Kusaidia nchi Je Tanzania tuanzishe mfumo wa seneti?

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,609
8,753
Je kwa hili bunge ambalo halisaidii serikali swali ni Je imefika wakati wa kuwa na bunge la seneti?

Bunge hili mfumo unaweza kubadilika lakini mifumo ya wenzetu ni sawa na seneta wawili kwa kila mkoa. Hili seneti litakuwa kama thinktank na viongozi ambao hawana ushabiki badala yake ni wataalamu tofauti. Ili sheria zipite zinatakiwa kupita mabunge yote mawili.

Kwa kupunguza gharama nashauri idadi ya majimbo yapunguzwe kwa bunge la sasa kwa idadi sawa. Mfamo kwasasa kama sijakosea tuna mikoa 31 hivyo kutakuwa na masenta 62. Nashauri kuwe na maseneta 70 kati ya hao
Group la kwanza: maseneta 62 wa kuchaguliwa kutoka mikoa yote Tanzania bara na visiwani
Group la pili: maseneta 8 kutoka makundi maalulu yasio ya kisiasa (1) Walemavu (2) Wafanya biashara (3)Diaspora (4) TLS ya wanasheria (5) Chama cha Madaktari wa binadamu (6) Chama cha wakulima (7) Mtaalamu wa mambo ya nje na uwekezaji (8) mwakilishi mmoja wa majeshi yetu yote. Hawa watu 8 ni lazima wawe wataalamu tutatafuta njia ya jinsi ya kuwachagua.

Maseneta watakuwa na kinga maalumu hawataweza kufukuzwa kwasababu za kichama au kupingana na Raisi bali kwa kukiua sheria za seneta tu. Masenata watakuwa na kipindi cha miaka 7 na sio mitano na mihula isio zidi miwili ili tusiwe na wanasiasa ambao wanafikira kura zaidi ya maslahi ya nchi. Ukitoka kuwa seneta hauruhusiwi kufanya kazi kwenye shirika lolote linalonufaika na tender za serikalini.

Maseneta wataruhusiwa kuanziasha sheria mpya au uboreshaji wa sheria zilizopo lakini ni lazima yaende kwenye bunge yapite na Raisi akubali ku sign. Lakini vilevile sheria mpya za serikali zitakuwa zinapitia kwenye seneta kupata kura na kurekebishwa kabla ya kwenda kwenye bunge. Pamoja na kuwa maseneta ni wawakilishi lakini wanafanya kazi kama maseneta wa nchi nzima na wanatetea nchi zaidi ya mikoa yao.

Seneti vilevile litakuwa na kazi ya kohoja majaji wa mahakama ya rufaa, wakuu wa vyombo vya ulinzi na wakuu wa vyombo vya ulinzi na nafasi nyingine kama kurugenzi za mashirika nyeti ya serikali. Kazi kubwa sio kuhoji tu lakini kufanya uchunguzi wa kiundani kuhakikisha kiongozi apelekwi sehemu ambayo atakuwa mla rushwa au kijinufaisha yeye na sio nchi. Vilevile kiongozi ripoti yake na mwenendo wake kutoka kwa vyombo vya kiuchunguzi itawakilishwa
 
Je kwa hili bunge ambalo halisaidii serikali swali ni Je imefika wakati wa kuwa na bunge la seneti?

Bunge hili mfumo unaweza kubadilika lakini mifumo ya wenzetu ni sawa na seneta wawili kwa kila mkoa. Hili seneti litakuwa kama thinktank na viongozi ambao hawana ushabiki badala yake ni wataalamu tofauti. Ili sheria zipite zinatakiwa kupita mabunge yote mawili.

Kwa kupunguza gharama nashauri idadi ya majimbo yapunguze sawa na majimbo ya seneti hii.
Naunga mkono hoja
P
 
Kusaidi hii nchi nikuionda ccm kwanguvu na kuanza upya.
 
Back
Top Bottom