Kushusha tozo za sukari kuna matokeo gani kwenye mfumuko wa bei

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
670
Waziri wa Fedha na Mipango, Dr. Mwigulu Nchemba mwenye PhD zake za uchumi amekubali kuondoa tozo kwenye sukari kwa 10%. Ni jambo jema lakini naomba nimkumbushe yafuatayo.

Sukari ina impat kwa bidhaa nyingine lakini impact kubwa na inayosafiri kwa haraka ni impact inayotokana na bei za mafuta. Ieleweke jambo moja kwamba mafuta ni bidhaa mama, au bidhaa inayobeba uzalishaji wa bidhaa nyingine ndio sababu impact yake husafiri kwa haraka kwa kuwa uzalishaji na usafirishaji wa bidhaa nyingine huathirika kwa haraka mara baada ya mafuta kubadilika bei zake.

Pia ameshauri rais mambo bora kwa kuwa hivi karibuni Rais amerudisha tozo ya Tsh. 100 kwa kigezo kuwa ilikuwa kwenye bajeti na wakati huo akubali kuondoa 10% ya tozo. Je, hii sio kumuonesha rais kuwa anajipinga muda wote?

Mwigulu, Mchumi unatambua unachojaribu kukitibu ni kile ambacho kina impact padogo yaani ni sawa na kukomaa kucontrol core inflation wakati uhalisia wa watu uko kwenye headline inflation. Mafuta yapo kwenye headline inflation.

Tuanze na bei za mafuta.

Signed
OEDIPUS
 
Wenzetu Zanzibar sukari 1kg shs 1,900 na wana kiwanda kimoja although nyingine inatoka nje, sisi huko bara viwanda kama 5 na kingine soo kinaanza kuzalisha ila sukari 2900/3100 kwa kg, mpaka hapo kuna msaada kweli?.
 
Mahitaji muhimu ya wananchi yapo mikononi mwa watu wachache ndiyo maana wanaamua kupandisha bei kwa kuwa wanajua tutanunua hata bei ikiwa mara 10 zaidi ya sasa.
 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dr. Mwigulu Nchemba mwenye PhD zake za uchumi amekubali kuondoa tozo kwenye sukari kwa 10%. Ni jambo jema lakini naomba nimkumbushe yafuatayo.

Sukari ina impat kwa bidhaa nyingine lakini impact kubwa na inayosafiri kwa haraka ni impact inayotokana na bei za mafuta. Ieleweke jambo moja kwamba mafuta ni bidhaa mama, au bidhaa inayobeba uzalishaji wa bidhaa nyingine ndio sababu impact yake husafiri kwa haraka kwa kuwa uzalishaji na usafirishaji wa bidhaa nyingine huathirika kwa haraka mara baada ya mafuta kubadilika bei zake.

Pia ameshauri rais mambo bora kwa kuwa hivi karibuni Rais amerudisha tozo ya Tsh. 100 kwa kigezo kuwa ilikuwa kwenye bajeti na wakati huo akubali kuondoa 10% ya tozo. Je, hii sio kumuonesha rais kuwa anajipinga muda wote?

Mwigulu, Mchumi unatambua unachojaribu kukitibu ni kile ambacho kina impact padogo yaani ni sawa na kukomaa kucontrol core inflation wakati uhalisia wa watu uko kwenye headline inflation. Mafuta yapo kwenye headline inflation.

Tuanze na bei za mafuta.

Signed
OEDIPUS
upo sahihi , wanataka kutuvusha kwenye maji kwa kutumia bajaji
 
Wenzetu Zanzibar sukari 1kg shs 1,900 na wana kiwanda kimoja although nyingine inatoka nje, sisi huko bara viwanda kama 5 na kingine soo kinaanza kuzalisha ila sukari 2900/3100 kwa kg, mpaka hapo kuna msaada kweli?.
Zanzibar sio wenzetu. Ndio maana Kwao bei iko chini.
 
Tozo na kodi kwenye fuel zinachangia %ngapi ya budget ya nchi? Na uliza hivyo kwa sababu ni kama hawataki kugusa mafuta kabisa.
 
Waziri wa Fedha, anakazania tu miradi miradi, anakwepa Ukubwa wa Serikali, na Posho zao, anasa zao na V 8 zao.

Serikali ipunguze matumizi ya anasa

Miradi inaendeshwa Kwa mikopo

Mmeweka Tozo, za Kijenge barabara, hospital..na mkakopa tena
 
Watu wakisha kufa kwa njaa hospitali itakuwa ina mtibu nani kwa mfano? Tunakoendea mbeleni wengine watashindwa mlo mmoja kwa siku na kubakia robo mlo au kutokula kabisa.

Ushindwe kuweka mazingira ya mtu asidondoke kwa hypoglycemia/njaa uweke mazingira ya kumdondosha ili ukamtundikie maji ya glucose wodini kwa gharama mara kumi zaidi. Wakati ulikuwa na fursa ya kuweka mazingira wezeshi ya kupata ugali na maharagwe.
 
Back
Top Bottom