Kushindwa Kwa Romney: Nini Sababu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kushindwa Kwa Romney: Nini Sababu?

Discussion in 'International Forum' started by Zakumi, Nov 7, 2012.

 1. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Huu ni mjadala wa kubadilishana mawazo kitaaluma. Hivyo kama unataka kumpa ongera Baraka Obama, nakushauri fanya hivyo kwenye thread nyingine.

  Jana nilipokuwa naangalia matangazo kutoka katika Boston na Chicago niliona vitu viwili muhimu. Kitu cha kwanza kwenye kambi Romney waliokuwa wanasubiri matokeo wengi walikuwa wazee na wazungu. Kitu cha pili katika kambi iliyokuwepo Chicago, wengi walikuwa ni vijana na vilevile kutoka jamii mbalimbali.

  Ukichunguza vitu hivi viwili kwa makini, unaweza kusema kuwa Obama amechaguliwa sio kwa sababu anamzidi Romney kiutendaji wa kazi. Amechaguliwa kwa sababu ya muundo wa jamii zilizopo Marekani. Hii ni sababu moja na zinaweza kuwepo zingine.

  Ningeomba tuzichambue hizo sababu hili tujifunze.

  Z10
   
 2. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mie naona sababu ni kushindwa tu. Hakuna sababu nyingine. Vinginevyo kama ipo basi anaijua Romney ambaye hata hivyo kwa sasa kwa alivyopigika hawezi kuiweka hapa JF tuijadili. Nampa hongera Romney kwa kuangukia pua. Maana kama angeangukia mgogo huenda angejinyonga. Bloodies as he is, he needs time to recuperate.
   
 3. Du Bois ideas

  Du Bois ideas JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 428
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zakumi,

  Nakubaliana na wewe kwani Obama amechaguliwa na watu wa rangi zote, rika zote, na dini zote ndiyo maana alishinda. Romney wazungu wengi na wazee wengi walifikiri watampitisha. That was a mistake to him. One mistake many goals!!!
   
 4. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #4
  Nov 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Kushindwa ni matokeo sio sababu.
   
 5. s

  saliha Member

  #5
  Nov 8, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  romney kashindwa kwa mambo mengi lakini kubwa ni kuwa sera zake hazikuwavutia wapiga kura ,amefuata siasa katili ya republican ya ubepari mkali bila ya kuzingatia wananchi wanaoumia kwa muanguko wa uchumina kuwafagilia mabilionea na trilionea wazidi kutesa bila ya kulipa kodi stahiki na walala hou kuendelea kubeba mzigo wa kodi huo ndio ubaya wa ubepari ,vita visivyokwisha ambavyo vinasababisha vijana wengi wafe nchi za nje ,tishio la kwenda muflisi na madeni makubwa ya serikali .ndio maana unaona makundi yote haya kumunguka mkono na kabakia na wazee weupe na vijana kiduchu waliomuunga mkono hata wanawake pia kawa udhi kwani nani anafurahi kuona kazi ilio sawa mwanamke analipwa tofauti na mwanamme chini ya mwanamme hata mama clinton na majitambo yake bado kimshara anapata kidogo na mwanaume angekuwa yupo wakati ule.Pia masuala ya kubakwa na upataji wa kinga za kuzuia mimba na dawa za bure za cancer yote haya hakuyaunga mkono wanawake wameona wamedharauliwa na bw Romney. ila amejitahidi sana na kamtoa jasho Mhe Obama.kubwa zaidi na la kujifunza ni maandalizi ya uchaguzi huanza mara baada ya uchaguzi kwisha hapo ndipo alipopata ushindi mnono Obama kwani timu yake ya wagonga milango kuhimiza kupiga kura walimaliza kazi kitambo na iliobakia ilikuwa ni mazoezi tu hdi kufikia ushindi .jee mnajifunza nini wana TZ Clinton kasema its all mathematics
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Nov 8, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,098
  Trophy Points: 280
  Alidhani anaweza kushinda kwa white votes tu...imekula kwake lazima wabadilike ili kuwa inclusive to US' demographic changes
   
 7. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #7
  Nov 8, 2012
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Nakubaliana na points zako nyingi. Naomba tuzungumze kuhusu kijiandaa. Romney amejiandaa kwa uchaguzi huu kwa zaidi ya miaka sita. Miaka miwili ya mwanzo alijiandaa kuwa mgombea wa uchaguzi wa 2008.

  Na baada ya 2008 alianza kujiandaa na 2012. Hivyo kwa kujianzaa, alikuwa kamili. Je kuna kasoro yoyote katika maandalizi yake?
   
 8. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #8
  Nov 8, 2012
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Hiyo ni sababu moja kubwa. Nyingine ninayoona ni hoja yake kuhusu viwanda vya magari. Alikuwa anadai kuwa Obama alifanya makosa kuvisaidia.

  Wiki alitoa Tangazo Ohio, alitoa tangazo kuwa kiwanda cha Jeep kilichopo Ohio kitafunga shughuli zake na kuhamia China. Na akamlaumu Obama kwa kusaidia China.

  Uongozi wa kiwanda cha magari ulikanusha na matokeo yake akaonekana kama anatumia mbinu zozote zile hili apate kwenda white house.
   
 9. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #9
  Nov 8, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Siwezi kuongeza chochote hapo mkuu!! hayo ndio zaidi ya majibu yenyewe. WATU USA WANAISHI KWA MATUMAINI...
  Ila mambo ya kukumbuka ni UONGO wa Romney wakati wa kampeni... labda hapa Watanzania tunaweza kujifunza kitu!!

  Na jambo kubwa kabisa la kutambua NI SERA ZA MAREKANI AMBAZO RAIS HUZIKUTA MEZANI.. Hii inawapelekea wote kufanana ila tofauti yao ni Sawa na PANYA MWENYE MKIA NA ASIEKUWA NAO WOTE HUGUGUNA!!
   
 10. Bu'yaka

  Bu'yaka JF-Expert Member

  #10
  Nov 8, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 851
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 80
  Taaluma gani? Wewe una taaluma gani?
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Nov 8, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,392
  Trophy Points: 280
  Hivi kwa kuangalia kura za watu (forget the electoral college for a minute) ni kweli unaweza kusema sera za republicans hazina mashabiki sana Marekani?
   
 12. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #12
  Nov 8, 2012
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Sera Republican zina mashiko pia ila tu wenzetu hawana tension ya demokrasia kama sisi, kwani mtu akikosa hamna kulalamika na kukataa kusaini matokea kuwa ameshindwa.

  Kama unakumbuka Obama amedeclare kuwa ataonana na mpinzani wake ili aweze kupata mawazo yake ambayo anaona yanafaa kwa maendeleo ya Marekani, vivyo hivyo hataka 2008 alimchukua mpinzani wake kichama Hillary Clintoni ili wafanye kazi pamoja na wameweza.

  So wenzetu hawana tension ya demokrasia kwamba ukikosa uongozi basi umepoteza kila kitu. Kwetu sisi bado sana, nikiwa mbunge nikipoteza leo basi hata ile nyumba niliyokuwa naishi Mikocheni ninaweza nikaiuza.

  Hebu tafakari Maige kukosa uwaziri na nyumba anauza! So what?
   
 13. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #13
  Nov 8, 2012
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Mwanakijiji,

  Swali muhimu sana. Hatuwezi kusema kuwa zina au hazina washabiki kwa sababu moja muhimu. Nao ni election cycles za Marekani ambazo zinatokea kila baada ya miaka miwili.

  Cycle inayojumlisha uchaguzi wa rais kama iliyotokea jana mara nyingi inawatoa minority na vijana wengi kwenda kupiga kura. Lakini Cycle inayojumlisha uchaguzi wa congress pekee yake, minority hawajitokezi kwa wingi.

  Katika uchaguzi wa 2010 ambao haukujumlisha uchaguzi wa rais, washabiki wa Republican ambao wanajitokeza kwa wingi katika cycles zote walitufanya tuamini kuwa Republican party is back. Na kuna wadokezi wa mambo wanaodai kuwa momentum ya 2010 ilimfanya Romney kujichanganya na right wingers in 2012 when he isn't.
   
 14. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #14
  Nov 8, 2012
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Avanti,

  Na wao wako passionate sana na politics. Kuanzia republicans washinde uchaguzi 2010, katika majimbo mengi wamepitisha sheria za kuzuia wapiga kura wasio na vitambulisho. Lengo lilikuwa ni kuwazuia minority ambao wengi wao wanapigia democrat.

  Lakini mpango huo badala ya kuwazuia minority uwafanye wajitokeze kwa wingi. Hivyo kwa kiasi fulani activions za republicans hazikumsaidia Romney.
   
 15. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #15
  Nov 8, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  He wasn't cute enough :whistle:
   
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  Nov 8, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hata Democrats waliposhindwa chaguzi mbili mfululizo kuna watu walidhani kuwa labda huo ndiyo mwisho wao. GOP wana nafasi kubwa sana ya kushinda uraisi 2016
   
 17. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #17
  Nov 8, 2012
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Mine is probabilistic modelling and reasoning.
   
 18. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #18
  Nov 8, 2012
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Nafasi hipo kubwa. Kama uchumi utabakia kuwa mbaya katika second term, basi watakuwa na nafasi kubwa. 2000, GWB alitumia slogan ya compassionate conservatism ambayo ilikuwa nzuri.

  Kama Romney angeweza kupita kwenye primaries kwa kutumia compassionate conservatism, angeweza kuchukua urais. Lakini kwenye primaries alijifanya kuwa unofficial chairman of tea party. Na baada ya kupata nomination akawa anajaribu kurudi kati bila mafanikio makubwa.
   
 19. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #19
  Nov 8, 2012
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  He's a decent guy. But the far-right in the republican party didn't help his cause. Take for example the guy who put this out during the campgain "If it's a legitimate rape, the female body has ways to try to shut that whole thing down."
   
 20. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #20
  Nov 8, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  * Hapo hatujaongelea suala la sauti :shut-mouth:
   
Loading...