Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,340
- 51,900
Kwema Wakuu!
Hakuna Jambo ambalo linanikera kama kumsikia MTU akisema Rais anashauriwa vibaya na washauri wake. Watu wengi wanaosema hivyo ni Watu wasioweza kueleza mambo bayana. Ni Watu wakupindisha pindisha maneno. Wasioweza kutamka nyeusi ni nyeusi na nyeupe ni nyeupe.
Rais kama kakosea sema kakosea. Inatosha. Mambo ya kuanza kumtetea kuwa kashauriwa, sijui washauri wake ni wabaya ni kujaribu kumnasua na Matendo anayoyafanya. Ni kama unajaribu kueleza kuwa Rais Hakosei Jambo ambalo ni Uongo. Hakuna binadamu asiyekosea.
Kusema Rais anashauriwa vibaya kunatoa tafsiri na maana nyingi kama ifuatavyo;
1. Woga na unafiki
Unashindwa kuongea moja Kwa moja kuwa hapa Rais kakosea. Yaani kiufupi unashindwa kuwa mkweli. Watu Wanafiki wanatabia ya kutaka kuongea lakini wakiongea hushindwa kusema Ukweli. Wanakuwa na kiherehere na uchawa au upambe. Huo ni unafiki.
Wakweli wananamna mbili ya kufanya, ni aidha aseme ukweli wote pasipo kufichaficha au kunyamaza Kabisa. Sio kutoa mambo nusunusu.
2. Inamaanisha Rais Hana Akili ya kujua kibaya ni kipi na kizuri ni kipi
Rais sio Mtoto Mdogo, kusema Rais anashauriwa vibaya yaani anadanganywa ni kujaribu kueleza kuwa Rais hana Akili.
Kwamba yeye akipewa ushauri anaufanya pasipo kufikiri. Kiufupi ni matusi kusema Rais anashauriwa vibaya.
Mbali na hivyo ni kujaribu kusema wapo Watu wanaomdharau Rais na kutokumheshimu(kutokumuogopa) ndio maana wanauwezo WA kumshauri vibaya(kumdanganya). Hiyo sio tuu kumtukana Rais Bali kutukana Taasisi nzima ya Urais.
3. Inamaanisha Rais ni Mbaya na muovu
Yaani waje Watu wakushauri hapo twende tukaibe, au tupige dili alafu ukakubali alafu atokee mtu aseme umeshauriwa vibaya.
Kikawaida washauri hutoa ushauri kulingana na MTU alivyo. Ukiwa Mbaya utapewa ushauri Mbaya. Ukiwa mzuri ni ngumu sana washauri kukupa ushauri Mbaya Kwa sababu wanakujua fika. Tena Kwa nafasi ya Rais ni ngumu MTU akakushauri vibaya ilhali anajua wewe ni Mwema.
Haya unashauriwa vibaya alafu unatenda Ule ushauri Mbaya. Alafu wasingiziwe washauri. Huo ni Uongo.
Kikawaida mtu hujaribiwa Kwa tamaa, matamanio yake. Ubaya wa mtu upo ndani ya MTU na ndio unaojaribiwa. Ubaya siku zote hautoki nje kwenda ndani ya MTU. Bali unatoka ndani ya mtu kwenda nje.
Nazungumzia Kwa Watu wazima.
Uovu au uhalifu mara nyingi haunaga kisingizio. Kama ulivyo Wema nao hauna kisingizio.
Ukiona jitu ni jizi, fisadi, jambazi, Muuaji, mbakaji, na dhambi zingine jua Yale ayafanyayo yanatoka ndani yake na hakuna sababu ya nje inayoweza mfanya MTU kuwa Mtu Mbaya.
Ukiona MTU ni Malaya anafanya ukahaba ili ajipatie fedha, umaskini anaosema ndio Sababu, huo ni Uongo. Ila yeye ndani yake ndio Yuko hivyo. Narurudia, ubaya wa mtu upo ndani yake na kamwe ubaya hautoki nje. Vinavyotokaje ni vichocheo tuu.
Hata hivyo, Mtu huweza kudanganywa na kupotoshwa kuhusu Jambo Fulani. Lakini mpotoshaji, na anayepotoshwa wote wanakuwa katika nafasi Sawa pale watendapo Kosa Hilo. Tena mtendaji anakuwa ndiye mkosaji Square.
Chagua Watu waadilifu, Wema na wapenda HAKI.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam