Kushindwa Kwa Romney: Nini Sababu?

Kushindwa Kwa Romney: Nini Sababu?

Huu ni mjadala wa kubadilishana mawazo kitaaluma. Hivyo kama unataka kumpa ongera Baraka Obama, nakushauri fanya hivyo kwenye thread nyingine.

Jana nilipokuwa naangalia matangazo kutoka katika Boston na Chicago niliona vitu viwili muhimu. Kitu cha kwanza kwenye kambi Romney waliokuwa wanasubiri matokeo wengi walikuwa wazee na wazungu. Kitu cha pili katika kambi iliyokuwepo Chicago, wengi walikuwa ni vijana na vilevile kutoka jamii mbalimbali.

Ukichunguza vitu hivi viwili kwa makini, unaweza kusema kuwa Obama amechaguliwa sio kwa sababu anamzidi Romney kiutendaji wa kazi. Amechaguliwa kwa sababu ya muundo wa jamii zilizopo Marekani. Hii ni sababu moja na zinaweza kuwepo zingine.

Ningeomba tuzichambue hizo sababu hili tujifunze.

Z10.......

sababu kubwa ya Romney kushindwa ni kutokana na matamshi yake kuwa asilimia 47% ya wamarekani wanaishi kwa kutegemea ruzuku/msaada wa serikali.

Hivyo watu wengi walio maskini walikasirika na kumuona Romney kuwa akichaguliwa atawapendelea matajiri na kuwaacha maskini wakitaabika kwa kuwafutia posho za serikali kama ilivyotokea kwa chama cha sasa kinachotawala Uingereza. Hili ndilo pekee lililomwangusha.

Lakini laiti wamarekani wangechambua kwa umakini kauli yake wangejua alikuwa hapendezwi na umaskini wao katika taifa kubwa kama lile na angefanya bidiii kuwapa fursa ambazo zingepunguza kiwango cha umaskini wao na utegemezi wao kwa serikali.

Hili ndilo tatizo la wapiga kura wengi wanaofikiria kushiba leo bila kujali kesho yake itakuwaje?
 
Typically CCM till 2015, after that utahamia CUF.

Mbona kabla ya CCM kulikuwa na vyama vingine? usishtuke sana kwa hilo, siku zijazo, si mimi wala wewe ajuae atakuwa wapi. Una contract ya kuwepo mpaka 2015?
 
Nakubaliana na points zako nyingi. Naomba tuzungumze kuhusu kijiandaa. Romney amejiandaa kwa uchaguzi huu kwa zaidi ya miaka sita. Miaka miwili ya mwanzo alijiandaa kuwa mgombea wa uchaguzi wa 2008.

Na baada ya 2008 alianza kujiandaa na 2012. Hivyo kwa kujianzaa, alikuwa kamili. Je kuna kasoro yoyote katika maandalizi yake?

Katika chaguzi za Marekani kuna two stages; Moja, kupata nomination kwenye chama na pili Kuomba kura kwa wananchi. Romney alitumia muda wake mwingi kupanga mikakati ya kupata nomination kubeba msalaba wa Republican. Hapa ndipo alipojikita zaidi akitegemea vita kubwa zaidi. Na kweli ilimtoa jasho hasa akikumbuka changamoto alizozipata mwaka 2008 kabla ya kujitoa. Ufuasi wake wa Mormon ulikuwa kikwazo hata kwa hardliner republicans.

Baada ya kupata nomination ndipo akaanza kupiga campaign za nchi. Nafikiri yeye na timu yake wamefanya kazi ya ziada kuweza kumshinda Obama ambaye hakuwa na kazi kubwa ya kujiandaa kwenye nomination ya Democrats. Sitashangaa kama 2016 Romney atakuwa Rais wa Marekani.
 
Machozi ya Obama ndo ilikuwa zuga kubwa, wamarekani walidanganyika na vilio vya Obama kwenye campaign zake za mwisho..! Walidhani anawalilia wamarekani kumbe alikuwa anaulilia urais
 
Huu ni mjadala wa kubadilishana mawazo kitaaluma. Hivyo kama unataka kumpa ongera Baraka Obama, nakushauri fanya hivyo kwenye thread nyingine.

Jana nilipokuwa naangalia matangazo kutoka katika Boston na Chicago niliona vitu viwili muhimu. Kitu cha kwanza kwenye kambi Romney waliokuwa wanasubiri matokeo wengi walikuwa wazee na wazungu. Kitu cha pili katika kambi iliyokuwepo Chicago, wengi walikuwa ni vijana na vilevile kutoka jamii mbalimbali.

Ukichunguza vitu hivi viwili kwa makini, unaweza kusema kuwa Obama amechaguliwa sio kwa sababu anamzidi Romney kiutendaji wa kazi. Amechaguliwa kwa sababu ya muundo wa jamii zilizopo Marekani. Hii ni sababu moja na zinaweza kuwepo zingine.

Ningeomba tuzichambue hizo sababu hili tujifunze.

Z10
Z10, wanabodi wamechangia hoja nyingi za msingi zilizosababisha Romney ashindwe. Naomba kuongezea muonekano wa Obama na mkewe pia ulikuwa na mvuto kwa wapiga kura. Ile familia ina mvuto fulani ambao umeifanya kukubalika na Jamii apart from sera.

Pia mke wa Obama amekuwa kivutio kwa Wanawake na wanaume pia. Nyota zao zinangaa Z10. Pia mchango wa Gaijin pia una maana, usisau TZ wengi walihagua Rais handsome, ukiuliza sera wanakwambia tabasamu lake sio la kawaida nk Wakati wa Mhe. Mkapa ilibidi mwl afanye kazi ya ziada. Nakuwaammbia huyo mzuri mkanywe nae chai.

Mwisho nimependa Mgombea anavyotafuta kura mwenyewe kwa asilimia kubwa na sio kubebwa na mara ohhh wakongwe, Mara ohhh chama n.k TZ we need a president who can stand alone, kwa muda mrefu tunaona watu wakibebana, inatosha.

Queen Esther
 
Machozi ya Obama ndo ilikuwa zuga kubwa, wamarekani walidanganyika na vilio vya Obama kwenye campaign zake za mwisho..! Walidhani anawalilia wamarekani kumbe alikuwa anaulilia urais
Huu ni uchambuzi au pumba? Anyway, Romney kashindwa kwa sababu nyingi tu, baadhi zikiwa ni:-
  1. Kutokuwa na msimamo katika masuala muhimu. Ikumbukwe kuwa Romney alikuwa na misimamo tofauti tangu kwenye Republican primaries na baadaye kuibadili baadhi ya misimamo hiyo baada ya kuteuliwa na Chama chake. Hii ilionyesha ni jinsi gani anaweza kubadilikabadilika ili mradi apate kura
  2. Hakujishughulisha na watu masikini na wenye kipato cha kati. Sera zake za kuwapa punguzo la kodi matajiri eti wawe na uwezo wa kupanua ajira kwa wananchi wenye vipato vya chini na kati zilimponza. Hii Top-down approach ya Romney kwenye ku-solve matatizo mara nyingi haiwi na mafanikio kama ile ya Bottom-up approach ya Obama. Obama alipigania watu wenye vipato vya chini na kati na kuahidi kuwabana matajiri wakubwa ambao kwa kawaida hawahitaji msaada wa unafuu kutoka serikalini
  3. Ubaguzi. Ikumbukwe kuwa Romney alionyesha ubaguzi wa wazi sana na yeye, Republicans pamoja na timu yake ya kampeni hawakutaka, kujali wala kuheshimu uwepo wa matabaka mbalimbali na mchanganyiko wa watu wa Marekani (American population diversity). Wao waliamini kuwa only The Whites ndio walengwa wa siasa za Marekani na kuwapuuza minorities (ambao sasa sio tena minorities) kama vile Hispanics, African Americans, Latinos, etc. Pia, Romney hakuweza kuwavutia sana wanawake hasa lilipokuja suala la mimba na afya ya uzazi.
  4. Alichelewa sana au hata kutoifanyia kazi kabisa mikakati yake mizuri kama vile early get-out-to-vote. Wafuasi wengi wa Democrats huhamasishwa kupiga kura mapema na hata Obama mwenyewe safari hii alipiga kura mapema kama njia ya kuhamasisha wafuasi wake. Romney hakuweza sana na hata alipohamasisha haikuwa kwa kiwango kikubwa. Matokeo yake, Republicans wengi walipumbazwa na ile Debate ya kwanza na kuamini kuwa Mitt Romney angeshinda na kusahau kuwa ni kura tu (na sio ukosoaji au uongeaji mzuri wa mgombea) ndizo zinazompa ushindi mgombea.
  5. Hata wanaomsifu Romney eti angeweza kufufua uchumi wa Marekani kisa tu ni mfanyabiashara maarufu, walishindwa kuonyesha (ku-link) ni namna gani angeweza kufanya hivyo akiwa White House. Kuendesha biashara binafsi ni tofauti na kuendesha nchi! Kwenye midahalo Romney mara kadhaa alimkosoa Obama kwa kuongezeka kwa deni la Taifa na ukosefu wa Ajira. Alipoulizwa ni njia zipi angezitumia ktk kupunguza na hata kuondoa deni hilo hakuwa na specifics. Kuwa bingwa wa kukosoa tu pasipo kutoa njia za kutatua matatizo husika kulimuonyesha Romney kuwa ni mtu wa kuota tu "and hence Romnesia" pasipo kuwa na uhalisia.
Hayo na mambo mengi ni baadhi tu ya sababu za Romney kuangukia pua licha ya fedha nyingi (zaidi ya $ 1billion) kutumika katika kampeni zake.
 
Demography ndo jibu la kila kitu ndugu zangu.
Whites 59% romney,obama 39%,
Blacks 77% obama,19% romney
Hispanics 73% obama,21% romney
Mfano dhahiri ni Florida,kati ya new voters laki saba ,laki sita wamempa obama na kashinda kwa tofauti ya kura 50,000.
Habari ndo hiyo na usishangae Rais ajaye wa marekani akawa anaitwa mithun chakraboty au fing peng hang!
 
Kambi ya Obama ilionekana kuungwa mkono na watu wa asili tofauti ukilinganisha na kambi ya Romney. Ni wazi kushindwa kwa Romney kumetokana na kuungwa mkono na wazungu wengi tena wazee ambao idadi yao katika ujenzi wa nchi ni mdogo. Sera zake za ndani hasa za uchumi was fine ila sera za nje hazikushawishi wapiga kura.

Muwaha,

Siwezi kusema mchango wa waliopigia Romney ni mdogo kwa sababu white, especially old men, bado wana-control uchumi wa nchi. Na ukiangalia kwenye michango utaona Romney alipata pesa nyingi kutoka kwa watu wachache matajiri. Wakati Obama alipata pesa nyingi kwa kuchangiwa kidogo kidogo na watu wengi.
 
Ndugu yangu Zakumi, heshima yako sana bro! loong time!:

- Romney ameshindwa kwa sababu zile zile zinazomfanya Giuliani Popular Mayor wa zamani wa New York ashindwe kwua Rais kila anapogombea,

- Republicans hawachagui Rais aliyewahi kuwa Gavana au Mayor wa East Coast, mikoa ambayo inafahamika sana kwa ku-support Gay Marriages, Food Stamps, Abortions na Unions. Hizi ni sumu kwa Conservatives na ndio maana Mayor wa sasa wa New York pia anaogopa kugombea Urais.

- Huwezi kushinda Urais wa USA as Republican bila 100% Support ya Conservatives, including watangazaji wa Radio Rush Limbaugh, The Great One Mark Levine na Sean kutoka ABC RADIO, hawa wote hawakuwa wanaamuunga mkono Romney.

- Again ni vigumu sana kwa Republican asiyetokea South States kushinda Urais wa USA, Romney Republican kutokea Boston, alikuwa ameshashindwa hata kabla ya uchaguzi kuanza, kulichomfikisha hapo alipofikia ni mapesa yake mengi sana, halafu pia Dini yake Romney nayo ni tatizo kubwa sana Wamarekani hawachagui a Mormon ambayo ndio dini yake kuwa Rais wao.

Media ya USA ilikuwa inajua toka day one kwamba Romney hashindi, lakini kwa sababu they had to make money wakaanza uongo mwingi wa kuwa Race is tight, ndio maana ya Capitalism ni kutengeneza faida popote pale kwa kugeuza geuza habari ingawa ukweli unafahamika.

- The best Candidate Republicans had kumshinda Obama, alikuwa ni Christie Chrstie Gavana wa New Jersey, ambaye hata kambi ya Obama ilishaanza kumshambulia bila kutangaza kwamba anagombea, lakini akaogopa uwezo wake mdogo wa kuchangisha pesa za uchaguzi, hivyo akakataa kugombea and that was it!!


Le Mutuz!!

I am doing fine bro.

Umeleta mtazamo mwingine mzuri katika uchambuzi huu. Romney alikuwa Governor Massachusetts, amezaliwa Michigan, na ana maskani New Hampshire. Paul Ryan anatoka Wisconsin.

Wameshindwa katika majimbo haya yote manne ya nyumbani: Massachusetts, Michigan, New Hampshire and Wisconsin. Hii inaonyesha kuwa tiketi hii ilikuwa na ulakini fulani kama unavyoonyesha.

Katika uchaguzi huu, sifa nyingi alizofanya Romney kama Gavana wa jimbo zake zilikuwa ni kigezo kikubwa kwake kwa conservatives. Na kwenye kampeni akawa anazungumza sana sifa zake kama mfanyabiashara na kuacha sifa za ugavana,
 
Watu wengi wa race nyingine wanawaogopa Republican sababu ya sera zao za immigration pia. Ukiangalia sana watu wahamiaji wamepiga kura kwa wingi kumchagua Obama kuliko Romney.
 
Every vote counts. Sasa wale wasiotaka "siasa" badala yake wanachagua mgombea kwa muonekano wake, lazima wafikiriwe kama Dr.Slaa anataka kura zao

*Sayansi ndio iliyosema kuwa wapo watu wanaochagua kwa muonekano, sio maneno yangu
.

Gaijin,

Watu wanakataa sayansi lakini kuna ukweli ndai yake. Kuna uchunguzi wa kina unaosema kuwa democracy inaongozwa na watu wachache. Hawa ndio ndio wanaotushawishi tumpigie kura mtu fulani.
 
Mwanangu Zakumi hata matokeo yanaweza kuwa sababu na sababu ikawa matokeo muhimu vyote ni sababu.
 
sababu kubwa ya Romney kushindwa ni kutokana na matamshi yake kuwa asilimia 47% ya wamarekani wanaishi kwa kutegemea ruzuku/msaada wa serikali.

Hivyo watu wengi walio maskini walikasirika na kumuona Romney kuwa akichaguliwa atawapendelea matajiri na kuwaacha maskini wakitaabika kwa kuwafutia posho za serikali kama ilivyotokea kwa chama cha sasa kinachotawala Uingereza. Hili ndilo pekee lililomwangusha.

Lakini laiti wamarekani wangechambua kwa umakini kauli yake wangejua alikuwa hapendezwi na umaskini wao katika taifa kubwa kama lile na angefanya bidiii kuwapa fursa ambazo zingepunguza kiwango cha umaskini wao na utegemezi wao kwa serikali.

Hili ndilo tatizo la wapiga kura wengi wanaofikiria kushiba leo bila kujali kesho yake itakuwaje?


Tatizo Romney alishindwa ku-connect na watu. Kampeni nzima alikuwa anasisitiza kuwa kama matajiri hawalipi taxes kubwa basi wataongeza nafasi za kazi. Kuna ukweli ndani yake lakini wapiga kura wengi sio matajiri. Hivyo delivery ya speeches zake zilitakiwa kuwa makini katika suala hilo.
 
Wanawake, wanawake, wanawake......hawa dada/mama zetu walimkubali Obama na wakamkataa Romney na kama kawaida wakapata walichotaka. Kura zao zinaweza patikana au kupotezwa kwa vitu vidogo sana (mara nyingine visivyo na mashiko kiakili ila kihisiatu).

With apology, women are probably the most unpredictable species curremtly on earth!
 
Romney only won a few groups this election...notably whites, men and church goers. And as a share of the total electorate, two of those groups are shrinking.
The Republicans has real problems...they can't win without the racists or the bible thumpers, but the former is killing them with minorities [a group that Obama did better with this cycle] and the latter's fixation on gay marriage is turning off the under 30's.

For all the talk about how Hispanics are social conservatives, among non-Catholic evangelicals, the Republicans can't even get 50% of that group's vote.
 
Sababu kubwa ni Independents kumsupport Obama zaidi ya Romney.

Pili, like Palin, Paul Ryan was a polarizing figure.Behind a moderate (flip flopper) Republican, just as Mcain was a moderate.

Tatu, the best campaign team ever assembled ... Dave Axleroid ameorganize strategy nzuri sana kwa kupigania suburban middle class voters. Hasa suburbs za swing states campaign ya Obama ilikuwea intense.Na alicapitalize on women too!! especially kwenye contraception ambayo ilikuwa a big mistake for republicans.Instead of insisting on abortion issue wakaenda far to contraception .... that wasn't smart na Obama camp wakaitumia.

Kwa mfano, Obama amecapitalize softer stance ya Raul Castro na kurahisisha utumaji hela, cell, phones na laptops Cuba. Pia uwezekano wa kusafiri kwenda kuona families Cuba ... hii imedilute ukali wa Miami cubanos (ukizingatia baadhi ya hawa immigrants wana allegiance to kennedies/dems based on bay of the pigs na pia watoto wao kukua na kuchukua a more liberal stance) Hii imemfanya angalau aweze kuchukua Florida.

Also, Obama campaign kama kawaida was full of community organizers ... ambao walitumia mbinu ya ku-mobilize Hippies kwenye toss up states kama za wisconsin capitalizing on Scott Walker's anti union stance....
Colorado ....weed.
Minnnesota gay rights. They almost got rid of Michelle Bachmann.
Pennyslvania na Ohio were easily won through their increased urbanization and improved middle class suburbs pamoja na immigrants wakatumia Auto bail out na voter supression bills as a platform.

Kwa hiyo generally, repubs and dems are fifty fifty, but if you capitalize on some issues that are at state level you are likely to get the toss up states., Thats what the Obama camp did..
 
Back
Top Bottom