja, lakini kutokana na mwenendo anaoenda nao, ni dhahiri kuwa wapo tofauti sana katika utendaji wao, wakati mwendazake alipenda sana kuendesha serikali yake kwa ubabe na kuona hakuna umuhimu wa kutotii sheria, kwa kupitia wateule wake. Huyu wa sasa, anaelekea ana hofu ya Mungu na angependa wateule wake, watekeleze majukumu yao kwa weledi na kwa kufuata sheria za nchi.

Mama Samia Suluhu ni kama vile amewasha "warning bell" na kwa hiyo wale viongozi waliokuwa wakitekeleza uonevu mkubwa kwa wananchi, hususani kwa viongozi wa vyama vya kisiasa vya upinzani kwa maelekezo ya mwendazake, watambue ya kuwa mwendazake keshatangulia mbele za haki na hivi sasa nchi ina kiongozi mpya, Rais Samia Suluhu, ambaye mwelekeo wake unaonekana una tofauti kubwa baina yake na mtangulizi wake.
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,657
2,000
Vijana wametuangusha sana kipindi hicho cha Mwendazake! Pia mafunzo ya uongozi yasikome kufanyika kwa vijana wetu. Bado wanahitaji kupikwa kweli kweli. La sivyo hatutakaa tupate viongozi kutoka kwa vijana.
Siyo vijana wote ni wabaya, ila kosa kubwa alilolifanya mwendazake ni kuweka "qualification" kubwa katika uteuzi wake ni lazima uwe mbabe na usiyelazimika kuzitii sheria za nchi!
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,657
2,000
Katika hiyo list, huwezi kumuacha Ndugai, Spika wa Bunge letu, ambaye kwa makusudi kabisa, ameamua kuisigina Katiba ya nchi kwa kuwakunbatia wale wabunge wa viti maalum, akina Halima Mdee, waliofukuzwa uanachama wao na chama chao cha Chadema
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
121,572
2,000
Mkuu walikuwa wanamuiga dikteta magufuli. Je, awamu ya Samia watashughulikiwa hao vidikteta uchwara wakati mama KISHADEMKA kwamba yeye na dhalimu ni kitu kimoja? Ngoja tuone. By the way ile ripoti ya pesa zilizochukuliwa BoT kuanzia January 1st hadi March 31st mbona mama kaifanya siri? KULIKONI?
Miongoni ya habari ambazo zimepokelewa kwa shangwe kubwa hapa nchini, ni hii ya kusimamishwa kazi kwa aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Ole Sabaya

Kulikuwa na malalamiko mengi sana toka kwa wananchi, kwa kipindi kirefu kuwa huyu jamaa, anatumia ubabe, tena kwa kutumia vyombo vya dola, kuwadhulumu wananchi wasio na hatia.

Malalamiko kama kutumia silaha za moto kwa kuwanyang'anya wafanyibiashara pesa zao, zimekuwa ni tuhuma zilizozoeleka masikioni mwa wananchi, kumhusu huyo, Ole Sabaya, aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai

Hatimaye kilio hicho kimesikika kwenye mamlaka ya uteuzi, ambapo Rais wa Jamhuri ya Tanzania na Amiri Jeshi mkuu, Samia Suluhu Hassan, amelazimika kuchukua uamuzi mgumu wa kumsimamisha kazi, ili kupisha uchunguzi.

Nimediriki kuuita ni uamuzi mgumu aliochukua Rais Samia Suluhu, kwa kuwa ilizoeleka wakati wa utawala uliopita wa mwendazake, kutosikiliza kabisa vilio vya wananchi, kuhusu wateule wake.

Kwa hiyo hii iwape funzo wateule wa Rais, kuwa enzi zimebadilika na mwendazake, ambaye ndiye alikuwa "akiwakingia" kifua, sasa hayupo na tuna kiongozi mpya, ambaye kwa kipindi kifupi, alichoongoza nchi hii, ingawa yeye mwenyewe amekuwa akikaririwa akisema kuwa yeye na Magufuli ni kitu kimoja, lakini kutokana na mwenendo anaoenda nao, ni dhahiri kuwa wapo tofauti sana katika utendaji wao, wakati mwendazake alipenda sana kuendesha serikali yake kwa ubabe na kuona hakuna umuhimu wa kutotii sheria, kwa kupitia wateule wake, huyu wa sasa, anaelekea ana hofu ya Mungu na angependa wateule wake, watekeleze majukumu yao kwa weledi na kwa kufuata sheria za nchi.

Mama Samia Suluhu ni kama vile amewasha "warning bell" na kwa hiyo wale viongozi waliokuwa wakitekeleza uonevu mkubwa kwa wananchi, hususani kwa viongozi wa vyama vya kisiasa vya upinzani kwa maelekezo ya mwendazake, watambue ya kuwa mwendazake keshatangulia mbele za haki na hivi sasa nchi ina kiongozi mpya, Rais Samia Suluhu, ambaye mwelekeo wake unaonekana una tofauti kubwa baina yake na mtangulizi wake.
 
Afande Tanzania

JF-Expert Member
May 3, 2020
460
1,000
Katika hiyo list, huwezi kumuacha Ndugai, Spika wa Bunge letu, ambaye kwa makusudi kabisa, ameamua kuisigina Katiba ya nchi kwa kuwakunbatia wale wabunge wa viti maalum waliofukuzwa na chama chao cha Chadema
Hatuna spika, tuna Mzee mmoja mhuni aliyekosa busara, asiyeheshimu katiba ya nchi Bali maslahi binafsi.
Hawa ndo wanaofanya chuki inaongezeka katika jamii, wamesahau vile wakipata matatizo jamii hufurahi, kiburi Cha madaraka shame on his face
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,657
2,000
Mkuu walikuwa wanamuiga dikteta magufuli. Je, awamu ya Samia watashughulikiwa hao vidikteta uchwara wakati mama KISHADEMKA kwamba yeye na dhalimu ni kitu kimoja? Ngoja tuone. By the way ile ripoti ya pesa zilizochukuliwa BoT kuanzia January 1st hadi March 31st mbona mama kaifanya siri? KULIKONI?
BAK
Tufahamu kuwa mama amepewa uongozi wa nchi, wakati mtangulizi wake mwendazake, alikuwa amesambaratisha kabisa mifumo ya utoaji haki nchi hii.

Mimi nadhani tungempa muda mama, madhari ameonyesha nia ya kutokuwa sambamba na mwendazake, basi tufanye subira, kwa kuwa wahenga walisema subira yavuta heri
 
Naipendatz

JF-Expert Member
Jul 27, 2011
2,856

Mkuu unataka Mama afanye mambo mangapi kwa wakati mmoja? Kuna ubaya gani kusubiri? Maadam alilisema hilo hadharani basi naamini litatolewa hadharani kulingana na ratiba zake, tuwe na subira kiongozi.
 
SAGAI GALGANO

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
30,516
2,000
Katika hiyo list, huwezi kumuacha Ndugai, Spika wa Bunge letu, ambaye kwa makusudi kabisa, ameamua kuisigina Katiba ya nchi kwa kuwakunbatia wale wabunge wa viti maalum, akina Halima Mdee, waliofukuzwa uanachama wao na chama chao cha Chadema
Ndungai huyu shughuli yake tayari.
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
121,572
2,000
Sawa Mkuu lakini wahenga walisema biashara asubuhi jioni kuhesabu faida. Rudia kauli yake kwamba, “mtasubiri sana kuhusu katiba mpya” Angalia ukimya wake kuhusu swala la Covid-19 kule mjengoni. Ni miezi miwili sasa bado hajakutana na Chadema ambao mimi nawaona ndiyo wapinzani wa kweli. Kutokana na haya nimeshapoteza imani na mama kwamba hana mia njema ya kuleta mabadiliko ya kweli ya kisiasa nchini kwa kuhofia asiwe chanzo cha maccm kuzikwa milele kwenye anga za kisiasa nchini.

BAK
Tufahamu kuwa mama amepewa uongozi wa nchi, wakati mtangulizi wake mwendazake, alikuwa amesambaratisha kabisa mifumo ya utoaji haki nchi hii.

Mimi nadhani tungempa muda mama, madhari ameonyesha nia ya kutokuwa sambamba na mwendazake, basi tufanye subira, kwa kuwa wahenga walisema subira yavuta heri
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
121,572
2,000
Wakati kule mjengoni wale COVID 19 wanaendelea kuvuta pesa ya walipa kodi kiharamu. Hivi inachukua muda gani kwa mama kutamka hadharani kwamba wale wako mjengoni kinyume na katiba hivyo wasiruhusiwe tena kuhudhuria bunge!? She can do this in less than 5 minutes but it’s 2 months and counting.
1620956638187.jpeg

Mkuu unataka Mama afanye mambo mangapi kwa wakati mmoja? Kuna ubaya gani kusubiri? Maadam alilisema hilo hadharani basi naamini litatolewa hadharani kulingana na ratiba zake, tuwe na subira kiongozi.
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
170,732
2,000
Miongoni ya habari ambazo zimepokelewa kwa shangwe kubwa hapa nchini, ni hii ya kusimamishwa kazi kwa aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Ole Sabaya

Kulikuwa na malalamiko mengi sana toka kwa wananchi, kwa kipindi kirefu kuwa huyu jamaa, anatumia ubabe, tena kwa kutumia vyombo vya dola, kuwadhulumu wananchi wasio na hatia.

Malalamiko kama kutumia silaha za moto kwa kuwanyang'anya wafanyibiashara pesa zao, zimekuwa ni tuhuma zilizozoeleka masikioni mwa wananchi, kumhusu huyo, Ole Sabaya, aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai

Hatimaye kilio hicho kimesikika kwenye mamlaka ya uteuzi, ambapo Rais wa Jamhuri ya Tanzania na Amiri Jeshi mkuu, Samia Suluhu Hassan, amelazimika kuchukua uamuzi mgumu wa kumsimamisha kazi, ili kupisha uchunguzi.

Nimediriki kuuita ni uamuzi mgumu aliochukua Rais Samia Suluhu, kwa kuwa ilizoeleka wakati wa utawala uliopita wa mwendazake, kutosikiliza kabisa vilio vya wananchi, kuhusu wateule wake.

Kwa hiyo hii iwape funzo wateule wa Rais, kuwa enzi zimebadilika na mwendazake, ambaye ndiye alikuwa "akiwakingia" kifua, sasa hayupo na tuna kiongozi mpya, ambaye kwa kipindi kifupi, alichoongoza nchi hii, ingawa yeye mwenyewe amekuwa akikaririwa akisema kuwa yeye na Magufuli ni kitu kimoja, lakini kutokana na mwenendo anaoenda nao, ni dhahiri kuwa wapo tofauti sana katika utendaji wao, wakati mwendazake alipenda sana kuendesha serikali yake kwa ubabe na kuona hakuna umuhimu wa kutotii sheria, kwa kupitia wateule wake, huyu wa sasa, anaelekea ana hofu ya Mungu na angependa wateule wake, watekeleze majukumu yao kwa weledi na kwa kufuata sheria za nchi.

Mama Samia Suluhu ni kama vile amewasha "warning bell" na kwa hiyo wale viongozi waliokuwa wakitekeleza uonevu mkubwa kwa wananchi, hususani kwa viongozi wa vyama vya kisiasa vya upinzani kwa maelekezo ya mwendazake, watambue ya kuwa mwendazake keshatangulia mbele za haki na hivi sasa nchi ina kiongozi mpya, Rais Samia Suluhu, ambaye mwelekeo wake unaonekana una tofauti kubwa baina yake na mtangulizi wake.
IMG-20210514-WA0039.jpg
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
170,732
2,000
Katika hiyo list, huwezi kumuacha Ndugai, Spika wa Bunge letu, ambaye kwa makusudi kabisa, ameamua kuisigina Katiba ya nchi kwa kuwakunbatia wale wabunge wa viti maalum, akina Halima Mdee, waliofukuzwa uanachama wao na chama chao cha Chadema
The next...!!!
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
170,732
2,000
Mkuu walikuwa wanamuiga dikteta magufuli. Je, awamu ya Samia watashughulikiwa hao vidikteta uchwara wakati mama KISHADEMKA kwamba yeye na dhalimu ni kitu kimoja? Ngoja tuone. By the way ile ripoti ya pesa zilizochukuliwa BoT kuanzia January 1st hadi March 31st mbona mama kaifanya siri? KULIKONI?
Kubwa kuliko hiyo kaka.. Maza anaenda nayo kwa timing kama kumchinja kobe
 
Naipendatz

JF-Expert Member
Jul 27, 2011
2,856
2,000
Wakati kule mjengoni wale COVID 19 wanaendelea kuvuta pesa ya walipa kodi kiharamu. Hivi inachukua muda gani kwa mama kutamka hadharani kwamba wale wako mjengoni kinyume na katiba hivyo wasiruhusiwe tena kuhudhuria bunge!? She can do this in less than 5 minutes but it’s 2 months and counting.
View attachment 1783885
Hapo unakosea pia Mkuu, wakati wa mwendazake kelele zilipigwa sana kwamba anaingilia mihimili mingine, Mahakama na Bunge, Mama akiingilia ishu ya covid-19 hatokuwa tofauti na mwendazake, ila kwa hili mtamshangilia kwa sababu tu atakuwa amewafurahisha nyinyi. Nafikiri kila muhimili uachwe ufanye shughuli zake bila kuingiliwa. BTW hao CDM wamekosa njia kabisa za kisheria kuwatoa hao Covid-19? Kisingizio chao ni kuwa wamekata rufaa Baraza kuu, kwa nini hilo baraza kuu lisikae na kuwavua moja kwa moja uanachama? Utasema watakimbilia mahakamani, wakienda mahakamani ni vizuri zaidi maana katiba ya CDM inasema mwanachama yeyote akienda mahakamani kukishtaki chama na akishindwa kesi anakuwa kajifukuzisha uanachama.
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
121,572
2,000
Kuingilia Bunge ili kuilinda na kuitetea katiba kama alivyokula kiapo mama siku alipoapishwa ni tofauti sana na yule dikteta na dhalimu kwani yeye aliingilia Bunge ili kuikanyaga katiba na hivyo kurahisisha udikteta wake. USIPOTOSHE.
Hapo unakosea pia Mkuu, wakati wa mwendazake kelele zilipigwa sana kwamba anaingilia mihimili mingine, Mahakama na Bunge, Mama akiingilia ishu ya covid-19 hatokuwa tofauti na mwendazake, ila kwa hili mtamshangilia kwa sababu tu atakuwa amewafurahisha nyinyi. Nafikiri kila muhimili uachwe ufanye shughuli zake bila kuingiliwa. BTW hao CDM wamekosa njia kabisa za kisheria kuwatoa hao Covid-19? Kisingizio chao ni kuwa wamekata rufaa Baraza kuu, kwa nini hilo baraza kuu lisikae na kuwavua moja kwa moja uanachama? Utasema watakimbilia mahakamani, wakienda mahakamani ni vizuri zaidi maana katiba ya CDM inasema mwanachama yeyote akienda mahakamani kukishtaki chama na akishindwa kesi anakuwa kajifukuzisha uanachama.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom